Kati ya Mbunge (MP) na Mkuu wa wilaya (DC) yupi ana mamlaka zaidi?

Kati ya Mbunge (MP) na Mkuu wa wilaya (DC) yupi ana mamlaka zaidi?

Ila mkuu mbona mbunge analipwa zaidi kuzidi DC? imekaaje hii?
Kichwa cha habari yako, umetaka kujua nani mwenye mamlaka, ukumbuke, siyo anaelipwa vizuri.
Mbunge yeye yuko jikoni, lazima wajipendee.
 
Kichwa cha habari, umetaka kujua nani mwenye mamlaka, ukumbuke, siyo anaelipwa vizuri.
Mbunge yeye yuko jikoni, lazima wajipendee.
Ni kweli, ila mkuu wa wilaya ni mwakilishi wa rais wilayani, ni kama rais wa wilaya, nilitegemea yeye ndio alipwe vizuri kwa mamlaka yake.

Nasema hivi kwasababu, juzi Mhe. Lissu alisema hakuna uwiano wa malipo kwa viongozi na ukubwa wa idadi ya watu wanaowawakilisha.
 
Jiulize swali Moja tuu,kwenye wilaya Kuna majimbo mangapi amabyo yanawabunge,na Kuna wakuu wa wilaya wangapi kwenye wilaya then utapata jibu
 
Ni kweli, ila mkuu wa wilaya ni mwakilishi wa rais wilayani, ni kama rais wa wilaya, nilitegemea yeye ndio alipwe vizuri kwa mamlaka yake.

Nasema hivi kwasababu, juzi Mhe. Lissu alisema hakuna uwiano wa malipo kwa viongozi na ukubwa wa idadi ya watu wanaowawakilisha.
Hapo sijamwelewa anachomaanisha, kuwa mbunge maslahi yake ni madogo au la.
Sema hawa wakubwa wawaangalie na watumishi wa nyanja nyingine wasipiganie tu maeneo ambayo wao wanaweza kukaa.

Mbunge anakamata mshahara milion 10, kwa mwezi, na mafungu kibao, na muda mwingi hana kazi lazima kama ilivyo kwa mwalimu na askari, wanaopata mshahara 600,000 mwenye mshahara mkubwa 3,000,000.
Alafu kiongozi bado anaumizwa na maslahi ya viongozi.
 
Kila mtu ana mamlaka yake.Mbunge hayuko katika mfumo wa DC wala DC hayuko katika Mfumo wa Bunge.Kwenye Ngazi ya Wilaya Mbunge ni Diwani tu ila DC haingii kwenye vikao vya madiwani.Kule anakluwepo Mkurugnezi mtendaji wa Halmashauri.

So kimamlaka hakuna anayewajibika kwa Mwenzake.Mbunge hawajibiki kwa Mtu yeyote yule nje ya Bunge ispokuwa wapiga Kura ila ndani ya Bunge anayawajibika kwa Spika to certain extent na Ndani ya vikao vya halmashauri kwa Mwenyekiti wa halmashauri au kwa Meya kwa kiwango Fulani.

So inshort Mbunge ni Mamlaka inayojitegemea ambayo inawajibu wa kuisimamia serikali katika Ngazi mbalimbali,
Umefafanua vyema.
 
Sasa mbona tunaona RCs na DCs wanaondoka huko na kugombea Ubunge?

Basi kuna kitu hakiko sawa. Lol
 
Kwema wakuu

Kama title inavyosomeka ningependa kujuzwa, kati ya Mbunge na Mkuu wa wilaya yupi ana mamlaka zaidi ya kiutawala/kiuongozi?

Naelewa mbunge yupo kwenye mhimili wa bunge(legislature) na mkuu wa wilaya yupo kwenye mhimili wa serikali kuu(executive), ila yupi kati yao ana nguvu ya kimamlaka/kiuongozi kuzidi mwingine?
Changia kwa hoja
Karibu
Kwenye hii serikali ya machawa kila kiongozi anayo mamlaka ya kiuongozi
 
Me bado najifunza, hivi kwani mbunge anaishi ndani ya wilaya iliyo bebwa na mkuu wa wila/mkoa au mkuu wa mbunge?
 
DC ana mamlaka zaidi, ana power na machinery za kuwajibisha. Mbunge hana sauti zaidi ya connection za kumtumia DC na DED
 
Me bado najifunza, hivi kwani mbunge anaishi ndani ya wilaya iliyo bebwa na mkuu wa wila/mkoa au mkuu wa mbunge?
Navyojua Mkuu wa wilaya anasimamia wilaya ambayo ndani yake inaweza kuwa na jimbo moja au zaidi, mbunge yeye anahusika na jimbo moja tu.
 
DC ana mamlaka zaidi, ana power na machinery za kuwajibisha. Mbunge hana sauti zaidi ya connection za kumtumia DC na DED
anhaa sawa, tunaweza kusema DC ana power ya kiutendaji na kutekeleza sheria wakati MP ana power ya kiushawishi na kutunga sheria
 
MaDC wengi wanautamani na kuhamia uMP sababu ya ulaji
 
Kwema wakuu

Kama title inavyosomeka ningependa kujuzwa, kati ya Mbunge na Mkuu wa wilaya yupi ana mamlaka zaidi ya kiutawala/kiuongozi?

Naelewa mbunge yupo kwenye mhimili wa bunge(legislature) na mkuu wa wilaya yupo kwenye mhimili wa serikali kuu(executive), ila yupi kati yao ana nguvu ya kimamlaka/kiuongozi kuzidi mwingine?
Changia kwa hoja
Karibu
Anayepigiwa saluti na Askari ndio mwenye mamlaka
 
Back
Top Bottom