baada ya kujua kuwa amesaliti damu isiyo na hatia, Yuda alirudiaha pesa kwa waliompa na walipokataa kuzipokea alizitupa hekaluni akaondoka zake na kwenda kujinyonga. Ndipo wahusika wa helalu walizichukua hizo pesa na kwenda kununulia konde (shamba) la kuzikia wageni. ...
njoo kwa YESU uokolewe
Hahaha hahahhha Hizo taarifa umezitoa wapi? au Ni just imagination zako?
lakini biblia inasema kuwa yuda alinunua eneo mwenyewe ndo maana ukisoma kwenye mathayo ametumia neno la kigiriki
ἠγόρασαν (
ēgorasan), ambalo linamaanisha kununua au kufanya biashara moja kwa moja. Katika Matendo 1:18, neno lililotumika kuelezea kitendo cha Yuda ni
ἐκτήσατο (
ektēsato), ambalo linaweza kumaanisha "kujipatia," "kumiliki," au "kupata...
kwahyo wote wanakunaliana alinunua eneo sasa wewe hiyo walinunua Watu wa hekalu umeitoa wapi?
"...καὶ ἀπελθὼν
ἀπήγξατο." (...
kai apelthōn apēnxato.)"...akaenda
akajinyonga."
sasa ngoja tupelekane Darasani kidogo..
Neno la Kigiriki: ἀπήγξατο (
apēnxato) linatokana na mzizi
apagchō, ambalo linamaanisha moja kwa moja
"kujinyonga" au
"kujikaba koo hadi kufa." nikupe taarifa tu kwamba Katika lugha ya Kigiriki, neno hili halina maana mbili, lina maana moja peke yake.
Mathayo alikuwa wazi kabisa kwamba Yuda alikufa kwa kujikaba shingo kwa kamba (strangulation). Hakuna sehemu yyte hapa kwamba yeye kuanguka au kupasuka.
haya twende kwenye matendo
"...καὶ
πρηνὴς γενόμενος
ἐλάκησεν μέσος, καὶ ἐξεχύθη πάντα τὰ
σπλάγχνα αὐτοῦ." (...
kai prēnēs genomenos elakēsen mesos, kai exechythē panta ta splanchna autou.)
"...na akawa ameanguka kwa
kichwa/kwa mbele,
akapasuka matumbo, na
matumbo yake yote yakamwagika."
Hapa sasa kuna maneno matatu mazito sana ya Kigiriki:
πρηνὴς (prēnēs): Neno hili linamaanisha kuanguka mweleka kwa mbele (falling headlong / face down au kiswali wanasema kupomoka). Linaleta picha ya mtu anayeporomoka kwa kasi na uso au kifua kikitangulia chini, si kuanguka kwa miguu.,,,(maana tunategenea mtu anayejinyonga aanguke kwa miguu au sio)
ἐλάκησεν (elakēsen): Neno hili linatokana na
laskaō. Katika Kigiriki cha kale, lilitumika kuelezea kitu kinachopasuka
kwa kutoa sauti kubwa (kama vile mpira unaopasuka au mti unaovunjika kwa kishindo). Inaonyesha mwili wa Yuda ulipasuka kwa kishindo katikati (mesos).
σπλάγχνα (splanchna) Linamaanisha viungo vya ndani vya mwili, hasa matumbo.
sasa kwanini nimesema zinatofautiana?
Ukiisoma Biblia kwa Kigiriki chake cha asili, ukweli unakuwa huu:
haisemi popote kwamba "kamba ilikatika." Ikiwa Luka alitaka kusema kamba ilikatika, angetumia maneno ya Kigiriki kama
schoinion errhagē (kamba ilivunjika/ilikatika). Badala yake, Luka anatumia neno
prēnēs (kuanguka kwa mbele), ambalo linaweza kutokea kama mtu alijirusha au kuanguka kutoka juu, bila kuhusisha kamba kabisa