Kati ya Madiba na Mwalimu nani alikuwa zaidi

blackmweusi

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Posts
241
Reaction score
186
Jamani hiki kitu nimekuwa nikikiwaza kwa muda mrefu sana, hivi kati ya Mwalimu na Mandela nani alitoa mchango mkubwa zaidi?
Kwa fikra zangu nijuavyo mimi, Nyerere alitoa mchango mkubwa sana. Lakini sasa mbona hajulikani na havumi huko nje kama namna Madiba anavopewa sifa? Narudia tena hii ni kwa elimu ya historia niliyonayo na fikra zangu hivo sijaongelea mawazo ya mtu.
Naombeni tueleweshane, ni nani alitoa mchango mkubwa Africa?

Nawasilisha.
Black.
 
Kitu pekee kinachompa credit Madiba over Mwalimu ni ile kufungwa 27yrs na baadae kuwasamehe waliomtesa. Only that
kuna tetesi nilisikia eti jamaa aliachiwa under that condition
ila sijui history vizuri
 
Kitu pekee kinachompa credit Madiba over Mwalimu ni ile kufungwa 27yrs na baadae kuwasamehe waliomtesa. Only that
Na speech zake zinahisia sana kuliko mwalimu
 
Mwalimu ndo Zaidi Huyo Mandela mwenye anatambua Hilo na alikuja Sana bongo kwa ticha kupata madini konki. Ticha levels zake Akina nkwame, marcus Garvey ,
 

Kila mmoja alikuwa zaidi kutokana na sehemu aliyoshiriki
 
Mwalimu ndo mtu pekee aloweza kuwaunganisha watu wengi kwenye makabila tofauti na dini tofauti. Hapa kiswahili kinafanya kazi yake, SA hili liliwashinda, shuleni wana soma kizulu na kixhosa. Huu ni ukabila tosha mpaka kuona kishwahili kinawafaa
 
Jibu alilitoa madiba mwenyewe akiwa anapokea tuzo ya Nehru nchini india.ya kuwa nyerere ni zaidi ya kiongozi.na nimakosa kumlinganisha nyerere na mm.bira nyerere leo mie nisingekuwa madiba huyu mnaempa tuzo hii leo .mm ni zao la nyerere.
 
Mwalimu alitoa mchongo Mkubwa kwa Nchi nyingi hasa za kusini mwa Afrika kupata uhuru hata South Africa ni Moja wapo .Jambo linalo mfanya Mandela kujulikana sana kimataifa ni kutokana Na zile Harakati zake kwa maana zilijulikana Nchi nyingi Duniani hata alipokuwa Gerezani Chini nyingi Duniani zilikuwa zina jitahidi kumtetea ikiwa pamoja Na Tanzania pili alionekana anaonewa . Kwaiyo Dunia nzima ililiangalia jambo hili kwa uzito .ndiyo maana akawa maarufu sana
 
Nyerere ndio zaidi.

Sababu ya Madiba kuwa maarufu kuliko Nyerere ni kwamba Madiba hakuwaondoa watu weupe RSA wala kutaifisha chochote walichokuwa wanamiliki, kitu ambacho kilimpa credit kwa mataifa makubwa (esp. Uingereza & Marekani) na kuonekana kuwa sii m'baguzi. Ila Nyerere alikuwa binadamu wa aina yake aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…