Kati ya Ford Ranger Double Cabin na Land Cruiser Double Cabin, lipi ni gari bora zaidi kwa kazi za "porini"?

Hayo magari uliyochagua yanafanana sana performance barabarani japo uimara
unatofauti. Mfano wa tofauti;
1. Ford ranger ina Luxury finishing (ndani na nje)
2. Ford Ranger - spare zake ni ghali na chache utapata hapa nchini nyingi ni hadi uagize
3. Driving yake ni luxury na unaweza kuweka 4wheel ukiwa ndani bila ku lock kwanza kwa nje)

Landcruiser- Pickup
1. Ni gari imara sana (Engine ya 1HZ ni moja ya engine bora sana (heavy duty)
2. Inatengenezeka kwa urahisi kwasababu mafundi wa kwetu wamezizoea
3. Spare zipo zote hapa Nchini kwa kuwa ndiyo magari yanatumiwa kwa kazi za utalii
4. Bodi yake ni rahisi kuibadilisha unavyotaka

Kwa ushauri wangu; chukua Landcruiser na unaweza kuendesha wewe hata mjukuu akaiendesha
 
🙏🙏🙏
 
Nenda na ford hizo land cruiser za kizamani mkuu.
 
Embu acha uongo ndugu,nina ford mwaka wa nne sasa,spea zakumwaga na wala sijawahi kuagiza nje,usimtishe jamaa spea ni bei chee mno ,msidanganye watu humu
 
Kwa kuwa umesema itabeba mizigo midogo chukua Ford ipo comfortable, japokuwa cruiser haina mpinzani ila ni kama umepanda punda
Wakuu sina uzoefu sana na magari ila kuna hizi gari za land rover 110, japokuwa zimesitishwa kutengenezwa lakini nahisi ni gari ambalo liko akilini mwangu tokea zamani.

Mwenye ujuzi naomba anisaidie faida na hasara za kumiliki hili gari.

Je katika kupambana na mazingira magumu linaweza kushindana na magari kama land cruiser?.

Nimefuatilia sana kuhusu upatikanaji wake sasa hivi umekuwa adimu sana. Je kwa nchi kama south Africa linaweza kuwa adimu kama ilivyo kwa tz? Ahsante.
 
Ford ranger ni mixture ya luxury and utility hivyo hautachoka sana kama utaendesha kwa muda mrefu haswa kwenye barabara korofi. Landcruiser ni utility vehicle, haina luxurious comfort yoyote ila ni gari ya kazi na ndiyo maana hata baadhi ya majeshi huitumia kama combat vehicle mfano darful, somalia n.k.

Hivyo, kama shughuli zako ni kazi kazi kama site Landcruiser is the best choice ila kama at times utahitaji kutumia kama usafiri wa hapa na pale basi ford ranger is the best choice.
 
Acha kufananisha LC na magari ya kibishoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…