Kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji unachagua yapi?

IMG_7319.jpg
 
Nilibishana na rafiki yangu, yeye ameamua kujengea matofali ya kuchoma. Anasema ubora wa tofali la kuchoma liliokwa sawa sawa unazidi matofali ya saruji. Yeye pesa anayo ila ameamua kutumia matofali ya kuchoma katika ujenzi wake. Hivi ni kweli kuwa matofali ya kuchoma ni bora kuliko ya saruji?

Nilichomwambia ni kuwa, matofali ya kuchoma unauhakika ni udongo 100% kuliko upate ya saruji yawe 1/3 ni mchanga na 1/4 ni saruji. Lakini kuhusu uboara hui sina uhakika.
we we umejengea yap?
 
Kuna tofali zinatoka holili boda ni nzuri nadhani kwakuanzia katika msingi ni nzuri Sana manake zinamwagwa Kama mawe hazivunjiki zinachongwa ktka miamba
Nitazipata vipi, kama una contact ninaomba.
 
Ni kwasababu hatuna utaalamu mzuri wa kuoka matofali. Ulaya wanatumia matanuri ya gas na wanaoka kwa wingi kibiashara.

Kuna Mwarabu mmoja hapa kwetu ni mshika dini sana, yeye anafuata ratio ya 30:1 bag katika matofali ya saruji. Kwa kununua huyu anaaminika na matofali yake yananunuliwa sana.
Kabisa.Hatuna utaalamu, na hata wakiwepo, sisi si watu wa kufuata kanuni. Maana kuna wakati unanunua mwenyewe material, unafyatu mwenyewe lakini unazidisha idadi kuliko uwezo wa saruji. Tabia hii si lazima uwe huna hela hapa tz, wapo watu na uwezo kabisa lakini hufanya vitu chini ya kiwango. Ninadhani tumelelewa kuogopa vitu vya bei bilashaka, au hatuna uelewa na exposure. Mtu anajenga gesti, sink la kupigia mswaki la sh.8000/=. Baada ya mwaka , zile tundu za kupitisha maji zinalika kutu.
 
Nilibishana na rafiki yangu, yeye ameamua kujengea matofali ya kuchoma. Anasema ubora wa tofali la kuchoma liliokwa sawa sawa unazidi matofali ya saruji. Yeye pesa anayo ila ameamua kutumia matofali ya kuchoma katika ujenzi wake. Hivi ni kweli kuwa matofali ya kuchoma ni bora kuliko ya saruji?

Nilichomwambia ni kuwa, matofali ya kuchoma unauhakika ni udongo 100% kuliko upate ya saruji yawe 1/3 ni mchanga na 1/4 ni saruji. Lakini kuhusu uboara hui sina uhakika.

Tofali za saruji ni the best, kama tofali za kuchoma zingekuwa ni bora kuliko za saruji tungeona watu wakijengea kwa kutumia matofali ya kuchoma, na hata hivyo saruji nazo zina viwango vyake yaani kuna aina kadhaa za saruji kulingana na kazi fulani.
 
Ndugu, wewe unaongea ukifahamu ama basi tu mradi unafuata kile akili na nafsi yako inajisikia? Yani kutokuona watu wakitumia haya matofali ndiyo tayari unapigia mstari hayafai? duh! Umenishangaza kidogo. Fuatilia maoni kwenye uzi huu, utajifunza jambo.

note: Hili la uimara kati ya material hizi si suala la hisia, ni la kisayansi, ni fani hii ya watu kabisaa, UHANDISI.
 
Nakuambia hivi; hapa Bongo hakuna matofali ya kuchoma yanayoweza kuzidi matofali ya Saruji, labda matofali ya kuchoma kutoka nje ya Bongo, mfano sisi tulikuwa tunaagiza tractors kutoka Pakistani (Massey Ferguson), zilikuwa zikiletwa ndani ya kontena 40 feet, humo ndani ya kontena wapakistani walikuwa wanaweka vitofali vya kuchoma kama vigingi kuzuia hayo matreka yasiseleleke wakati wa usafirishaji, hayo matofali yalikuwa ni magumu ajabu kuliko matofali ya Saruji, kumbuka muulizaji alikuwa anataka kujua ubora kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji yanayopatika HAPA HAPA Bongo ambako huyo nduguye ndipo anapojenga.

Hapa Bongo historia inaonyesha kwamba watu wenye kipato kidogo ndio hujengea kwa matofali ya kuchoma isitoshe mimi mwenyewe nimewahi kushuhudia nyumba nyingi zikijengwa kwa matofali ya kuchoma na si mara moja nimewahi kujaribu ugumu wa hayo matofali ukilinganisha na matofali ya Saruji (1 bag for 25 bricks).
 
Ninadhani unasababisha ubishani usio na sababu. Mtoa post aliuliza kiujumla. Na baadhi ya wachangiaji tumemjibu kuwa kama mambo yatafanyika kikanuni, kwa tofali zote, kuchoma ni namba moja. Wewe post hii ndo umeonesha kuwa kumbe unakiri la kuchoma ni kiboko mradi tu viwango viwepo. Ile hoja yako ya mwanzo hadi nikakujibu vile ni kwa vile uliongea kiujumla tu. Yani kama unafundisha basi mwanafunzi anaelewa la kuchoma halifai, na sababu ni vile huoni watu wakijengea. Hii ni dhambi aisee!

Halafu bado hoja zako si madhubuti sana. Eti za kuchoma hutumiwa na masikini. Umeipata wapi hii? wabongo baadhi kwa kutojua ama sababu za kimazingira ndo huchagua saruji. Na wanatumia matofali ya kiwango cha chini mno. tofali unakuta 1:40. ndo majengo yaliyojaa miji yetu hasa Dar na maeneo jirani. Sababu kubwa kwa hapa kwetu watu kutumia ya kuchomwa ama saruji ni mazingira. Mpaka mkazi wa Dar pale magomeni apate tofali la kuchomwa litamfikia kwa kiasi gani? Hali hii ni tofauti ukiwa Iringa. Yale majumba ya wazee vibopa wa Kikinga kule Kihesa na Gangilonga yote ni tofali za kuchomwa. Kuna nyumba zimejengwa Dar mwaka jana, lakini haziingii kwa nyumba zile aisee zenye miongo kadhaa. Kakague chuo kama Mkwawa, sekondari kama Ifunda n.k. kisha njoo utuambie ule ni umasikini ama la.

Cha ajabu, ukizungumza kuhusu saruji, unataja standard hiyo ya 1:25, na hzi za kuchomwa pia zina viwango vyake, vikifikiwa ni bora zaid ya saruji. Na wangapi bongo wanajengea tofali za 1:25? Tumuogope Mungu aisee!
 
Hivi kwa mfano Dodoma utapsta wapi tofali za kuchoma!
 
Ni kwasababu hatuna utaalamu mzuri wa kuoka matofali. Ulaya wanatumia matanuri ya gas na wanaoka kwa wingi kibiashara.

Kuna Mwarabu mmoja hapa kwetu ni mshika dini sana, yeye anafuata ratio ya 30:1 bag katika matofali ya saruji. Kwa kununua huyu anaaminika na matofali yake yananunuliwa sana.
Sasa mbona ratio ni 1:23?
 
Ninadhani unasababisha ubishani usio na sababu. Mtoa post aliuliza kiujumla. Na baadhi ya wachangiaji tumemjibu kuwa kama mambo yatafanyika kikanuni, kwa tofali zote, kuchoma ni namba moja. Wewe post hii ndo umeonesha kuwa kumbe unakiri la kuchoma ni kiboko mradi tu viwango viwepo. Ile hoja yako ya mwanzo hadi nikakujibu vile ni kwa vile uliongea kiujumla tu. Yani kama unafundisha basi mwanafunzi anaelewa la kuchoma halifai, na sababu ni vile huoni watu wakijengea. Hii ni dhambi aisee!

Halafu bado hoja zako si madhubuti sana. Eti za kuchoma hutumiwa na masikini. Umeipata wapi hii? wabongo baadhi kwa kutojua ama sababu za kimazingira ndo huchagua saruji. Na wanatumia matofali ya kiwango cha chini mno. tofali unakuta 1:40. ndo majengo yaliyojaa miji yetu hasa Dar na maeneo jirani. Sababu kubwa kwa hapa kwetu watu kutumia ya kuchomwa ama saruji ni mazingira. Mpaka mkazi wa Dar pale magomeni apate tofali la kuchomwa litamfikia kwa kiasi gani? Hali hii ni tofauti ukiwa Iringa. Yale majumba ya wazee vibopa wa Kikinga kule Kihesa na Gangilonga yote ni tofali za kuchomwa. Kuna nyumba zimejengwa Dar mwaka jana, lakini haziingii kwa nyumba zile aisee zenye miongo kadhaa. Kakague chuo kama Mkwawa, sekondari kama Ifunda n.k. kisha njoo utuambie ule ni umasikini ama la.

Cha ajabu, ukizungumza kuhusu saruji, unataja standard hiyo ya 1:25, na hzi za kuchomwa pia zina viwango vyake, vikifikiwa ni bora zaid ya saruji. Na wangapi bongo wanajengea tofali za 1:25? Tumuogope Mungu aisee!

Wewe sasa sio mtafiti77 bali ni mtafiti 0.

Matofali ya kuchoma ya huku kwetu ni tofauti na yale ya ulaya na Asia kwani haya ya huku kwetu ni watu huchukua udongo "naturally" bila kuongeza chochote ndani yake na kuuponda, kuchanganya maji kupiga tofali, kukausha kisha kuchoma, kumbuka kwamba ubora wa tofali za kuchoma hutegemeana na natural constituents zilizomo ndani ya huo udongo na kamwe haiwezekani natural constituents za udongo wa Iringa, Kigoma, Morogoro nk, zikawa exactly sawa na hii inapelekea kuwa na utofauti kati ya tofali za kuchoma kati ya mkoa na mkoa au hata sehemu mbili tofauti za mkoa mmoja.

Wazungu au Waasia wao tofali zao za kuchoma hutengenezwa kwenye KIWANDA kutokana na UDONGO uliotengenezwa (udongo maalumu uliochanganywa na compound zinazosaidia tofali liwe na ugumu unaotakiwa wakati wa kuchoma) kifupi ni kwamba katika uchomaji kila kitu wao ni calculated ili kufikia ubora wa tofali tofauti na sisi huku, ndio maana nasema tofali zetu za kuchoma sio bora kuliko tofali za saruji zenye (1:25) mimi sisemi zile zilizochakachuliwa za 1:40 nk.--- pia kumbuka pia kuna aina karibu 4 za saruji zenye ubora tofauti.

Ninazungumzia ubora wa tofali za kuchoma za huku kwetu tofali zinazotengenezwa mitaani ambako TBS wanaogopa kufika, sizungumzii tofali zilizokaguliwa na kusimamiwa na wazungu wakati wanajenga hizo shule za kikoloni.
 
Hakuna unachoongeza hapa. Usemacho ndicho tusemacho wenzako. Swali halikuwa tofali la wapi bali tofali lipi kati ya la kuchomwa na la saruji. Nilikuepeleka Iringa baada ya kuona unaropoka tu ,eti, kisa huoni watu wakijengea basi ni ya masikini. Hii hoja ya kindezi sana ndugu yangu. Kha! Rejea post ndugu. Unachokifanya ni redundunt. Sisi tulishasema kuwa kama factors zote zikiwa constant, la kuchomwa ni bora zaidi. Hii hata Engineering inakiri. Hii ndo hoja hapa. Sasa unarudia kitu ambacho wenzako ndicho tunakisema.

Ukija hapa kwetu , bado huwezi kusema tu "through armchair thinking", eti tofali za saruji ni bora kuliko za kuchomwa. Kwa ujenzi wa kibongo chochote kinawezekana. Watu wengi tunajenga kwa materials yaliyo chini ya kiwango. Kwa hizi tofali itategemea tu ufyatuaji ulivyofanyika. Tupo maelfu ambao matofali yetu ni ya saruji lakini yanamomonyoka kama biskuti zile digestive kwa kutokufuata kanuni. Huyu akilinganishwa na aliyechoma tofali vema, tayari tutasema ya saruji si bora.Na kinyume chake ni hivyohivyo. Sasa hiki si kigezo cha kisayansi maana tunazungumzia matofali ambayo tayari kuna tatizo.

So, hoja ya msingi ni hiyo hapo juu, tukitumia standards , za kuchomwa ni madhubuti zaidi. Suala la uduni wa bidhaa kwa watanzania ni kesi nyingine.
 
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??
Umeongea kwa emotions na sio kwa facts ama rational mind mkuu.
Hebu Kama vipi tuingie maabara.
Inategemeana ni wapi.jamaa ameongelea nyumba na sio hizo structures zako.
Choma in terms of tension force iko poa zaidi ya sementi.
Ila la sementi liko poa in terms of compressive strength Ila sio tension.

Ila pia ghorofa ukiweka hata vioo ni sawa Ile ni weather protection.
Choma ghorofani yanakubali Mana kazi ya Wall katika ghorofa sio load bearing wall Bali ni weather protection.
Kumbuka ghorofa ni beam ,column,slabs , foundation na stairs ndo Zina kazi ya kulishikilia jengo Ila wall Haina kazi kiusalama.
 
Back
Top Bottom