Kati ya Mwingereza na Mmarekani Ni yupi huwa unamuelewa kwa urahisi akiwa anaongea kingereza?.

Huwa napata ugumu kidogo nikiwa namsikiliza Mmarekani ila namuelewa kwa urahisi zaidi mwingereza.

Wataalam wa kingereza karibuni.
Uingereza kuelewa changamoto wanaongea kile cha ndani kabisa ni kama ukutane na Kiswahili cha Bwana JORAM
 
Huwa napata ugumu kidogo nikiwa namsikiliza Mmarekani ila namuelewa kwa urahisi zaidi mwingereza.

Wataalam wa kingereza karibuni.
Naelewa wote ila kuna baadhi ya British accents/dialects huwa zinanipa tabu muda mwengine kuelewa mfano cockney huwa wana silent "T" sasa jua kwamba maneno yoote yenye "T " wao wanameza mfano Maji kwa kiingereza "Water" inatamkwa "Wota" wao wanatamka "wo a" hapo bado zile intonations kuna pia scottish accent .

Kwa marekani english yao ni very simple ila kuna "Black american venacular " au "ebonics " na hii inategemeana na maeneo sasa ukute yule aliyekulia kwenye ghetto's hizi kumuelewa ni ngumu maana wana misamiati yao ambayo kwenye standard american english haipo .

Kingine ukiacha ya kuwa american english ni rhotic language ( yaani wanaweka emphasis kwenye mid na Last "R" ) hakipo tofauti saaana na british english labda kwenye matamshi na kuna vitu vina majina tofauti.

Kwa mimi nadhani ni ishu ya accent & dialect sana sana ila viingereza vyoote vinaeleweka haijalishi maeneo.
 
Umeshakutana na wale wa kutoka Scotland au Ireland? Nilikutana na mmoja nilichoka. Neno moja lenye herufi 4 au zaidi herufi unaweza kuzisikia zikitamkwa zinaweza kuwa 2 tu
 
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂

Nimecheka sana
 
Asante kwa elimu
 
Kiswahili cha Mkenya na Mtanzania huwa unawahi kukielewa kipi?Au kiingereza cha Mganda na Mnaigeria huwa unakielewa kipi zaidi?

Kiingereza cha hawa wenzetu kusini mwa sahara kinaeleweka nadhani hata watoto wa english medium wanawaelewa.
 
Jaribu kuzungumza na waingereza toka LIVERPOOL, unaweza kuhisi ni kichaga, si kichaga, si kipare, ni hatari.
 
Wa Scottish ndiyo hawaeleweki kabisaa!

Mimi huwa hata sijui kama wanazungumza kiingereza.
 
We mtoa mada hujui ngeli ya mwingereza akiongea huwezi sikia neno hata moja British accent sio mchezo kiujumla American English ni maarufu na imesambaa sana kupitia miziki films zote hizo ni American English
Kiengera ni cha waengereza BBC unaelewa zaid kuliko CNN au fox anaebisha hajui hata kiengereza ni nn
 
Movies na music vimefanya iwe rahisi kuwaelewa Wamarekani kuliko Waingereza. Ila Wanaigeria watolewe kwenye nchi zinazozungumza kiingereza.
 
Movies na music vimefanya iwe rahisi kuwaelewa Wamarekani kuliko Waingereza. Ila Wanaigeria watolewe kwenye nchi zinazozungumza kiingereza.
😂 wanatamka maneno kama yalivyo, hawataki shida. Na wanatumia nguvu kubwa kama ugomvi vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…