Kati ya Songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na ufugaji na kilimo?

Mara mia uende singida coz iko jirani na miji mikubwa ya soko kama Dar Arusha,mwanza na Dom,,pili ni transit,,Ruvuma hata ulime au ufuge hakuna soko,dar iko mbali,pili miundombinu ya barabara na umeme ni shida ,mwisho iko kanda ya kilimo hakuna mzunguko wa pesa,
Last hata ukilinganisha maendeleo na ukuaji wa miji hii Singida iko mbele ya Dar
 
Sasa hivi barabara zimefunguka uelekeo wote, vijiji vyote ukiwa unatokea barabara ya njombe viko accessible, wilaya ya namtumbo pia barabara ya uelekeo wa mtwara ni lami tupu, koote huko ardhi ina rutba na mvua za kutosha, na wenyeji hawana maneno ukitua popote ulizia ofisi ya mtendaji nenda kajitambulishe eleza lengo lako utasaidiwa bila shida, ardhi ipo ya kutosha. Kwa vile unaenda vijijini basi ni vizuri kuchukua barua ya utambulisho kutoka huko utokako, na kama ulkuwa mwajiriwa ukaacha kazi beba vitambulisho vyako. Ruvuma zao kuu wanalolima ni mahindi, pia wanalima maharage, kahawa, korosho, karanga, mihogo nk, kifupi ardhi ni inakubali mazao kibao, niwewe tu. Na kwavile wewe unataka kwenda kuishi hukohuko nakushauri tafuta vijiji ambavyo haviko mbali sana na mji, Maeneo kama Mlilayoyo, Mtangimbole, Shuleyatanga, jirani na barabara kuu na pia huduma za umeme na zingine za kijamii, unaweza kujikuta unafuga samaki pia ambao wanahitajika sana Songea. Kiikubwa tafuta kijiji uhame kwanza mkuu, ukipata hata ekari 10 za jirani kijijini we lipa jenga kajumba kako zungushia uzio anza mambo.
Dah we mjumbe Safi sana umeeleza facts yaani nimependa
Binafsi hili suala la kuwekeza katika sekta ya kilimo inakuna sana nilikuwa najiuliza niende wapi nikajichimbie huko hata kama ni kijijini sana mi niko poa kabisa, naanza kupata mwanga na nilifocus sana RUVUMA kulingana na hali ya hewa ya kule na mazingira ya soko baada ya kuzalisha. Miki nipo Iringa ila nikilinganisha hali ya hewa ya hapa ni nzuri sana but in my opinion naona si poa sana kwa ufugaji wa kuku maana ni baridi ila kama wapo watakao nishauri kubaki hapa na wakanipa muongozo itakuwa poa pia
 
Upon iringa sehem gani?
 
Samahani Mkuu nimezaliwa Dar japo huko Mtwara ni Nyumbani kwa upande wa ' Bidashi ' wangu ( Mum ) pamoja na Lindi ila sijawahi ' Kukanyaga ' kabisa Mtwara isipokuwa Lindi hasa ' Nachingwea ' niliwahi kwenda mwaka 1988 kama siyo 1989. Mkoa ambao nimeenda na naenda sana ni wa Mara ( Musoma ) ambako ndiko ' Mshua ' wangu ( Dingi ) anatokea. Na naenda sana Mara ( Musoma ) kwasababu ya Samaki wengi na naogopa kwenda Mtwara kwakuwa Panya ni wengi halafu wametukuka. Narudia tena kukuomba usipoteze kabisa muda wako kwenda sijui Ruvuma au Singida huko hakuna Kitu halafu Watu wa huko ni ' Washamba / Mambwigira ' sana.
Povu wa huko Songea naona walishakula na kutafuna ndugu zako nini? Maana huko nasikia nyie wa Mara mkienda na wake zenu wakikunwa kidogo na wangoni wanaanza kuwadharau, Nasikia wangoni ni Expert wa kukamua papuchi
 
Mkuu nenda singida, kwa ufugaji wa kuku utafauru mi mwenyewe mwezi kama miwili mbele ntakua na Safari yakwenda huko nataka nikawe mkulima na mfugaji mpaka kieleweke.
 
Singida kuna kuku wengi wa kienyeji halafu bei rahisi lakini kati ya mkoa wa Singida na Ruvuma kwa kuishi na kufanya shughuli za kilimo ni bora uende Songea. Singida ni kukame sana kuliko Ruvuma
Nyie kumbe hamjui, bora singida ili usafirishaji kwenda makao makuu ya nchi hata mwanza ni rahisi sana , sasa huko ruvuma au awe anauza msumbiji?
 
Mara mia uende singida coz iko jirani na miji mikubwa ya soko kama Dar Arusha,mwanza na Dom,,pili ni transit,,Ruvuma hata ulime au ufuge hakuna soko,dar iko mbali,pili miundombinu ya barabara na umeme ni shida ,mwisho iko kanda ya kilimo hakuna mzunguko wa pesa,
Last hata ukilinganisha maendeleo na ukuaji wa miji hii Singida iko mbele ya Dar
Ati??
 
Sio ati soma uelewe,kwa hoja hizo hapo 100 times Singida kuliko Songea,hata mji wa Singida ni mkubwa na unaendeleaj kuliko songea
Tatizo limeanzia kwa " singida kuwa mbele ya dar". Soma vizur mpaka mwisho
 
Mkuu pole nmekuambia soma post yako ya kwanza mpaka jamaa akauliza Ati?
Mwishon umemalizia singida ipo mbele ya dar. Jaribu kurudia halafu tuambie kuwa ulikosea au thibitisha kuwa singida ipo mbele kwa dar
 
Mara mia uende singida coz iko jirani na miji mikubwa ya soko kama Dar Arusha,mwanza na Dom,,pili ni transit,,Ruvuma hata ulime au ufuge hakuna soko,dar iko mbali,pili miundombinu ya barabara na umeme ni shida ,mwisho iko kanda ya kilimo hakuna mzunguko wa pesa,
Last hata ukilinganisha maendeleo na ukuaji wa miji hii Singida iko mbele ya Dar
Soma hii post niliyo-quote mwishon umesema hata kimaendeleo singida ipo mbele ya dar
 
Sasa hivi barabara zimefunguka uelekeo wote, vijiji vyote ukiwa unatokea barabara ya njombe viko accessible, wilaya ya namtumbo pia barabara ya uelekeo wa mtwara ni lami tupu, koote huko ardhi ina rutba na mvua za kutosha, na wenyeji hawana maneno ukitua popote ulizia ofisi ya mtendaji nenda kajitambulishe eleza lengo lako utasaidiwa bila shida, ardhi ipo ya kutosha. Kwa vile unaenda vijijini basi ni vizuri kuchukua barua ya utambulisho kutoka huko utokako, na kama ulkuwa mwajiriwa ukaacha kazi beba vitambulisho vyako. Ruvuma zao kuu wanalolima ni mahindi, pia wanalima maharage, kahawa, korosho, karanga, mihogo nk, kifupi ardhi ni inakubali mazao kibao, niwewe tu. Na kwavile wewe unataka kwenda kuishi hukohuko nakushauri tafuta vijiji ambavyo haviko mbali sana na mji, Maeneo kama Mlilayoyo, Mtangimbole, Shuleyatanga, jirani na barabara kuu na pia huduma za umeme na zingine za kijamii, unaweza kujikuta unafuga samaki pia ambao wanahitajika sana Songea. Kiikubwa tafuta kijiji uhame kwanza mkuu, ukipata hata ekari 10 za jirani kijijini we lipa jenga kajumba kako zungushia uzio anza mambo.
Unit cost of production ni kubwa huko Songea kwa peasant unless ww ni large scale farmer
Barabara sio hoja hata rukwa au mbeya kuna barabara lakini kilimo hakijawa na tija kwa mkulima mdogo sababu ya soko kuwa mbali so madalali ndo mnawafanyia kazi
Better Morogoro kama ishu ni kilimo,songea hakuna soko huko
 
Mara mia uende singida coz iko jirani na miji mikubwa ya soko kama Dar Arusha,mwanza na Dom,,pili ni transit,,Ruvuma hata ulime au ufuge hakuna soko,dar iko mbali,pili miundombinu ya barabara na umeme ni shida ,mwisho iko kanda ya kilimo hakuna mzunguko wa pesa,
Last hata ukilinganisha maendeleo na ukuaji wa miji hii Singida iko mbele ya Songea
 
Mkuu pole nmekuambia soma post yako ya kwanza mpaka jamaa akauliza Ati?
Mwishon umemalizia singida ipo mbele ya dar. Jaribu kurudia halafu tuambie kuwa ulikosea au thibitisha kuwa singida ipo mbele kwa dar
ooh true,typing error ps alipitiwa,nilikuwa namaanisha Singida inakua kwa kasi na iko mbele ya Songea not Dar
 
Hapo sawa mkuu!. Ok nashukuru sana kwa mawazo yenu yananijenga na kunipa changamoto za kutosha kuweza kufanya maamuzi.
Mungu awabariki na bado napata challenges
 
Kiukweli Mimi nilikuaga najua Dar ndo mambo yote... Mwaka Jana nilienda Singida kupiga kazi flani for around 5 months.. Kazi imeisha lakini nimejikuta safari za Singida haziishi, sio kufanya kazi kama ile niliokwenda kuifanya mwanzo, Bali michakato ya kiujasiliamali.... Kuanzia kwenye Kuku wa kienyeji, mafuta ya alizeti, Asali mpaka Vitunguu... Usipoamua kuchuuza hizo bidhaa, basi Lima au fuga kabisa.... Nenda Singida Mzee baba..
 
Back
Top Bottom