Watanzani baadhi wamekuwa wavivu wa kusoma na hili ni janga ktk taifa letu, maaana kusoma hawataki lkn wanaamini tu kwa yale wanayoambiwa na watu wa pembeni jambo ambalo si zuri hususani katka suala hili muhimu la katiba, mtu kama hukuisoma vema katiba hii basi isiwe kero humu kukaidi na kujigamba kuwa wewe utapiga hapana, kuwa na busara tafuta muda isome vema na utagundua kuwa asilimia ya watu wengi wanaoipinga na kuikejeli hawajaisoma na ndo walioko mstari wa mbele ktika kuipinga, je watu hawa tuwaite Wazalendo au Wasaliti?
Tukumbuke ya kuwa Katiba Inayopendekezwa imewajali watu wote pasipo upendeleo wowote na hilo halina ubishi, hata wewe unayekaidi na kuipinga jua ya kwamba imekujali uwe mtoto, kijana, mzee n.k ujue kuwa haki zako zimo mule ndani, sasa kama kila kilichokizuri kimo iweje sasa uipinge tena kwa kusikiliza maneno ya watu? Huko ni kukosa uzalendo kwa nchi yako ukiwa kama Mtanzania.
Wito wangu kwako ewe mtanzania ni kwamba tuweni wazalendo, tuijenge nchi yetu kwa kuhakikisha kuwa katiba hii inapita kwa kura nyingi za Ndiyo hapo muda utakapowadia, maendeleo ya nchi hii huletwa na mimi pamoja na wewe na sio kwa kubisha bisha na kupotosha wengine kuichukia hii katiba, haitakuwa na maana kuendelea kuitumia hii ya 1977 kwani tumeshaona kuwa ina mapungufu kibao.
Kwa mfano mzuri, Katiba Inayopendekezwa imewajali Wasanii kwa mara ya kwanza katika ibara ile ya 59, pia tumeona kuwa PCCB kwa mara ya kwanza imewekwa katika ibara ya 249 pamoja na mambo mengine mengi ambayo kwenye hii ya 1977 hayakuwepo.
Nahitimisha kwa kusisitiza watanzania wote kuisoma katiba hii kwa makini na mwisho wa siku tuipigie kura nyingi za NDIYOOOOOO!
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, Long live KATIBA INAYOPENDEKEZWA.