Hivi ni kipi kilichosababisha wamarekani weusi wakawa na matamshi tofauti na wamarekani wa kizungu?
Hilo ni kweli, lakini si ukweli wote.
Hata weusi kwa weusi [Foundational Black Americans] wana lafudhi tofauti tofauti kulingana na eneo watokalo.
Kwa mfano, weusi [Foundational Black Americans] wa Texas wana lafudhi tofauti kabisa na weusi wa Georgia.
Weusi wa Maryland wana lafudhi tofauti kabisa na weusi wa Mississippi.
Weusi wa Virginia wana lafudhi tofauti kabisa na weusi wa Alabama.
Malcolm X na Martin Luther King walikuwa na lafudhi tofauti.
Malcom X alizaliwa Omaha, Nebraska na akakulia Milwaukee, Wisconsin, Lansing, Michigan, na Boston, Massachusetts.
Martin Luther King Jr., alizaliwa na kukulia Atlanta, Georgia.
Hawa wawili ukizisikiliza hotuba zao utagundua walikuwa na lafudhi tofauti.
Pia, hata wazungu kwa wazungu nao wana lafudhi tofauti.
Wazungu wa Arkansas na Kentucky wana lafudhi tofauti na wazungu wa South na North Dakota.
Wazungu wa Kansas wana lafudhi tofauti na wazungu wa Alaska.
Sababu hasa ya tofauti hizo siijui au sizijui. Ila ninachojua elimu nayo huwa na mchango mkubwa sana.
Mambo mengine ambayo huchangia utofauti huo ni maeneo ya kijiografia na labda exposure na contact na watu wa sehemu zingine.
Kwa mtu ambaye hujaishi na Wamarekani kwa muda mrefu, baadhi ya tofauti hizo za kilafudhi ni ngumu kuzibaini.
Ni kama vile ambavyo wao wakija huku kwetu, itawawia vigumu kuzibaini lafudhi za wazungumzaji wa Kiswahili ambao ni Wasukuma, Wachaga, au Wahehe.
Ila mimi na wewe haitotuwia vigumu kumbaini Ngosha ni yupi na Mangi ni yupi.
Na hata kwa Wasukuma, sisi kwa sisi kupitia lafudhi huwa tunagunduana kirahisi yupi ni Mnyantuzu, yupi ni wa Shinyanga, na yupi ni wa Mwanza.
Ila Mnyakyusa ambaye hajaishi na Wasukuma, kwake atasikia lafudhi tu ya Kisukuma.