Kati ya Kimara, Kigamboni na Kinondoni wapi ni bora zaidi kuishi?

Kati ya Kimara, Kigamboni na Kinondoni wapi ni bora zaidi kuishi?

MaT2B

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2019
Posts
658
Reaction score
2,081
Habari za mida hii wakuu

Poleni na Majukumu,

Poleni pia na maswaibu ya DPworld

Nimepata kibarua maeneo ya Posta.
Kwa sasa ninaishi Kibaha.

Hivyo nataka nihamie sehemu ambayo nitapunguza gharama ya usafiri na muda wa kusafiri.

Maeneo ambayo nashawishiwa ni Kimara, Kigamboni na Kinondoni.
Kati ya sehemu hizi ni wapi patakuwa bora zaidi.

Ukizingatia

Gharama ya chumba( <100K/month)
Usalama.
Urahisi wa kufika eneo la kazi(posta)
Hali ya hewa(joto).


Asanteni.

AbaMukulu Accumen Mo adden Aelknes Africa Yangu Aaliyyah Half american
Mabula Msirikale Mwachiluwi Saint Anne @Mwifa National Anthem Mzee wa kupambania mzabzab rikiboy
mshamba_hachekwi @
 
Tatizo la huko kigamboni uswahilini Sana , vibaka n.k , na maeneo ya kishua Kwa kigamboni yapo mbali Sana na posta na usafr ni ghali , binafs nashauri Kimara , vyumba vingi tuu vipo karbu na road , dk 15 au 20 ashafika main road , anapanda mwendo kasi moja Kwa moja
Kimara/ubungo ni best option, unapata nyumba mpya na bei nafuu hasa kimara
 
Gharama ya chumba( <100K/month)
Usalama.
Urahisi wa kufika eneo la kazi(posta)
Hali ya hewa(joto).

Gharama ya chumba - Kigamboni na Kimara

Usalama - Kote kuna vibaka haswa wa usiku itategemea umepata eneo gani, maana kuna vitongoji vina vibaka zaidi ya vinginevyo...

Urahisi wa kufika Posta - Kinondoni

Hali ya hewa (joto) - Kigamboni na Kimara

Hivyo tafuta wastani hapo....
 
usidanganywe hao maeneo ya kimara , kinondoni mengi ya uswahili na watu ni wengi kuna wizi wa ajabu na usafiri unajaa sana.

Kama kupanga angalia na ukaribu wa sehemu unafanya shughuli zako ,ila unataka kujenga kigamboni ni best choice maana hata hilo Panton miaka kadhaa halitakuwa na shida sana huko mbeleni .
 
Back
Top Bottom