Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Kuna sababu zaidi ya 99% kua mgombea wa CCM amepewa ushindi na katiba ya JMT kwa sababu za msingi zifuatazo, labda wananchi waamue wenyewe kutokujali katiba hii.
SABABU ZENYEWE
1. Mwenyekiti wa CCM na mngombea wa Urais ndiye anayewateua mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na makamishna wake. Yaani kocha wa Yanga ateue waamuzi mchezo kati ya Yanga na Simba?
2. Matokeo ya Uchaguzi hayahojiwi Mahakamani. CCM wanajua kabisa kwamba hata wasiposhinda Mwenyekiti wa NEC akiamua kumtangaza mshindi ndio ingeshatoka hiyo na atakayehoji anaweza kudhibitiwa kisheria. Kwahiyo hapa Mwenyekiti anaweza kutangaza tu hata asiposhinda.
3. Katiba inamtambua Rais mpaka pale atakapoapishwa mpya.Kwahiyo haijalishi kua anagombea Urais bado yeye ni Rais na anaweza kufanya maamuzi yeyote ya nchi akiwa katika wadhifa huo. Yaani yeye ni Rais na hapo hapo ni mgombea na anatumia rasilimali zote za umma.