Pasco, hivi wangetoa hoja kwa kutumia kanuni ya 86 mjadala ungesimamishwa automatically au Spika angeuliza Bunge na Bunge kuamua? Unafikiri Wabunge wa CCM wangekubali kusimamisha mjadala baada ya kuulizwa na Spika?
Sidhani kama wame lose; ukiangalia zaidi utaona kuwa wao wamegain kwa sababu mstari umechorwa kati ya wale wanaoamini Rais na wana CCM wanaweza kufanya yote wayatakayo na wale ambao wanaamini the CCM government is in contempt of the people. Tofauti hii ya maoni ni ya muhimu. Rais na CCM wameweza kulazimisha sheria waitakayo wao kupita - kama walivyofanya kwenye sheria ya gharama za uchaguzi - lakini mwisho wa siku watajikuta ni wao pekee ndio wanaandika hiyo Katiba mpya na wale wanaowaamini au kuwafuata. Je kwa vile sheria imepitishwa ina maana mchakato utakuwa halali kwa kuangaliai first principle? Ukweli ni kuwa CCM hawakuhitaji hoja za CDM au za mtu mwingine yeyote juu ya mswada huu, walikuwa na mawazo yao na wameyatekeleza bila kuzuiwa kwani hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuwazuia.
Siyo lazima. Watanzania ambao hawaamini katika uhalali wa mchakato huu kwa sababu umevunja the First Principle wanaweza kuupinga, kukataa kushiriki na kuwahamaisha wengine wasishiriki kwa hoja ambazo zitaonesha kuwa mchakto mzima umekosewa toka mwanzo na haukuwa nafasi ya kufanikiwa kwa sababu ulikuwa ni wa kulazisha kwa kutumia tyranny of thte majority. Wananchi hawawezi kulazimishwa kuitii tume ambayo hawaamini ni halali. Tume kupitishwa na kuundwa hakuipi uhalali (legitimacy) kwani uhalali wa sheria hauji kwa kupitishwa tu bali pia kwa uhalali wa hoja zake na mantiki yake. Mwanadamu hawezi kulazimishwa kutii kitu ambacho ni kinyume na dhamira yake, ukweli na mantiki yake au kile ambacho kinaonekana kwa makusudi kimetengezwa ili kumkandamiza.
Wanaoamini kuwa sheria hii ni halali na kuwa mchakato ni halali wanayo haki ya kujitokeza kwa furaha kwenda kutoa maoni yao. Wale ambao wanaamini mchakato huu umesurp power ya wananchi na kuwa umelazimishwa wanayo haki ya kukaaa kushiriki na kuhamasishana kutoshiriki hadi hoja zao zisikilizwe vinginevyo wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa itakapokuja kura ya maoni wataenda na kuhamasishana kupigia kura ya "hapana" hiyo referendum na kuzuia Katiba Mpya itakayopitishwa na wana CCM.
Wanaweza kukataa kusikiliza maoni juu ya mchakato na wanaweza kabisa kulazimisha watu waje kwenye tume yao lakini watakapoletwa swali hilo kwa wananchi hawana namna ya kuwazuia wale wasioshiriki mjadala kupiga kura ya hapana. Unless waseme watakaopiga kura ya maoni ni WALE TU walioshiriki kwenye kutoa maoni! Kitu ambacho hakimo kwenye mswada huu hadi waufanyie mabadiliko.
Mzee MM
Nakubaliana na wewe kiasi kikubwa. Napenda kufanya makusanyiko(Summarize .. i hope niko sawa kwenye translation) at the end of the day tunachotaka ni katiba BORA mpya na sio BORA katiba, kama Pascal anaona kuna makosa yameshafanyika (kama kweli yapo) na kwa maelezo yake basi tuache uchafu uendelee kutokea kwa kweli napata shida kuelewa ajenda yake, maana naamini kila mtu mwenye nia njema na nchi hii anaelewa katiba tuliyonayo imetufikisha wapi.
Nilitegemea sana Pascal aeleze makosa ambayo tumefanya kisha namna ya kurekebisha ili lengo letu liwe hilo moja kupata katiba bora(sio bora katiba), lakini inavyoelekea bwana Pascal anataka kutuaminisha kuwa madhali kuna kosa moja(kwa kweli kwa upande wa CCM na washirika wake makosa ni mengi mno kuliko hilo moja ambalo Pascal anakazana kulielimisha) basi sasa tuwape watu wale wale wanaofanya mambo kwa mazoea(eti sababu babu alifanya nasi tufanye) tuendelee na tusubiri watu wale wale watuamulie mustakabali wa taifa baada ya 2015.
Kwangu mimi huu ni upotoshaji mkubwa unaotaka kuendeleza, kama utakumbuka nimetoa angalizo(comments) kwenye moja ya post yako ya kuendeleza kitu wenzetu wanita "DIVERSIONARY TACTIS" ili hoja za msingi zisijadiliwe tena, tuendelee na mjadala wa CDM na CCM, Wanaharakati na CCM, (wanazuoni, wasomi, makundi mbali mbali na CCM), e.t.c
Jamani KATIBA ni fundamental law, its the basis of your life. Wengi tunafikiri katiba ni sheria kama sheria zingine lakini kwa kweli katiba ni msingi wa maisha yetu, ndo una define sisi ni watu wa aina gani. Labda kwa kuongezea kwenye mjadala niliongalia jioni ya leo, kuna swali aliulizwa Tindu Lissu kuhusu ufahamu wa katiba leo jioni kama watanzania wanaifahamu katiba,,,, naomba nimpe mtazamo wangu binafsi kuwa watanzania wanaijua katiba yao vizuri sana kupitia maisha yao wanayoishi, wanavyokula, wanavyopata huduma za jamii (mf. afya, elimu e.t.c) huo ndio ufahamu wa katiba ambao unaweza kuwapelekea. Hakuna sehemu duniani unaweza kupata katiba ambayo hata 25% ya wananchi wake wanaifahamu ki elimu dunia (academically)... NOOOOO!!!!
TUWE SERIOUS NA HII MIJADALA.