Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Pasco,

..mawazo yako ni sawa na ya Dr.Kashilila, katibu wa bunge.

..tofauti ndogo ni kwamba Dr.Kashilila amekwenda mbali na kueleza kwamba baada ya mswada kusimamishwa na hoja kutolewa kura zingepigwa. sasa mtego upo hapo kwenye KURA.

..bila kutueleza kwamba you have some info that we dont have, kwamba kulikuwepo na wabunge wa kutosha waliokuwa wamepania mswada usipite ikiwa CDM wange-invoke hicho kifungu unachosema, then naweza kukubaliana na hoja uliyoileta hapa kwamba CDM made a mistake.

..vinginevyo inawezekana kabisa CDM walishajua watashindwa kwa namna yoyote ile, na wakaamua kufanya hicho walichoweza kufanya.

NB:

..naomba nikukumbushe kwamba you can invoke kila pingamizi unalolitaka ndani ya bunge, lakini at the end of the day lazima uwe na KURA za kutosha.

..hivi kuna wakati wowote ule in this whole process ambapo CDM wamejaribu kuwashawishi/kuwa-rectruit wabunge wa vyama vingine wawaunge mkono ktk kuupinga mswada wa katiba?
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Hindi ndivyo nisemavyo kila siku, watu waacha mada muhimu na kujikita katika kuposha mada.
Hata kama kifungu 86 kilishatumika huko nyuma, Chadema walipaswa kukumilisha ili hansadi ziweke kumbukumbu na miaka 100 toka sasa wajukuu zetu wakija kutusuta waje waseme wapo waliojaribu wakazidiwa nguvu na watawala WALIOKUWEPO hivyo kutohukumiwa.
Kwa hili ni uungwana wa kawaida kusema Chadema hawakuwa makini na wamepoteza fursa ambayo kiutaratibu na kimuongozo wa bunge kifungu 86 wamechemsha.
 
 
Nashangaa kwa nini hadi leo post hii hajawekwa kule juu na title ya uzi huu haijabadilishwa!
 
Jamani kila kitu chama cha magamba walishapanga, sasa unachowalaumu chadema ni nini? Na we ni gamba (snakes ;>)
 
Chadema hawajachemsha!. Saa hizi wako lunch Ikulu!.
 

Nimejaribu kuipitia hii post yangu na kulinganisha ni kinachoendelea nimekujikuta I was right somehow.

1. Kitendo cha Chadema kumuona rais Jakaya Kikwete, ni dalili ya kukubali yaishe, hili ni jambo jema!
2. Kwa mujibu wa taarifa rasmi, wataipa tume ushirikiano na tutaweza kusonga mbele, hili pia ni jambo jema.
3. Nakiri kuwa hoja yangu ya kuwaambia Chadema walikosea, imepigwa chini, hawakukosea, hivyo hawana sababu yoyote ya kuomba radhi.
Leo au kesho muswada unasainiwa kuwa sheria, this time Chadema wataalikwa kwenye signing ceremony, na kama kawaida yao watasusa sherehe lakini wataipa tume ushirikiano!.

All and all, life goes on.

Wasalaam

Pasco.
 
Kama nakuona vile ulivyo na furaha! 'Hongera sana' kwa kuyaona haya mapema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…