Kati ya haya makundi mawili, ni nani anakula maisha ya kifahari na kitajiri?

Kati ya haya makundi mawili, ni nani anakula maisha ya kifahari na kitajiri?

Aigle

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2020
Posts
1,540
Reaction score
7,973
Kwa sasa chukulia makundi haya mawili, kundi la kwanza ukiwaweka watu wa aina ya Kitenge, Mwijaku, Baba Levo na mwanasiasa mmoja, na kundi la pili ukawaweka wasomi wenye digirii na ambao hawajibia mitihani au kununua vyeti watatu tena wenye HIGH CLASS za vyuo vikuu nchini.

Je, kundi gani kati ya hayo mawili kwa sasa yana pesa, yanakula maisha ya kitajiri na ya kifahari? Kundi ambalo linaweza kununua gari kwa cash milioni 500 kama tano, au kujenga nyumba ya Bilioni 1..

Je kwa sasa elimu muhimu ni wewe kujua kusoma na kuandika tu?

Je "connection" ndio kila kitu?
 
Je kundi gani kati ya hayo mawili kwa sasa yana pesa, yanakula maisha ya kitajiri na ya kifahari? Kundi ambalo linaweza kununua gari kwa cash milioni 500 kama tano, au kujenga nyumba ya Bilioni 1..
kwa uliowataja hakuna wa kujenga nyumba ya b1 wala hakuna wa kununua gari la 500m kwahyo toka usingizini ukafanye kazi maisha ya mtandaoni yasikupum aze utakojoa kitandani
 
Hapo umeelezea watu wa aina 3
Kuna wenye tabia za kike/umbea/ushoga
Kuna mwizi wa mali za umma.
Kuna msomi anayeishi maisha yake kwa elimu yake.

Chagua moja.

Ni sawa na kuniuliza mbona kuna watu wanacheza pornograph na wana pesa kuliko waliosoma?

Jibu unalo.

Kumbuka kuwa na elimu sio kuwa tajiri. Ulishasoma historia ya Nicola Tesla? alikufa masikini sana chumba namba 3327 hotelini New York akiwa na umri wa miaka 86, mwili wake ulipatikana siku mbili baadae akiwa ameweka alama ya "do not disturb" kwenye mlango ndipo muhudumu wa hotel akaona apuuzie alama hio na kuingia ndani ndipo kumkuta Tesla amefariki.

Alikuwa mwanasayansi mkubwa aliyeleta mapinduzi makubwa tokana na vumbuzi zake kwenye AC motor, Alternating current n.k but he died dirty poor.....

Leo hii billionaire mkubwa duniani Elon Musk ameiita kampuni yake Tesla.
 
Kwahio mkuu hawa watoto wetu tukae nao na tuwape hizo option mbili na matokeo yake wachague waende wapi, kuliko kuwapa matumain hewa kwamba watafanikiwa sana kiuchumi na kipesa maishan tena hapa tanzania kwa kupata high class chuo kikuu
 
Back
Top Bottom