Kila sehemu uliyotaja ni nzuri sana endapo unafocus na plan zako haitokuchukua miaka mingi kusimama imara isipokuwa kwa uzoefu wangu
Mpanda, pamepoa sana. Mlipuko wa magonjwa na muingiliano na wakimbizi ni mkubwa sana lakini pia usalama wa afya na mali ni mdogo
Ifakara, kipindi cha mvua utapachukia mno maana sio kwa mafuriko yale, pia huduma za afya ni mbovu sana. Joto ndiyo balaa
Gairo, pamepoa sana, wenyeji wana wivu sana, vumbi la pale utalikimbia, mpangilio mbaya wa mji, vyakula havieleweki
Mvomero, nilichoshwa na mafuriko tu ila kila kitu bye sana
Nb:
Pafikirie na Kahama na maeneo jirani na pale ni wilaya nzuri sana na inatoa kimaisha chap tu ukiwa bz na unachokifanya