Kati ya Mwingereza na Mmarekani Ni yupi huwa unamuelewa kwa urahisi akiwa anaongea kingereza?.

Kati ya Mwingereza na Mmarekani Ni yupi huwa unamuelewa kwa urahisi akiwa anaongea kingereza?.

We mtoa mada hujui ngeli ya mwingereza akiongea huwezi sikia neno hata moja British accent sio mchezo kiujumla American English ni maarufu na imesambaa sana kupitia miziki films zote hizo ni American English
Hakuna British accent moja.

Hakuna American accent moja!

Watu wa Boston wanasikika tofauti kabisa na watu wa Louisiana!

Wa Minnesota wanasikika tofauti kabisa na watu wa New Jersey.

Baltimore na Philadelphia hawafanani kivile.
 
Sikiliza interview za sky sport za wachezaji wa kiingereza wa EPL ndio utajua haujui.

Halafu msikilize Mzee Biden pamoja na Trump tower utapata jibu kama kiingereza cha wasomi wa Tz ni rahisi kukielewa sababu wasomi wanazungumza kwa kutumia kigugumizi ili wasidhalilike.
 
Kwa hapa Afrika napenda mno kiingereza cha waganda na wazambia.
 
We mtoa mada hujui ngeli ya mwingereza akiongea huwezi sikia neno hata moja British accent sio mchezo kiujumla American English ni maarufu na imesambaa sana kupitia miziki films zote hizo ni American English
ngeli ya mwingereza haijawahi kunipa tabu kuielewa
nilifanya field na waingereza tukawa tunaelewana bila shida yoyote
ila shida hua inakuja nikiwa nawasikiliza wamarekani
Huwa inachukua muda kidogo kuelewa walichokiongea haijalishi ni face 2 face conversion au kinyume
 
Mmarekani aliharibu kingereza. Back in the days wamarekani ni waingereza waliokuwa wanafinyiliwa wakasema wameenda kutafuta green pastures na they swore to come back na ku colonise wenzao. Sasa kila kitu juu ya chuki walikiweka opposite na wenzao. Kwa mfano keep right in England is keep left in america. Fly over in England ni overpass in America. Degree centigrade ni Degree Fahrenheit, kilometres ni miles ,feet ni yard ,litres ni gallons. Kwa kifupi kwa lugha America hufupisha maneno. Example it doesn't in British ni it daet in American it is in British is ain't in American, colour ni color . simply America loves short cuts in everything. Waingereza na wamarekani ni cousins
 
Hakuna British accent moja.

Hakuna American accent moja!

Watu wa Boston wanasikika tofauti kabisa na watu wa Louisiana!

Wa Minnesota wanasikika tofauti kabisa na watu wa New Jersey.

Baltimore na Philadelphia hawafanani kivile.
Hivi ni kipi kilichosababisha wamarekani weusi wakawa na matamshi tofauti na wamarekani wa kizungu?
 
Hivi ni kipi kilichosababisha wamarekani weusi wakawa na matamshi tofauti na wamarekani wa kizungu?
Hilo ni kweli, lakini si ukweli wote.

Hata weusi kwa weusi [Foundational Black Americans] wana lafudhi tofauti tofauti kulingana na eneo watokalo.

Kwa mfano, weusi [Foundational Black Americans] wa Texas wana lafudhi tofauti kabisa na weusi wa Georgia.

Weusi wa Maryland wana lafudhi tofauti kabisa na weusi wa Mississippi.

Weusi wa Virginia wana lafudhi tofauti kabisa na weusi wa Alabama.

Malcolm X na Martin Luther King walikuwa na lafudhi tofauti.

Malcom X alizaliwa Omaha, Nebraska na akakulia Milwaukee, Wisconsin, Lansing, Michigan, na Boston, Massachusetts.

Martin Luther King Jr., alizaliwa na kukulia Atlanta, Georgia.

Hawa wawili ukizisikiliza hotuba zao utagundua walikuwa na lafudhi tofauti.

Pia, hata wazungu kwa wazungu nao wana lafudhi tofauti.

Wazungu wa Arkansas na Kentucky wana lafudhi tofauti na wazungu wa South na North Dakota.

Wazungu wa Kansas wana lafudhi tofauti na wazungu wa Alaska.

Sababu hasa ya tofauti hizo siijui au sizijui. Ila ninachojua elimu nayo huwa na mchango mkubwa sana.

Mambo mengine ambayo huchangia utofauti huo ni maeneo ya kijiografia na labda exposure na contact na watu wa sehemu zingine.

Kwa mtu ambaye hujaishi na Wamarekani kwa muda mrefu, baadhi ya tofauti hizo za kilafudhi ni ngumu kuzibaini.

Ni kama vile ambavyo wao wakija huku kwetu, itawawia vigumu kuzibaini lafudhi za wazungumzaji wa Kiswahili ambao ni Wasukuma, Wachaga, au Wahehe.

Ila mimi na wewe haitotuwia vigumu kumbaini Ngosha ni yupi na Mangi ni yupi.

Na hata kwa Wasukuma, sisi kwa sisi kupitia lafudhi huwa tunagunduana kirahisi yupi ni Mnyantuzu, yupi ni wa Shinyanga, na yupi ni wa Mwanza.

Ila Mnyakyusa ambaye hajaishi na Wasukuma, kwake atasikia lafudhi tu ya Kisukuma.
 
Kwanini msijiulize, Zanzibar wanaongea Kiswahili lakini lafudhi na lahaja ni tofauti? Ukizingatia ni sehemu ndogo.
Wakojani
Wanungwi
Watumbatu
Wamakunduchi
Wapemba
Waunguja n.k
Hayo ni maeneo na sio Kabila,lakini wanatofautiana matamshi na lafudhi. Sembuse America ambayo jimbo moja ni kubwa zaidi ya nchi yetu,washindweje kutofautiana?
 
Back
Top Bottom