Kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji unachagua yapi?

Kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji unachagua yapi?

Mimi nimewahi kupata tofali za kuchoma pcs kadhaa kutoka pakistan ni ngumu ile mbaya, huwezi kulinganisha na hizi zetu tunazochoma kienyeji, ukitaka kujaribu chukua tofali yetu moja, chukua hiyo ya kutoka pakistan na chukua kipande cha tofali ya Cement weka hivyo vipande vyote kwenye barabara ya lami na magari yavisage, tofali letu la kuchoma litasagika na kuwa unga completely na lile la cement litakuwa vipande vipande kama changarawe (partially ground) na hilo la Pakistan almost litabaki intact.

Conclusion yangu ni kwamba, matofali ya saruji ni bora kulinganisha na matofali yetu ya kuchoma ambayo hata yanaweza kushambuliwa na mchwa wajengao kirahisi.
Maelezo yako yanakosa sifa ya kuhitimisha namna unavyohitimisha. Kuhusu uimara, itategemea tu kila tofali mtengenezaji amejitahidi kufuata viwango kwa kiasi gani. Kuna ya kuchoma, udongo si wa mfinyanzi,ama hayakuchomeka vema, utajuta. Kuna ya saruji ratio ikawa magumashi, mfuko kwa tofali 40 au hayakushindiliwa vema pia utajuta. Na haya ndo yamejaa miji ya Pwani na Dar. Kwa namna hii huwez kusema ya saruji ni bora kuliko ya kuchoma. Si kweli.

Msisitizo
Tukiacha hayo matatizo ya kibongo (ya kutofuata viwango), kuchoma ndiyo tofali mujarab.
 
Umeongea kwa emotions na sio kwa facts ama rational mind mkuu.
Hebu Kama vipi tuingie maabara.
Inategemeana ni wapi.jamaa ameongelea nyumba na sio hizo structures zako.
Choma in terms of tension force iko poa zaidi ya sementi.
Ila la sementi liko poa in terms of compressive strength Ila sio tension.

Ila pia ghorofa ukiweka hata vioo ni sawa Ile ni weather protection.
Choma ghorofani yanakubali Mana kazi ya Wall katika ghorofa sio load bearing wall Bali ni weather protection.
Kumbuka ghorofa ni beam ,column,slabs , foundation na stairs ndo Zina kazi ya kulishikilia jengo Ila wall Haina kazi kiusalama.

Mkuu haya mambo usichanganye. Naona unaniambia hapa kinachoongelewa ni nyumba za kawaida na "sio structure zangu" lakini cha kushangaza na wewe badala ya kuongelea hizo nyumba ukarudi kwenye structure zangu!!

Kama uko kwenye sekta ya ujenzi utakubaliana na mimi kwamba hata nyumba huwezi kuta mtu anaye jiweza anajenga kwa tofali za kuchoma! Ukija kwenye majengo makubwa nako huwezi kuta tofali ya kuchoma.

Swali ni kwamba kama tofali za kuchoma ni imara na zinakubalika kuliko za kuchoma kwann nyumba nyingi zinajengwa kwa kutumia matofali ya cement? Je hawa watu hawapendi uimara wa tofali za kuchoma mpaka watumie za cement??

Turudi kwenye hii statement yako..

===

Choma in terms of tension force iko poa zaidi ya sementi.
Ila la sementi liko poa in terms of compressive strength Ila sio tension.

=====

Mkuu uko serious kweli??
 
Ndugu, wewe unaongea ukifahamu ama basi tu mradi unafuata kile akili na nafsi yako inajisikia? Yani kutokuona watu wakitumia haya matofali ndiyo tayari unapigia mstari hayafai? duh! Umenishangaza kidogo. Fuatilia maoni kwenye uzi huu, utajifunza jambo.

note: Hili la uimara kati ya material hizi si suala la hisia, ni la kisayansi, ni fani hii ya watu kabisaa, UHANDISI.

Mkuu naomba nikuulize swali rahisi...

Umesema ni swala la kisayansi..

Sasa je umeona wapi jengo la serikali linajengwa kwa tofali za kuchoma??

Au mainjinia wa serikali hawajui hiyo sayansi yako?
 
Tofali za kuchoma zinaleta joto kali kwenye nyumba. Zinafaa mikoa yenye ubafidi. Kwa uimara za kuchoma ni imara zaidi sema zinakula cement nyingi wakati wa kuzijenga!
Kama ni imara zaidi ya tofali za cement kwann hata huko kwenye maeneo ya baridi huwezi kuta serikali inatumia tofali za kuchoma? Au serikali haitaki huo uimara unao usemea wewe?
 
Mkuu naomba nikuulize swali rahisi...

Umesema ni swala la kisayansi..

Sasa je umeona wapi jengo la serikali linajengwa kwa tofali za kuchoma??

Au mainjinia wa serikali hawajui hiyo sayansi yako?
Kuwa muelewa. Swali lako linaaishiria hujui. Kwa kesi yetu hapa, huwezi kuthibitisha kwa kutoona. Kutoona kunaweza kuwa ni udhaifu wako kutojua dunia, au udhaifu wa wako au jamii yenu kutomudu matofali husika. Hoja ya msingi ni je, tofali lipi ni imara kuliko lingine? Hapa jibu ni la kuchoma. Hii ni hoja ya kisayansi na majibu yanaweza kuwekwa hapa kutoka kwa watafiti. Tumeshafanya hivyo, soma uzi wote utapata.

Tunachosema ni kwamba kutokana na tabia zetu(kutojali na kupenda mseleleko) au uwezo wetu kuwa duni, wengi hatuna uwezo wa kuwa na matofali bora iwe ya kuchoma ama saruji (tunaongea kiujumla). Serikali ,kwa dhati yake, inapaswa kujenga kwa kiwango stahiki, sasa kuna kiwanda cha matofali ya kuchoma hapa nchini? Hebu nitajie kiwanda kinachotoa matofali ya kuchoma yale yenye ubora wa kimataifa, unakijua? Tofali ambazo walau unaweza kudhibiti (na bado wanapigwa sana) ni za saruji, za kuchoma unazitoa wapi? Hizi za kienyeji nipasua kichwa, hazinyooki, hazina vipimo linganifu, na pengine hazikuchomwa vema. Miaka ya nyuma ndo kulikuwa na uzalishaji wa tofali za kuchoma na ulikuwa mdogo sana. Kuna mchangiaji ametoa mfano huko misheni Peramiho walifanya kazi hii.

Kama unataka mfano wa tofali za kuchoma, nenda ama waulize waliosoma Mkwawa , utazikuta. Acha hizi bora niishi tunazojengea akina sisi.

Kwahiyo, serikali kutojengea tofali za kuchoma au kutoona tofali hizi zikijenga maghorofa hapa bongo kunasababishwa na sababu za kimazingira na siyo kwamba hazifai. Tofali za saruji zinatawala si kwa sababu ya uimara, bali zenyewe zinapatikana kirahisi na bilashaka hata shape ina afadhali kuliko ya kuchomwa. Kuhusu uimara wa hizo za saruji, hii bado ni mjadala. Bado serikali na wadau wote wanapigwa tu. Na pakifanyika utafiti wa ubora wa majengo kipengele cha matofali , mtafiti akafanya kazi yake kwa kumuogopa Mungu, wallahi matokeo yake utakimbia hapa.

Matofali ya kuchoma yanajenga maghorofa mkuu. Baadhi ya nchi ndo matofali yao. Wewe kutoona ni shida yako na jamii yako.
 
Kama ni imara zaidi ya tofali za cement kwann hata huko kwenye maeneo ya baridi huwezi kuta serikali inatumia tofali za kuchoma? Au serikali haitaki huo uimara unao usemea wewe?
Unakomaa na serikali hivi. kwani, hata hayo ya saruji wanayojengea ni bora sasa? Majengo ya serikali ilikuwa zamani, miaka ya 90 kurudi nyuma huko. Siku hizi ni balaa tupu. Ushaona jengo mwaka juzi waziri sijui mkuu wa mkoa akilikataa? Alikuwa anapigapiga ukuta unamomonyoka kama biskuti zile digestive.

Sasa, sababu hii ya ujenzi duni haiwezi tumika kufananisha matofali haya mawili. Maana huyu ataesema nimeona ya kuchoma yapo hivi, na yule ameona ya saruji yapo vile. Tukiondoa factors zetu hizi za ndani, tujifanye tupo kimataifa, tofali la kuchomwa ndiyo mujarab
 
P
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??
Kama ulishaenda New York, London, Berlin, hamburger German, masachussate, Boston, ghorofa nyingi za zamani walitumia tofari choma, ghorofa mpaka 50 kwenda juu. Sasa hivi wanatumia material tofauti chuma na bao au hard Wood kupunguza uzito ghorofa inaenda mpaka 200 .
 
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??

Screenshot_20210803-135545.png


Screenshot_20210803-135459.png


Screenshot_20210803-135258.png
 
Hii nyuzi inagusa pahala ninapojihusisha napo,
Tofali za kuchoma ni bora kuliko za saruji pasi na shaka, ila huo ubora sasa unatokana na "factors " ambazo huko juu awali kuna baadhi ya wadau wameziainisha kwa uwazi kabisa. Sisi watanzania ( hata na baadhi ya wenzetu hapa africa) tumeaaminishwa katika kutumia saruji kwenye ujenzi ili kujitanabaisha kuwa tuna maendeleo sababu tumeaminishwa ujenzi wa kutumia udongo ni wa mtu baki asiye na elimu asiye na maendeleo kwa wakati mwingine mtu masikini asiye na uwezo, kumbe udongo huo huo ( readily and locally available in abundancy) ukichakatwa kwa njia sahihi ukabumbwa kwa ustadi (moulded) ,ukachomwa kwa joto sahihi utapata tofali zuri lenye durability na strength maradufu ya tofali ya saruji ambayo ina expiration date.
 
IMG_1247.JPG
mfano hizi zina clay content 44% , udongo ulichakatwa ukaingizwa kwenye machine zikakandamizwa kwa kiwango cha 9 MPa ( wataalam walivyotuelezea), then hapo zikapangwa tayari kwa uchomaji.
 
Ni kwasababu hatuna utaalamu mzuri wa kuoka matofali. Ulaya wanatumia matanuri ya gas na wanaoka kwa wingi kibiashara.

Kuna Mwarabu mmoja hapa kwetu ni mshika dini sana, yeye anafuata ratio ya 30:1 bag katika matofali ya saruji. Kwa kununua huyu anaaminika na matofali yake yananunuliwa sana.
Yuko wapi huyu mwarabu?
 
Mkuu naomba nikuulize swali rahisi...

Umesema ni swala la kisayansi..

Sasa je umeona wapi jengo la serikali linajengwa kwa tofali za kuchoma??

Au mainjinia wa serikali hawajui hiyo sayansi yako?

Screenshot_20210807-175629.png


Screenshot_20210807-175712.png


Screenshot_20210807-175559.png


Screenshot_20210807-175532.png
 
Back
Top Bottom