Kati ya Mbunge (MP) na Mkuu wa wilaya (DC) yupi ana mamlaka zaidi?

Ila mkuu mbona mbunge analipwa zaidi kuzidi DC? imekaaje hii?
Kichwa cha habari yako, umetaka kujua nani mwenye mamlaka, ukumbuke, siyo anaelipwa vizuri.
Mbunge yeye yuko jikoni, lazima wajipendee.
 
Kichwa cha habari, umetaka kujua nani mwenye mamlaka, ukumbuke, siyo anaelipwa vizuri.
Mbunge yeye yuko jikoni, lazima wajipendee.
Ni kweli, ila mkuu wa wilaya ni mwakilishi wa rais wilayani, ni kama rais wa wilaya, nilitegemea yeye ndio alipwe vizuri kwa mamlaka yake.

Nasema hivi kwasababu, juzi Mhe. Lissu alisema hakuna uwiano wa malipo kwa viongozi na ukubwa wa idadi ya watu wanaowawakilisha.
 
Jiulize swali Moja tuu,kwenye wilaya Kuna majimbo mangapi amabyo yanawabunge,na Kuna wakuu wa wilaya wangapi kwenye wilaya then utapata jibu
 
Hapo sijamwelewa anachomaanisha, kuwa mbunge maslahi yake ni madogo au la.
Sema hawa wakubwa wawaangalie na watumishi wa nyanja nyingine wasipiganie tu maeneo ambayo wao wanaweza kukaa.

Mbunge anakamata mshahara milion 10, kwa mwezi, na mafungu kibao, na muda mwingi hana kazi lazima kama ilivyo kwa mwalimu na askari, wanaopata mshahara 600,000 mwenye mshahara mkubwa 3,000,000.
Alafu kiongozi bado anaumizwa na maslahi ya viongozi.
 
Umefafanua vyema.
 
Sasa mbona tunaona RCs na DCs wanaondoka huko na kugombea Ubunge?

Basi kuna kitu hakiko sawa. Lol
 
Kwenye hii serikali ya machawa kila kiongozi anayo mamlaka ya kiuongozi
 
Me bado najifunza, hivi kwani mbunge anaishi ndani ya wilaya iliyo bebwa na mkuu wa wila/mkoa au mkuu wa mbunge?
 
DC ana mamlaka zaidi, ana power na machinery za kuwajibisha. Mbunge hana sauti zaidi ya connection za kumtumia DC na DED
 
Me bado najifunza, hivi kwani mbunge anaishi ndani ya wilaya iliyo bebwa na mkuu wa wila/mkoa au mkuu wa mbunge?
Navyojua Mkuu wa wilaya anasimamia wilaya ambayo ndani yake inaweza kuwa na jimbo moja au zaidi, mbunge yeye anahusika na jimbo moja tu.
 
DC ana mamlaka zaidi, ana power na machinery za kuwajibisha. Mbunge hana sauti zaidi ya connection za kumtumia DC na DED
anhaa sawa, tunaweza kusema DC ana power ya kiutendaji na kutekeleza sheria wakati MP ana power ya kiushawishi na kutunga sheria
 
MaDC wengi wanautamani na kuhamia uMP sababu ya ulaji
 
Anayepigiwa saluti na Askari ndio mwenye mamlaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…