Kati ya udereva wa mjini na masafa marefu upi ni mgumu.

Kati ya udereva wa mjini na masafa marefu upi ni mgumu.

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
5,197
Reaction score
14,380
Tuseme dereva A anaendesha coaster transmission manual ambayo ni daladala route ni Mbezi to Mnazi Mmoja dereva B anaendesha Special hire gari ni Ile Ile kakodiwa kuwapeleka abiria Arusha kwenye Send off.

Nani ana kibarua kizito.
 
Kazi ni kwenda masafa,barabarani kuna vioja,kama hujaaguliwa unakufa mapema sana,asikudanganye mtu,hakuna dereva wa masafa ambaye hana mganga wake.
 
Nyie watu mnaijua kazi ya daladala? Unaamka SAA 10 usiku na unalala SAA 7 usiku alafu upo na manual transmission kwenye foleni za mjini .... Gari imechoka kilakitu kigumu kuanzia usukani Hadi gear zinaingia Kwa jasho.
Dereva wa special hire na rubani wa ndege hawana tofauti kwenye utanashati huwezi kumfananisha na dereva wa daladala
 
Lakini yeye hajasema udereva wa gari zipi mkuu.

Kauliza mjini na masafa wapi kuendesha kugumu japo pia mimi naona mjini ni jau zaidi muda wowote unapata msala wa kugonga mtu au gari.
 
Back
Top Bottom