Katiba inakupa uhuru wa kukosoa/kutoa maoni haikupi uhuru wa kutoa lugha za kuudhi na kuchonganisha

Sana tu, waambie akitoka atakuwa kanyooka.Yule muota ndoto haoti tena siku hizi
Watu kama nyinyi ndio utakuta simu unaazima ili kupost huu uharo wako na Kula yako ni kwa jirani

In God we trust
 
Mkapa alirudia tusi mbele ya JPM kwa mara ya pili akiwatukana watanzania zaidi ya mil 6 kuwa ni wapumbavu na malofa,JPM akakenua meno akichekelea!Kwako hilo sio tusi wala lugha ya kuudhi!

Point of correction. Hakutukana watanzania. Aliwatukana wale wajinga na malofa. Sikusikia popote aliposema nyie watanzania ni wajinga na malofa. Ila kwa huyo zezeta wenu Tundu Lissu alimtaja Raisi Magufuli na Raisi Mstaafu mzee wetu Mwinyi waziwazi. Sijui ni mwanasheria wa wapi anayeweza kutoa kashfa kwa kutaja watu waziwazi. Watoto wa mjini wanasema anatafuta kiki. Ataipata tu.
 
Tundu lissu kweli anawatoa jasho ccm na mtukufu magufuli yaani hamna speech ya lissu ilokosa mjadala au kumpa kesi mara analipwa na acacia mara lawyer anaegopa kushtakiwa ......all i can say its the govt vs tundu the great lissu ....
 
Rafiki wewe naona huna mpya zaidi ya kupigia makofi kila atakacho kisema Lisu.Soma uchambuzi wangu hapo ndo utagundua hoja zote alizotoa ni za uongo na uchonganishi

Nimesoma uchambuzi wako lakini naona umelalia kwenye kujipendekeza tu kwa wenye madaraka. Hivi nikuulize ni lazima uishi kwa kujipendekeza kwa wanaume wenzio ndio watoto wako wafanikiwe kutoa makinikia chooni?
 
La msingi hapa kila mmoja ahukumiwe kwa makosa yake lakini siyo kufanya references za nani kafanya nini na kufanyiwa nini! Ni vema ukijua fulani kafanya kosa, mimi, wewe au ninyi tumchukulie hatua stahiki za kisheria na siyo kunyosheana vidole au kufanya makosa yaleyale waliyoyafanya wao. Huo utakuwa ni ujinga mara dufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakitukana kina sizonje mnakenua meno ila lisu akisema ukweli mnamkamata .yani unamkamata mtu kwa kukuambia ukweli unasema ametoa lugha za kuudhi , ndio zitakua ni za kuudhi kwasababu hampendi kuambiwa ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea hoja za msingi sana.........

Ingekuwa,wanaccm wote wana mawazo kama yako, hakika nchi hii isingefika hapa tulipo ambapo nchi ipo kwenye mfumo wa vyama vingi theoretically lakini practically tupo kwenye mfumo wa chama kimoja cha CCM.
 
ahsante kwa kutufunua uelewa
 
ahsante kwa kutufunua uelewa
 
Maelezo mengi but no sense in it
 
meanwhile katiba ina mruhusu JPM kuita wapinzani VILAZA.
Kilaza ni kivumishi cha sifa,,,Alimaanisha wanashindwa kuelewa kuwa katiba hairuhusu mtu kutumia lugha za kuudhi na kuchonganisha ,Ni hawa hawa pia hawajui kuwa Tanzania Ilisha kombolewa mikononi mwa wakoloni hata CIVICS/URAIA Hawajui .Mtu asiejua kitu na hataki kuelimishwa wewe ungemuitaje kwa mfano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…