Katiba inasemaje kuhusu uteuzi wa Bashiru Ally?

Katiba inasemaje kuhusu uteuzi wa Bashiru Ally?

Naomba unisome vizuri.JF ni sehemu ya kuelimishana nami najua kuwa atakalo rais liwe huwa linakuwa ila Kikatiba na kisheria.Ningetegemea uweke vifungu vya katiba/sheria ili tuwe na mjadala mzuri!
Mkuu MIGNON, nimeshawishika nami kujiunga katika mjadala huu wa 'kuelimishana' juu ya katiba na sheria.

Sijaona ukipewa jibu la kukuelimisha/kutuelimisha.

Lakini, pengine iwe ni kutumia tu fursa kuelimika, na sio kwamba hicho kilichomo kwenye sheria/Katiba kinamanufaa yoyote kwa wakati huu tuliomo; kwani Katiba na sheria hata kama zipo zinazozungumzia uteuzi huu, mteuzi kama ujuavyo hadi sasa hazuiwi na Katiba au sheria yoyote kufanya anayoona yeye yanafaa.

Kuna mifano mingi inayoonyesha kuwa kiongozi huyu hazuiwi na sheria wala katiba. Kwa hiyo pengine kuhoji/kuelimishwa unakotafuta hapa kutokana na uteuzi huu, pengine ni kujiridhisha tu kuwa Katiba na sheria zipo zinazohusu aina ya uteuzi huu, hata kama hazifuatwi.

Nami pia ningependa kuelimika tu juu ya hili, hata kama sihoji chochote juu yake, kwa kujua kuwa ni utaratibu wa kawaida wa mteuzi.
 
Sijui unataka kujua nini. Kikatiba raisi anayo haki ya kumteua Katibu kiongozi. Kama matakwa ya kikatiba yamekidhi huenda ya kisheria yamekidhi pia. Anayaeteuliwa anatakiwa awe mwananchi. Aliyeteuliwa ni Nshomile Mtanzania halisi wala si Mganda Kyaka. Hii ina maana naye amekidhi matakwa ya kikatiba na kwa hiyo ya kisheria. Una swali lingine?
Nafasi za uteuzi za
1. Wakurugenzi
2. DAS + RAS
3. Makatibu

Hawa wotee ni watumishi wa umma.
Huwa kama promotion kwao.

Sasa kwanini Magu anavunja Sheria hii ya utumishi wa umma?

#YNWA
 
Ujanjaujanja Mwingi Unafki Bhalaa
Ni hivyo, hata mkulima anaweza kuwa mtumishi wa serikali muda wowote na kuwa katibu kiongozi, mbona Hatu shangai mawaziri ambao wanateuliwa kuwa wabunge then anakuwa waziri, mambo ni Yale yale tu
 
Ni muendelezo wa uvunjivu wa katiba yetu tena wa waziwazi kabisa. Hii ni aibu kubwa mno.

Mambo ni ku force force king tu.
 
Watumishi waandamizi wa umma ni nani na nani?

..utumishi wa umma ni serikali kuu na taasisi zake.

..watumishi waandamizi ni manaibu katibu wakuu, makatibu wakuu, na wateule wa raisi ktk taasisi za serikali.
 
Mkuu MIGNON, nimeshawishika nami kujiunga katika mjadala huu wa 'kuelimishana' juu ya katiba na sheria.

Sijaona ukipewa jibu la kukuelimisha/kutuelimisha.

Lakini, pengine iwe ni kutumia tu fursa kuelimika, na sio kwamba hicho kilichomo kwenye sheria/Katiba kinamanufaa yoyote kwa wakati huu tuliomo; kwani Katiba na sheria hata kama zipo zinazozungumzia uteuzi huu, mteuzi kama ujuavyo hadi sasa hazuiwi na Katiba au sheria yoyote kufanya anayoona yeye yanafaa.

Kuna mifano mingi inayoonyesha kuwa kiongozi huyu hazuiwi na sheria wala katiba. Kwa hiyo pengine kuhoji/kuelimishwa unakotafuta hapa kutokana na uteuzi huu, pengine ni kujiridhisha tu kuwa Katiba na sheria zipo zinazohusu aina ya uteuzi huu, hata kama hazifuatwi.

Nami pia ningependa kuelimika tu juu ya hili, hata kama sihoji chochote juu yake, kwa kujua kuwa ni utaratibu wa kawaida wa mteuzi.
Swadaktaaa,ni kuelimishana kwani hatuwezi kubadili.Kule Jamhuri ya Twitter naona vipengele vimeanza kuwekwa na fununu za kuwa "afisa kipenyo"
 
Back
Top Bottom