Nadhani Kuna mmomonyoko wa maadili katika jeshi la polisi,labda mmomonyoko huu unatokana na mfumo wa ajira uliokuwepo kipindi fulani ambapo,ajira nyingi walipata watoto wa polisi line.Kwa hiyo wanalindana wakifanya makosa/mambo ya kinyume na maadili ya kazi yao,utakuta wanalindana badala ya kurekebishana (hii inasababisha raia kunyimwa haki zao).
Kazi /Majukumu mama ya Jeshi la Polisi ni" kulinda Usalama wa raia na Mali zao," inasikitisha kuona baadhi Askari wachache wanafanya mambo kinyume.
IGP hawa Askari wachache watukutu,usiwafumbie macho,toa onyo kadi ya njano na wakirudia rudia wape kadi nyekundu kwa majibu wa sheria na taratibu na staff rules za Jeshi la polisi.ili jeshi la polisi lisipakwe matope.