Kati ya Profesa Kabudi na Daktari Samia nani msomi?

Kuna wazazi wanatakiwa wakataliwe na watoto wao hadharani.Hivi,mtoto anaweza kumpa laana mtu mzima yeyote anayeng'ang'ania aitwe mzazi?
 
Mlinganishe Prof Kabudi vs Profesa J, nitakuambia (kwa mtazamo wangu) Profesa J ana akili nyingi kuliko Profesa Kabudi (ni kwa sababu elimu ya mtu hupimwa pia kupitia matendo yake, mchango wake kwenye jamii, nk). Na ukija kwa huyo mwingine, tulishakubaliana kitambo!

Udaktari unaotambulika rasmi ni wa aina mbili tu; wa kusomea shahada ya kutibu binadamu, wanyama, nk. Na ule wa PhD unaohusiana na ukufunzi kwenye vyuo, nk! Nyerere alipewa hizo PhD za heshima zaidi ya 20 kutoka vyuo tofauti duniani kote! Na bado hakuwa kujiita Daktari! Vivyo hivyo kwa Mkapa!

Ni vizuri kama huna sifa nilizozitaja hapo juu, usikubali kuitwa Daktari! Kwa sababu utakuwa umekubali kudhalilishwa mbele za watu mchana kweupe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…