Kati ya hawa mmojawapo anaweza kuwa Rais 2025

Kati ya hawa mmojawapo anaweza kuwa Rais 2025

mwigulu na januari ni rais wa wapi?

uwezo wa januari ni kuwa waziri.

mwigulu hata ubunge hafai nawashangaa wanaomchagua.
 
Umemsahau Dr chrispin Manyonyi huyu anatajwa sana katika kufanya kazi zake kubwa za kufichua mafisadi kwa umahiri mkubwa!!
 
Kwanza poleni na majukumu, pia poleni na misiba ya wazee wetu, misiba ambayo inahisiwa ama kuhusishwa moja kwa moja na Covid19. Ama hakika ugonjwa huu upo hivyo tuendelee kuchukua tahadhari zote kama tunavyoelekezwa na wataalamu wa afya.

Turudi kwenye mada

Inasemekana sasa hivi kambi mbalimbali tayari ziko kazini kuhakikisha hazifanyi kosa na mtu wao anapenya na kuwa rais wa awamu ya sita. Harakati hizi zinaendeshwa kwa usiri sana ili kuhakikisha mkubwa hastuki hasa ukizingatia kwamba jamaa hataki makundi kwani anaamini kuwa kwa namna moja ama nyingine yataharibu utendaji kazi wa serikali.

Watu wenyewe naowapa karata yangu ni hawa:

1. Hussein Mwinyi
Sababu;
a) Hana makundi
b) Anafanya kazi zake kwa umakini mkubwa toka akiwa waziri wa ulinzi mpaka sasa ambapo ni rais wa Zanzibar
c) Ana uhusiano mzuri marais wote wastaafu walio hai na pia zinaiva na rais aliyeko madarakani. Huyu nampa asilimia 80 za kutoboa.

2. Kassim Majaliwa
Sababu;
a) Anaendana kihulka na rais aliyeko madarakani
b) Anajitahidi kufanya kazi kwa bidii na hilo limetokea kuwavutia baadhi ya Watanzania.
Huyu nampa asilimia 20 za kutoboa na anaweza kutoboa iwapo tu Mwinyi ataharibu hapo katikati.

Hata hivyo kinyang'anyiro hicho kitanogeshwa na watu wafuatao;
1. Mwigulu Nchemba
Huyu anautamani sana urais toka 2015

2. January Makamba
Huyu toka aambiwe na marehemu Ruge kuwa anastahili kuwa rais basi muda wote anakiwaza cheo hicho na anafanya kila kinachowezekana kukipata cheo hicho.

3. Samia Suluhu
Huyu anaweza kuingia ili kujaribu bahati yake huku akitegemea sapoti kubwa kutoka kwa akina mama.

4. Bernard Membe
Huyu hisia zangu zinanituma kuwa aturudi kundini (CCM) kisha atajitosa kwenye ulingo.

5. Orodha itakuwa kubwa zaidi, si ajabu hata akina Makonda wakajitosa

Mwisho:
- Upinzani sijauweka kwasababu kwa hali ilivyo sidhani kama unaweza kutoboa.

- Lolote linaweza kutokea, anaweza kuja mtu asiyetarajiwa kabisa.

- Haya ni mawazo yangu binafsi, mi ni mfuatiliaji wa siasa zetu japo sina chama.

* Nawatakieni majukumu mena.
Ondoa namba 2 na namba 4 hapo juu nisije nikatapika.
 
Umemsahau Dr chrispin Manyonyi huyu anatajwa sana katika kufanya kazi zake kubwa za kufichua mafisadi kwa umahiri mkubwa!!
Huyu yeye yuko wapi? Sijawahi kumsika. Weka taarifa zake hapa angalau kwa uchache watazania wapate kumfahamu
 
Siku Mwigulu akiwa Rais, sio kuwa tu watu watalimia meno kama ilivyokuwa kwa Magufuli, bali wataongeza kwa kufanyia palizi na kucha, na kumwagilia kwa machozi ....
 
Mwigulu ni dikteta afai 2025,ni zamu ya muislamu Mwinyi au Majaliwa Hawa Wana hekima na busara,utu, uvumilivu.Makamba,Jafo hazina ya baadae.Membe kwisha habari yake, bashite ni mfungwa mtarajiwa.
Mwislam wa nn? Katiba haina hizo zamu
 
Huyu yeye yuko wapi? Sijawahi kumsika. Weka taarifa zake hapa angalau kwa uchache watazania wapate kumfahamu
sema wewe upate kumfahamu watu wote wanamjua ila wewe wa kijiji.

Ili uka mtest kichawi au!!!
 
Atakaeweza kupeperusha bendera ya CCM ni Dr Msukuma tu. Na atashinda asubuhi kweupe.
 
Back
Top Bottom