Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,480
- 7,443
Jeshi la polisi ni chombo muhimu sana kwa ulinzi wa taifa lolote lile.
Hiki ni chombo amabacho kina jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao.
Lakini katika kulinda usalama wa raia na mali zao polisi wanatakiwa kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ili kulinda haki za raia.
Raia nao wana wajibu wa kutii sheria za nchi ili kuhakikiasha amani na usalama wa nchi unakuwepo.
Kama raia akitokea akavunja sheria za nchi basi sheria ifuate mkondo wake.
Lakini kumekuwepo na lawama nyingi sana kwa jeshi la polisi. Kupiga watuhumiwa, kuua watuhumiwa na hata kudhulumu mali za watuhumiwa.
Hakuna anayepinga jeshi la polisi kutumia nguvu pale inapobidi. Lakini nguvu gani za ziada zinahitajika kwa mtuhumiwa akiwa mahabusu ya polisi? Kwa nini malalamiko ya watu kupoteza ndugu zao wakiwa mikononi mwa polisi ni mengi?
Sasa hivi Tanzania ni taifa lilioendelea hivyo linahitaji jeshi la polisi lisilokuwa na chuki na wananachi.