Kati ya Mfaransa na Mreno nani alifanikiwa kwenye assimilation policy Africa?

Kati ya Mfaransa na Mreno nani alifanikiwa kwenye assimilation policy Africa?

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
8,082
Reaction score
17,838
Assimilation sijui neno lake kwa kiswahili.

Niiweke hivi asimileshen ni idea flani hivi watu wanalazimishwa kwa hiari kufuata na kuridhia tamaduni za wengine nakuacha tamatuni zao.

Mfaransa na Mreno waliweza kufanikisha hili kwenye makoloni zao walizotawala Africa kwa mafanikio makubwa sana.

Lakini kwa upande wangu mimi naona Wareno walifanikisha zaidi.

Kwasababu mataifa wareno waliyoyatawala Africa Cape Verde, Guinea Bissau, Angola na Msumbiji yani wameiga kila kitu kutoka Ureno hadi majina yao ya ukoo ni ya kireno ukiachilia mbali na lugha.

Tofauti na nchi zilizotawaliwa na Ufaransa. Ambapo nyingi tu unakuta bado lugha zao za asili wanaongea sana mfano Senegal Wolof na majina yao ya ukoo bado wanatumia ya ukoo.

Mental slavery is real.
 
Muhispania Naye kapandikiza mbegu yake ya asimileshen kwenye koloni moja la kipekee alilotawala Africa Equatorial Guinea. Wananchi wa hili taifa wengi nao wanajionaga wahispania ila wamejitaidi sana kuhifadhi majina yao asili tofauti na waliotawaliwa na wareno.
 
Mreno alifanikiwa sana katika assimilation.

Vilevile alijisahau kwa kujua kwamba makoloni yake ni majimbo ya Ureno, hivyo aliwekeza sana katika sekta mbalimbali, ikiwemo miundo mbinu akitegemea kuwa hataondoka kamwe! Mpaka Leo amebaki maskini sana, miongoni mwa nchi zilizokuwa na makoloni, kutokana na suala hili.
 
Back
Top Bottom