Kati ya Madiba na Mwalimu nani alikuwa zaidi

Kati ya Madiba na Mwalimu nani alikuwa zaidi

Jamani hiki kitu nimekuwa nikikiwaza kwa muda mrefu sana, hivi kati ya Mwalimu na Mandela nani alitoa mchango mkubwa zaidi?
Kwa fikra zangu nijuavyo mimi, Nyerere alitoa mchango mkubwa sana. Lakini sasa mbona hajulikani na havumi huko nje kama namna Madiba anavopewa sifa? Narudia tena hii ni kwa elimu ya historia niliyonayo na fikra zangu hivo sijaongelea mawazo ya mtu.
Naombeni tueleweshane, ni nani alitoa mchango mkubwa Africa?

Nawasilisha.
Black.
Mwalimu alifanya vitu vingi sana kwa ajili ya ukombozi wa Afrika, lkn ipo nguvu kubwa sana ktk kitu kinaitwa msamaha, pale unaposamehe adui zako,mbingu ufunguka na baraka uanza kukuijia juu yako, kitendo alichokifanya Madiba kilimpa mailegy ya umaharufu mkubwa sana duniani.
"Kuna nguvu kubwa sana katika msamaha" wasamehe wrote waliokukosea......
 
Jamani hiki kitu nimekuwa nikikiwaza kwa muda mrefu sana, hivi kati ya Mwalimu na Mandela nani alitoa mchango mkubwa zaidi?
Kwa fikra zangu nijuavyo mimi, Nyerere alitoa mchango mkubwa sana. Lakini sasa mbona hajulikani na havumi huko nje kama namna Madiba anavopewa sifa? Narudia tena hii ni kwa elimu ya historia niliyonayo na fikra zangu hivo sijaongelea mawazo ya mtu.
Naombeni tueleweshane, ni nani alitoa mchango mkubwa Africa?

Nawasilisha.
Black.
Mwalimu nyerere alipewa madaraka mezani yaani uhuru wa bendera ila Nelson Mandela alikaa gerezani gerezani kupigania uhuru wa taifa lake
 
Kwenye nyanja ipi unawalinganisha siasa zao ni tofauti nyerere alijikita kwenye ukombozi wa Africa na kuiunganisha Africa nzima laki tata madiba alijikita kwenye ukombozi wa mtu mweusi na demokrasia ulimwenguni.
 
Kitu pekee kinachompa credit Madiba over Mwalimu ni ile kufungwa 27yrs na baadae kuwasamehe waliomtesa. Only that
Hakuna kitu kama hicho angeweza fungwa hata miaka 50 na kutoka na asingewafanya kitu chochote ni serikari ya de Klerk iliamua kuachana na apartheid na yeye alivo kua president akaamua kuendeleza what he has been fighting for. Mandela has nothing over Nyerere bana!
 
ila mwalimu alitoa mchango mkubwa katika ukombozi wa nchi za Afrika na south africa ikiwemo
alitoa hadi rasilimali za nchi yake ili kusaidia Afrika. He saw the bigger picture
Mwalimu nyerere alipewa madaraka mezani yaani uhuru wa bendera ila Nelson Mandela alikaa gerezani gerezani kupigania uhuru wa taifa lake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania ipo ilipo kwa sababu ya misingi mibovu ya kiuchumi iliyowekwa na mwalimu.

Caring for Africa?? Inatufaidisha nini Leo? Umeskia raia wa south Africa kuzamia bongo kutafuta maisha?? Ni Sisi ndio tunaelekea huko.

Kila unaloshika halishikiki ndani ya Tanzania, na hii ni kukuonyesha kwamba muasisi alikosa maono. Lichama lake alilolianzisha ndio hili mnaliona ilimradi balaa juu ya balaa
 
offcourse mwalimu ni zaidi ya madiba kwanza mwalimu mwenyewe alim coach madiba ss tamgu lini mwanafunzi ashindane na mwalimu wake ..ukisikia sisimizi kumpanda tembo ndio huko. Tz chini ya mwal. tuliwasaidia sana nchi na wapigania uhuru akiwepo madiba,..yaani mwalimu ali risk na kuifanya tz kama chuo cha kuwanoa wapigania uhuru hili lipo wazi..... historia inajua ilo...kuanzia madiba, thabo mbeki, samora masheli, and mention other in southern africa walipita hapa TANZANIA ikiwa chini ya mwalimu.
 
Madiba Anafananishwa Na Nabii Huko South Na Dunia Kwa Ujumla Unajua Kwanini Wamempa Michuano Ya Kombe La Dunia
 
Mchango upi wa mwalimu mkuu Wakuitia nchi ufukara au? Katawala nchi miaka 20 kaicha nchi na watu wajinga na fukara kutoka wananchi wake mpaka seekali yake.
Katika moja ya vitu ambavyo huwa sivielewi toka kwa waTZ wachache ni mawazo km haya. Hivi kweli mtu mwenye akili sawia anawezaje kufikiria jambo kama hili?

Hivi ukiulizwa kuhusu jinsi gani Nyerere alilitia umaskini/ufukara taifa la TZ utaweza kuelezea kwa ufasaha? Tusiwe km sponge
 
Kwani madiba alifanya jambo gani kubwa la kusifiwa, maana maisha yake yote kayatumia kifungoni
 
Sio vizuri kuwalinganisha.
Ila Kamabarage ni kiboko. Alikuwa na mapungufu sana ila alijitahidi.
Chezea mtu anaye come up na ideology yake mwenyewe inayosomwa na vyuo mbali mbali duniani.
 
Mwalimu Nyerere
Amewasaidia Wengi Sana
Nelson Mandela
Samora Machel
Kenneth Kaunda
Na Wengi Wengi Wengine
 
Back
Top Bottom