Kati ya maji ya mvua na maji ya chemchemi, yapi ni masafi zaidi?

Kati ya maji ya mvua na maji ya chemchemi, yapi ni masafi zaidi?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habari waungwana.

Eti kati ya maji ya mvua na maji ya chemichemi yapi ni masafi na salama zaidi.
 
Kama ya mvua yakivunwa kwa njia salama ni mazuri sana.

Ya chemchem pia kama chanzo chake kikilindwa vizuri bila kutupiwa taka yatakuwa Safi.

Ila bora ya mvua muhimu bati liwe safi
Naomba kupata uelewa kidogo, mvua inaponyesha yale matone/maji kabla kufika chini hapo kati angani yanaweza kupata contamination?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maji ya chemchem ndio safi maji ya mvua yakikaa zaidi ya siku 3 yanaweka vijidudu inategemea na bati na chemchem kama chanzo ni kizuri kama vya kijijini.
 
Kwa nchi zetu maji ya mvua ni salama zaidi maana chemichemi hutegemea na kiwango cha kemikali kilichounda udongo au mwamba katika sehemu husika. Ndio maana kuna baadhi ya mikoa wanatumia maji ya chemichemi na mito lakini yanawaunguza meno ila kwa maji ya mvua, hiki kitu si rahisi
 
Maji ys chemchem ndio safi maji ya mvua yakikaa zaidi ya siku 3 yanaweka vijidudu.

Kama maji ya mvua umeyavuna kwenye bati na ukayaacha nje kwa kiasi ni lazma yatakuwa na vijidudu hivyo, kabla ya kuyaweka ndani ni lazma uyachuje kwa kitambaa safi au la, unabidi uyawekee chumvi ili yakae muda mrefu.

Maji ni safi ila yanavyovunwa na kuhifadhiwa ndio tatizo
 
Kama ya mvua yakivunwa kwa njia salama ni mazuri sana.

Ya chemchem pia kama chanzo chake kikilindwa vizuri bila kutupiwa taka yatakuwa Safi.

Ila bora ya mvua muhimu bati liwe safi
Kwa maeneo ya viwanda au ukitokea mlipuko wa volcano, mvua huwa na kemikali nyingi na kusababisha acid rain. Pia angani kuna vimelea wengi, japo si wengi kiasi cha kuwa hatari kubwa.
 
Habari waungwana. Eti kati ya maji ya mvua na maji ya chemichemi yapi ni masafi na salama zaidi.

Hakuna maji safi na salama kati ya aina zote mbili, mpaka pale baadhi ya vitu muhimu vitathitishwa kuwa viko sawa.

1: Maji ya mvua: yatategemea na anga husika dhidi ya uwepo wa moshi, kemikali, vumbi, mionzi ambavyo vyote via uwezo wa kuathiri maji husika.

2: Maji ya chemichemi: hutegemea utunzaji wa ardhi husika kutokuwa na kemikali, mizoga, na uchafu mwingine uwe kutokana na viwanda au ecosystem ambao ni chanzo wa uchafuzi.

3: Madini na specific gravity vinavyokubalika: maji pia huitajika kuwa na milinganyo wa madini mbalimbali ndani yake. Hivyo ni muhimu kujua chanzo cha maji kilipo na madini husika ndani ya ardhi.

NB: Hapa ndio umuhimu wa upimaji wa maji yanayotumiwa na familia au jamii ni muhimu.
 
Mkuu nawezaje kupima maji kama ni salama?
 
Maji ya chemichemi ni bora zaidi hasa chanzo chake kikiwa hakijawekewa takataka.

Ya mvua hata ukinge leo ukiongea kuna hali flani ya utelezi na yanawahi kuweka wadudu
 
Unazungumzianusafi upi?? Maji yamebeba million of bacteria sio ya chemchem lawa kisima yote ni machafu ndio maana unambiwa hakikisha unachemsha maji na kuchuja ili kuondoa vimelea vya magonjwa kwaio maji safi ni Yale yaliochemshwa au kutibiwa Kwa water guard usidanganywe na clear appearance ya maji.
 
Ya mvua ni bora kwa usalama lakini ya chemichemi ni bora zaidi kwakuwa yana madini muhimu miilini mwetu
 
Back
Top Bottom