Kati ya samaki wa maji chumvi/bahari na maji baridi unapenda yupi?

Kati ya samaki wa maji chumvi/bahari na maji baridi unapenda yupi?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Kila mtu na anavyoonja ladha kinywani mwake, kuna sisi wengine samaki ni samaki tu bora atengenezwe vizuri hatuchagui maji bahari wala chumvi.

Ila kuna watu wanasema mara samaki wa maji chumvi sio mtamu kama wa maji bahari na wengine wanasema samaki wa maji baridi ni matamu kuliko wa maji chumvi.

Kwa upande wako, samaki wa maji gani ndio unapendelea zaidi?
 
Yaani unataka kusema samaki kama mbala na kitoga kutoka Ifakara, samaki kama sangara na Sato kutoka Ziwa Victoria, Migebuka kutoka Ziwa Tanganyika wamepitwa ladha na samaki wa baharini wenye chumvi!
 
Asee sipendi samaki na wenzake kina dagaa
Duh itakua una matatizo wewe

Nilienda hospital nikapigwa sindano damu ikaruka yule nurse akanambia nyie mnakula samaki sana ndo mana mna damu nyingi
 
1.Sangara

2.Kambale

3.Ngisi

4.Kamba kwa aina zake zote

Imeisha iyo
 
Duh itakua una matatizo wewe

Nilienda hospital nikapigwa sindano damu ikaruka yule nurse akanambia nyie mnakula samaki sana ndo mana mna damu nyingi
Alikudanganya huyo 😂😂😂
 
Duh itakua una matatizo wewe

Nilienda hospital nikapigwa sindano damu ikaruka yule nurse akanambia nyie mnakula samaki sana ndo mana mna damu nyingi

Kwa uzoefu wangu wa kufanya kazi hospitali ... damu ikiruka kwa speed hivyo huwa kuna 60% possibility kwamba huyo mtu ni HIV+ 🤦‍♀️
 
Kwa uzoefu wangu wa kufanya kazi hospitali ... damu ikiruka kwa speed hivyo huwa kuna 60% possibility kwamba huyo mtu ni HIV+ 🤦‍♀️
🤣🤣🤣🤣🤣 unanitishaaaa?
Kipindi iko nilimpeleka wife hospitali alikua na mimba na kashajifungua since septembre na tukapimwa sote tupo vizuri tu

Sijaukwaa bado na gridi ya taifa ipo mbali nami
 
🤣🤣🤣🤣🤣 unanitishaaaa?
Kipindi iko nilimpeleka wife hospitali alikua na mimba na kashajifungua since septembre na tukapimwa sote tupo vizuri tu

Sijaukwaa bado na gridi ya taifa ipo mbali nami

Heheheh ndio maana nikatumia 60% tu 😁
 
Samaki wa maji baridi ni habari nyingine ni watamu sana na wana ladha nzuri na hawana shombo kama la samaki wa baharini

Sato, Kitoga, Sangara watabaki kuwa samaki bora wa wakati wote Tz

Kitu kitamu cha baharini ni dagaa mchele wale ukipata mpishi mzuri unainjoi mboga yake
 
napenda sana nyama ya kamongo esp kale ka mlija ka katikati kalivyo kama mpira flani na mayai ya samaki yaliyo chemshwa, na kichwa cha sangara mnono alie chemshwa nivute ule ubongo😋😋 naishiwaga pawa
 
Baharin kuna Samaki wazuri na watamu zaidi..

Ingawa asilimia kubwa wana Miba sana.

Hawa wa maji baridi ni wananyama sana.

Hata DAGAA, wale wa baharini wana miba mingi ukilinganisha na hawa wengine mfano wale Dagaa mnaitq DAGAA wa Nyama..
 
Back
Top Bottom