Kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji unachagua yapi?

in Mara ya kwanza naona watu wanalinganisha choma na saruji. Tofali la kuchoma lina heshima yake. Sema tuu basi waswahili tumekuwa experts wa slope na magumashi. Lakini tofali lililochomwa kitalaam halina mpinzani.
 
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??
Ndio tena yako mengi tuu
 
Sasa kwanini magorofa na matenki ya maji wanatumia tofali za cement? Au hao wajenzi wa magorofa na matenki hawataki uimara?
Shida ni kasumba na pia haya ya saruji uandaaji wake hadi yapelekwe maabara kuyapima strength ni WA haraka kuliko tofari za kuchoma zenyewe zina process ndefu kuanzia uchaguaji wa udongo hadi kuichoma.

Sasa huwezi kutumia hizi za kubumba unless ujiridhishe na size,uimara na strength yake maana hizo ni Kazi za serikali mkuu.
 
Na wewe una shida zako binafsi pia,kwa taarifa yako wenye pesa wanaagiza tofari choma maalumu kutoka maeneo zinakopatikana za uhakika wanajengea nyumba kali Sana 👇👇

 
Mmesahau matofali mabichi yanayotumika uku Mbeya nayo ni standard sana🤓🤓🤓
Inategemeana na udongo,kuna udongo mwingine ukichoma unahatibu ubora,huo wa Mbeya unafaa kujengea wenyewe ila Ili yawe imara zaidi inafaa yaongezewe saruji kiasi afu fyatua kausha utaona mziki wake.
 
Nadhani anaejiweza atajengea tofari choma zile za viwango sio blocks wa choma kawaida.

Mimi niwe na pesa zangu naachaje kujenga kwa tofari kama hizi hapa chini?👇👇





 
Hahahah eti standard za kuni
 
  1. matofali ya blocks yana high compressive strength than choma, sababu strength ya bloko iko prpotion to cotent ya cement where by sand,water quality ni costant sasa kadri uongezapo cement kwenye mchanga na maji strengh inaongezekaa toafuti na choma, ukiongeza poda ya vumbi kwenye paste ya tofali unaongeza plascity index ya paste then unapunguza bearing capacity ya tofali.
  2. kama hakuna magunzo ya zege kwenye structure, bloko ndo nzuri
  3. water raiser ndio hata government wanatumia bloko lakini ratio ni kali kidogo 1:3 hadi 1:4(hapo mfuko mmoja utapata tofali 9 au 10 za nch 6)
 
mimi nyumba yangu sipendi kutumia tofali za choma au blocks napenda sana mahekalu kama ya mjerumani napenda nyumba iwe kama chuma
  1. hatua ya msingi , napenda raft foundation haijalishi eneo likoje, option ya pili napenda nichimbe msingi kwenda chini 70cm -100cm , upana 60cm, then nacast chini ya msingi kwanza blinding concrete grade 15, 6cm thickness baada ya hapo najenga ukuta wa msingi kwa kutumia matofali ya zege(1:2.5:5 mix hapa unapata strength ya 17.5MPA Ambayo ni class 15 kali kidogo) hadi usawa wa juu ya ardhi, then ukuta unaenda 1M high above original ground level ili nipate ngazi 5 za veranda hata mvua ikinyesha nakuwa niko juu then naweka moramu ndani ya msingi,then mawe na fill pores za mawe kwa sand baada ya hapo nanyunyuzia dawa ya kuua wadudu altmeticn baadae naweka DPM (damp proof membrane) hilo ni kapeti laini baadae nasuka nondo y12 kuzunguka misingi mama(bearing) au yote kama na fund baadae nafunga box namwaga zege la jamvi ratio ileile 1:2:4.5 hadi hapo nakuwa na msingi imala
  2. hatua ya boma, najenga kwa tofali za zege inch 6 hadi juu ,lenta natumia zege la ratio 1:1.75:3.5 ambayo ni class 20 itakayokupa 22.5MPA Stength
  3. naezeka na araf steel truss pamoja na branderring, kwenye bati natumia roman tiles gauge 28, bodi gypsum kwa ajili ya dari
  4. skimming natumia wall putty
  5. rangi natumia weather na silk paint
  6. milango natumia mbao za mninga na vitasa natumia 3 levers au vile vya kisasa vya pasword
  7. sakafu, napenda 3d expoxy.
  8. madirisha upv slinding windows
nazani nyumba imeisha
 
Natamani unielewesha zaidi, natamani sana nyumba ya tofali za kichina, Uganda wanjengea tofali za kuchoma na ni nzuri mno,
 

Mzee 1M kwa 5steps za ngazi!? Hiyo riser na tread zitakuwa na sizes gani?
 
Tofali za kuchoma zinaleta joto kali kwenye nyumba. Zinafaa mikoa yenye ubaridi. Kwa uimara za kuchoma ni imara zaidi sema zinakula cement nyingi wakati wa kuzijenga!
Naomba kuuliza mkuu, unavyosema zinakula cement nyingi unamaanisha nini maana hata za cement pia si zinakengwa kwa kutumia cement, naomba unieleweshe napenda sana nyumba za ma tofali ya kichina hua zina vitia, na inawezekana kupiga plasta na rangi au lazima matofali yaonekane tu
 
Hapa ndipo umuhimu wa shule huonekana. Bravo kiongozi.
 
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??
kwenye ujenzi wa maghorofa huwa hayakai matofali pekee, ila matofali hayo ya saruji, uwaga yanasapotiwa na nguzo za zege na nondo. Structurs za matenk zipo nyingi sana, ukienda kaliua-tabora, ile tank kubwa pale n tofali choma, ikapigwa plasta vzr, na ukienda kilumbi-sikonge, katika kitongoji cha mtendeni ipo stand ya tank, la tofali za choma.
 
Huyo jamaa hajatembea tu na hajui vingi kuhusu ujenzi, yaani yeye anaamini kusimama kwa ghorofa eti ni uimara wa tofali tu

Mwambie aende pale Mwanza "kwa Kishimba" akaone ghorofa lililojengwa kwa tofali za kuchoma.
 
Huwezi kua serious.
 
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??
Zipo ghorofa nyingi tu zimejengwa kwa tofali za kuchoma, nyingi haswaa
Konachofanya huko ulipo usione tofali za kuchoma zikijengwa ghorofa ni sababu ya ugumu wa upatikanaji wake, Ila ungekua unaishi sehemu kama sumbawanga basi usingeandika hiki umeandika

Tofali ya kuchoma ni bora kuliko ya cement. Hapa Kama una ufahamu mkubwa wa mambo ya construction au ww Ni civil eng, basi tunaweza weka mjadala
 
Huyo jamaa hajatembea tu na hajui vingi kuhusu ujenzi, yaani yeye anaamini kusimama kwa ghorofa eti ni uimara wa tofali.

Mwambie aende pale Mwanza "kwa Kishimba" akaone ghorofa lililojengwa kwa tofali za kuchoma.
Hapo yupo sahihi, kusimama kwa ghorofa ni uimara wa tofali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…