Kwa Singida utategemea kilimo cha mvua sana sana,ila utalima Alizeti hiyo ni simple sana,Nenda Singida Vijijini has kule pembeni kabisa karibu na Wilaya ya Hanang (mf.Kijiji kimoja kinaitwa Ngamu saa mbili hadi Singida town) ardhi iko na rutuba. Utaanza kukaa kijiweni kuna umeme utakodisha nyumba elf 15-30 kuna umeme,na huduma zingine za kijamii zipo.
Utakodisha sijui ni eka ngapi lakini ni vizuri ukaanza na eka 10-20. Bei yake ni rafiki kuanzia kukodisha hadi kulima
Mfano wa mchanganuo wa eka 10 katika alizeti.
Kukodisha ni elf 50-100 inategemeana na majira na anayekodisha ana changamoto kiasi gani ,Tufanye wastan elf 80/eka
so
Kukodisha
Tsh 8,0000 x eka 10=800,000. Kukodisha ,bei iko very flexible itategemeana na wewe.
Tsh 40,000x 10=400,000 hapa ni Kulima kwa ajjili ya kuweka mbegu/Kupanda.hiyo ni bei ya trekta ya ng'ombe ni elf 30.
Tsh 5,000 x 10=50,000 hiyo ni mbegu ya kienyeji nyeupe( sisi tunaita serena) inatoa ukiamua kukamua mafuta.
Tsh 30,000x10=300,000 hii ni palizi kumbuka alizeti ina palizi moja tu.
Tsh 5,000x10=50,000 hapa ni kukata kwa ajili ya kupiga piga
Tsh 20,000x1= 20,000 kukusanya toka shambani hadi sehem utakayo pigapiga.(sisi tunaita kupura) kwa eka zote.
Tsh 20,000x1 =20,000 kupiga(Kupura) na kupepeta-kwanza hapa we fanya hiyo kazi ni rahisi sana.
Tsh 5,000x1 =5,000 Uzi wa kushonea pamoja na Sindano
Tsh 600x 120(idadi ya gunia) =72,000 hii ni mifuko ya kuhifadhia.Japo ukipata safari ya Arusha utapata kwa tsh 300.
Tsh tufanye 50000 kodisha sehem ya kuhifadhia,japo unaweza kuhifadhi bure au ukaweka hapo nje ka nyumba ina geti.
Jumla kuu =(1,767,000) au
Eka moja inatoa kati ya gunia 10-15. Lets make 12/eka=120 Kuuza hadi kufikia December bei yake ni hadi elf 75.Lakini we uza kwa mwezi wa 9 ili ujiandae kukodisha tena bei ni kati ya elf 50-55 .Uza kwa elf 50
Mauzo
Idadi bei@ Jumla kuu
120x 50,000 =6,000,000
Mauzo-Gharama = Faida
6,000,000 - 1,767,000 =4,233,000
Sasa rudi tena shambani kafanye eka 30.Mavuno yake ukakamue mafuta,utauza mafuta,mashudu,na mafuta ghafi-ingawa hayana bei sana haya crude oil.
Pia kuna watu wanauza mimea ikiwa shambani,amepanda amepalilia afu mnafanya tathimini unanunua,Wakulima wengine wanauza gunia kwa elf 25 ikiwa shambani akivuna anakulipa(Sisi tunaita tunatoa advance)
Mengine unaweza kulima vitunguu ila ukishakuwa mwenyeji hapa ndio patamu zaidi,japo risk ni kubwa sana,ila ukifanikiwa baasi,Utalima mahindi pia.
Risks zake zaweza kuwa,ni mda mrefu tangu umepanda hadi kuvuna, Kukodishiwa eka 1 watu wawili-Hapa dawa yake ni mfanye kwa maandishi,Wadada wazuri na watajitaidi kwa kila namna akumiliki ata kwa kutumia miundo mbinu-Ila itakuwa ni uzembe wako,Mvua kuchelewa n.k
Ufugaji wa kuku ,tutafuga chotara,kwa vile wanakuwa haraka,pia watu wa huku hawapendi wa kisasa wanaamini huwa wanakuzwa kwa dawa,wanaume wakila wanaota matiti.
Mchanganuo wake tutafanya siku tukionana kijijini.