Kati ya walio tuma ujumbe wa moja kwa moja ni huyu padre siku ya kuapishwa rais Samia

Kati ya walio tuma ujumbe wa moja kwa moja ni huyu padre siku ya kuapishwa rais Samia

Pendaelli

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
13,075
Reaction score
38,625
Screenshot_20251104-092423_YouTube.jpg

Wakati wa sherehe za kiapo cha rais zilizofanyika jana, Padre huyu wa Kanisa Katoliki alionekana kuvaa stola ya rangi ya zambarau badala ya nyeupe au dhahabu kama inavyozoeleka kwenye matukio ya furaha.

Kwa mujibu wa utaratibu wa Kanisa, rangi ya zambarau huashiria toba, maombolezo, na upatanisho.

Kwa kuwa kipindi hiki kimekuwa na kumbukumbu za vurugu na vifo vilivyotokea kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi,baadhi ya watu wanasema huenda mavazi hayo yalibeba ujumbe wa toba na uponyaji wa taifa, au heshima kwa waliopoteza maisha.
Lakini mimi naona ni ujumbe wa moja kwa moja kwa mamlaka ingawa kwa upeo wao wanaweza wasigundue.

Haiukuwa bahati mbaya baraza kuto mtuma askofu mkuu wa dodoma ama yoyote au katibu mkuu wa baraza badala yake amekuja padre tena kwa mwonekano wa kimaombolezo zaidi .

Tuseme tu taifa lilipaswa kuwa bendera nusu milingoti maana damu zisizo na hatia nyingi zimemwagika, na mara nyingi bila toba huwa haipiti hivi hivi.

Asante padre na kanisa kwa kutukumbusha ni wakati sasa wa kuomba toba na rehema pia upatanisho.
 
Ata baba yake na Benjamin Fernandez aliua
 
Back
Top Bottom