Vision ya Nyerere ilikuwa kuingunisha Afrika kama muungano wa North America. Aliona umoja ndiyo utakaoleta maendeleo.
Alitumia resources nyingi katika ukombozi wa bara la Afrika. Siasa za ujamaa hazikuleta tija pia vita ya Kagera iliturudisha nyuma sana.
Hiyo ndio kufaill yenyewe.
Ukiingia kwenye Vita bila kuwa na sababu kama nchi utaishia kupata hasara.
Afrika Kusini walosaidiwa Leo wanawaua waafrika wenzao Hadharani.
Zimbabwe leo imekua ni nchi maskini ya kitupwa.
Viongozi wa Afrika walikurupuka Kwa sababu waliishi na wazungu,wakasomeshwa na wazungu, wakaonja raha za wazungu na wakatamani viti walivyokalia wakoloni, badala ya Kutamani maendeleo ya wananchi.
Ndio maana waliendelea kutumia sheria na katiba za wakoloni kuwatawala waafrika wenzao kikatili kuliko Wazungu. Kabla ya Kile kilichoitwa Uhuru kule Uganda hapakua na Maiti zinazoelea baharini Kwa kuuawa na vyombo vya Dola.
Baada ya Uhuru Kila mmoja alijali madaraka yake kwanza.
Kwame Nkrumah alipotaka Nchi za Afrika ziungane alipingwa na waroho wa madaraka ambao walitumiwa na Mabeberu Kwa maslahi ya Wachina ,Warusi,na Wamagharibi bila kuangalia Maslahi ya Waafrika.
Baada ya Uhuru hapajawahi kuwa na mijadala ya pamoja ya wananchi inayofanyika kwa Amani ,umoja na Kwa Uhuru kujadili mustakabali wa Nchi zao zaidi ya kuburuzwa na Watawala Kwa sheria kandamizi.
Watawala waliwatisha watu na kuifanya jamii ya Kiafrika ione siasa Afrika ni kazi ya hatari sana inayohitaji watu wakatili, wasiojali,waongo,washirikina ,walaghai,Wabinafsi,wanafiki n.k wakati huo huo watawala wakiwa wanaogopwa kuliko Mungu.
Hofu ya waafrika iliyojengwa na watawala baada ya Uhuru ilififisha uwezo wa kimaarifa na ubunifu.
Wanafunzi waliwaogopa walimu kuliko hata polisi, unategemea kuwa na taifa lenye wasomi huru kweli!!