Ubest wa lugha unaangaliwa kwa wingi wa uzungumzwaji wa watu au kwa ubora wa lugha ? Ila kama kwa wingi hapo sawa ila kwa ubora wa lugha, aisee hakuna lugha bora hapa duniani na kamili kielimu kuzidi lugha ya KIARABU, kuanzia kihistoria,udhibiti,na fani zake, yaani hakuna.
Hawajui hawa,
Historia ya Kiswahili imeanza takriban miaka 1000 iliyopita kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki.
Neno Swahili lina asili ya Kiarabu: Sahil ina maana ya pwani; sawahil ’’as-sawāhilī’’ (السواحلي) ni wingi wake kwa kumaanisha yote yanayohusiana na pwani, watu au utamaduni wa eneo la pwani.
Mwanzo katika miji ya pwani
Kiswahili kilianza kama lugha ya miji na mabandari ya biashara ya kimataifa kwenye pwani ya Afrika ya mashariki.
Tuna historia jinsi gani miji kama vile Kilwa, Lamu na mingine kadhaa ilianzishwa na wafanyabiashara Waarabu au Wajemi waliooa wenyeji. Idadi ya wahamiaji kutoka Uarabuni haikuwa kubwa sana, hivyo lugha ya wenyeji ilitumika kila mahali ila tu maneno mengi yameingia kutoka Kiarabu. Kwa ujumla Kiswahili kina maneno yenye asili ya Kiarabu kati ya 30-40%, hali inayokaribia kiasi cha maneno yenye asili ya Kilatini au Kifaransa katika lugha ya Kiingereza.
Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa wa Kiafrika na wa Kiislamu ukajielewa kuwa sehemu ya dunia ya Uislamu. Hivyo Kiswahili kilizaliwa kuwa lugha ya Kibantu kilichopokea maneno mengi ya asili ya nje.
Kiswahili kiliandikwa muda mrefu kwa herufi za Kiarabu. Haya ni matini kwenye sanamu ya askari huko Dar es Salaam, Tanzania. Yanasema: "Huu ni ukumbusho wa askari wenyeji Waafrika waliopigana katika Vita Kuu."
Lugha hii ilionekana kuwa na ustaarabu wa Kiarabu zaidi, yaani Uislamu.