MTK
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 8,924
- 6,854
Sijaafiki mtazamo wako wa kusema "Mchakato wa kutengeneza katiba ulivurugwa kwa ubabe wa CCM, rushwa na vitisho na kukiuka sheria ya mabadiliko ya katiba" kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za mchakato wa kuanzishwa Katiba Mpya. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 limezingatia na kuwekwa pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Sheria hii tangu ilipotungwa mwaka 2011 hadi tarehe 31 Desemba, 2013 na limechapishwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria ya Urekebu Sheria, Sura ya 4. Sheria ni nzuri mno na ipo wazi inaonesha kuanzia Jina lenyewe la Sheria, Matumizi, Tafsiri, Madhumuni, Uundaji wa Tume, Uteuzi wa wajumbe wa Tume, Muundo wa Tume, Hadidu za rejea, Kazi za Tume, Uhuru wa Tume, Kiapo cha wajumbe na Katibu wa Tume, Ukomo wa ujumbe, Sekretarieti, Gharama za Tume, Kinga kwa wajumbe wa Tume na Sekretarieti, Ukaguzi wa Hesabu zaTume, utaratibu wa utendaji kazi wa Tume, kuitisha Bunge Maalum.
Kuhusu hoja yako ya 2. Inayohusu "Muundo wa BMK uliandaliwa mahsusi kuiwezesha CCM kuupiku mjadala mzima" Wewe siyo mfuatiliaji wa mambo, hoja yako hii ni dhahania tu.
Bwana, Kama huna facts usiwadanganye Watanzania. Pennye ukweli tuwe wakweli, Jamani Bunge Maalum lilitishwa Sheria Na. 9 ya mwaka, 2013 na Tangazo la Serikali Na.394 la mwaka 2011 Amri ya 2 aya (r) SEHEMU YA TANO. Sehemu hii inahusu kuitishwa kwa Bunge Maalum ambapo litakalokuwa na wajumbe wafuatao: (a) wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; (b) wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; (c) wajumbe mia mbili na moja watakaoteuliwa na Rais kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar kama ifuatavyo: (i) wajumbe ishirini kutoka Taasisi zisizokuwa za Kiserikali; Sheria ya Mabadiliko ya Katiba [Sura ya 83 Toleo la mwaka 2014] (ii) wajumbe ishirini kutoka Taasisi za Kidini; (iii) wajumbe arobaini na mbili kutoka Vyama vyote vya Siasa vyenye usajili wa kudumu; (iv) wajumbe ishirini kutoka Taasisi za Elimu; (v) wajumbe ishirini kutoka katika makundi ya watu wenye ulemavu; (vi) wajumbe kumi na tisa kutoka Vyama vya Wafanyakazi; (vii) wajumbe kumi kutoka Vyama vinavyowakilisha Wafugaji; (viii) wajumbe kumi kutoka Vyama vinavyowakilisha Wavuvi; (ix) wajumbe ishirini kutoka Vyama vya Wakulima; (x) wajumbe ishirini kutoka makundi mengine yoyote ambayo yana malengo yanayofanana.
Kuhusu hoja yako ya 3. Inayohusu "Maoni yaliyowasilishwa na tume ya mabadiliko ya katiba yalikataliwa hata kabla ya kujadiliwa kulingana na mahitaji ya sheria". Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 imezingatia na kuweka pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Sheria hii tangu ilipotungwa mwaka 2011 hadi tarehe 31 Desemba, 2013kwa kuanzaia ambapo kazi hiyo ilianza na uundwaji wa Tume, utaratibu wa utendaji kazi wa Tume, kwa kuzingatia Utaratibu wa utendaji kazi, Mabaraza ya Katiba, Ripoti ya Tume, Uwasilishaji na uchapishaji wa ripoti hatimaye kuitisha Bunge Maalum ambapo taratibu zote zimefuatwa kwa uhalisia wake.
Cha kusikitisha zaidi ndg MTK, hoja yako ya 4 Inayohusu "Serikali ilijihusisha katika vitendo vya kuihujuma tume ya mabadiliko ya katiba kwa kuivunja kinyemela na kuifunga Tovuti yake ili wananchi wasiyasome maoni ya tume kwa kina. (walikuwa na jambo wanalificha hapa)", MTK, acha uongo,mimi naipenda nchi yangu, siko tayari kwa udanganyifu unaoufanya bila kuwa na uthibitisho wenye uhalali unaoweza kunishawishi kuhusu masuala hayo uliyoyaainisha. Ukweli ni kwamba Kuvunjwa kwa Tume kumefuata hatua zote na halali kisheria zaidi ya hapo kumetambuliwa hata kwenye Tangazo la Serikali Na.394 la mwaka 2011 Amri ya 2 aya (cc) Sheria Na. 9 ya mwaka 2013 kifungu cha 5. Baada ya kuwasilishwa kwa Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum chini ya kifungu cha 20(3), Rais, kwa amri iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serikali, ataivunja Tume. (2) Kuvunjwa kwa Tume kwa amri ya Rais kutakuwa na maana ya ukomo wa mamlaka ya Tume na Sekretarieti. Jamani wanaJF, watu hawa ambao wanatoa maneno yasiyo na msingi mimi huwa wananikwaza kwa kuwa siyo wakweli bali wanawahadaa Watanzania na wasomaji wa JF. Ndg wachangiaji na wasomaji wa jukwaa hili sitachoka kusema ukweli palipo na ukweli. Sasa basi nchi yetu inaheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu, tusikubali wapotoshaji wachache wachafue nchi hii kwa maslahi yao binafsi
Tukumbuke kuijenga, kuikuza na kuendeleza amani, umoja, ujirani mwema na ushirikiano na mataifa mbalimbali ya Afrika na dunia kwa ujumla; urithi tulioachiwa na Waasisi wa Taifa letu wa kujenga nchi yenye umoja wa watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila, dini, rangi, jinsi, ulemavu au ubaguzi wa aina nyingine yoyote. MUNGU IBARIKI TANZANIA
Hata wewe umekaririshwa tu kama mleta mada mtangulizi! sioni input yako binafsi isipokuwa kunukuu yale uliyokaririshwa! Archaic metality; na bado umegusia baadhi tu ya niliyoyasema; mbona huzungumzii kufungwa kwa tovuti ya tume?! kwa nini huzungumzii katiba kuukana utanganyika wetu?!
Ukweli unaojinasibu nao is a relative term kutegemea maono yako; maslahi is a relative term kutegemea unataka kutetea nini!
Bro read between the lines; think out of the box, usisome katiba au sheria kama unapiga picha.
kumbuka
Una macho lakini huoni! una masikio lakini husikii! una akili! unazibaniabania; hutaki kuziacha zivinjari! hilo swala la katiba pendekezwa ya "nyoka wa makengeza na Six" mpaka limefikia mahali linatolewa matamko makali makali na viongozi wa kiroho na makundi mbali mbali katika jamii; nchi imegawanyika nusura Amani ivunjike kisa hiyo katiba; Rais anatoa msimamo wake kuhusu katiba bado maaskofu wanamjia juu na kusisitizia tamko lao bado wewe unaimba prose; Ngonjera eti wewe ni mkweli mkweli! mkweli kuliko nani na kuhusu nini?! wacha wewe! usijipigie tarumbeta kaka waache watu wakusifie; Do not blow your own trumpet; let others sing praises for you!
Nchi iko njia panda kutokana na katiba hii; juzi serikali imeuweka mswada wa mahakama ya kadhi kwapani; bado tu wewe hjuoni kama kuna tatizo! unachekesha kweli!
KATIBA YA NYOKA WA MAKENGEZA NA SIX kura ni HAPAAAANA; and believe you me; we are a big movement; (VUGUVUGU LA NGUVU) na tuko kazini kuipata kura ya HAPANA. Anza kujiandaa kisaikolojia tafadhali!