Katiba Mpya: Dk. Slaa awasilisha maboksi 17 - Yanahusu maoni ya Katiba, Warioba agoma

Katiba Mpya: Dk. Slaa awasilisha maboksi 17 - Yanahusu maoni ya Katiba, Warioba agoma

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165

Dk. Slaa awasilisha maboksi 17
• Yanahusu maoni ya Katiba, Warioba agoma

na Abdallah Khamis
Tanzania Daima

TUME ya kukusanya maoni ya Katiba mpya inayoongozwa na Jaji mstaafu, Joseph Warioba, jana imegoma kupokea maboksi 17 ya maoni yaliyokusanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na badala yake ikapokea vitabu viwili vya randama kwa ajili ya maoni hayo.

Kutokana na tume hiyo kukataa kupokea ushahidi wa kile kilichoandikwa katika randama mbili zilizowasilishwa na CHADEMA, chama hicho kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, kimesema mpango huo unaashiria dhamira ya tume hiyo kuvibeba vyama ambavyo havina ushahidi wa ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wananchi.

Maoni hayo ya wananchi kuhusu rasimu ya Katiba, yamekusanywa kupitia mikutano mbali mbali iliyofanywa na CHADEMA yalifikishwa katika ofisi za tume jana majira ya saa 5:56 asubuhi yakiwa katika gari aina ya Range Rover yenye namba T 162 CDA, ambapo ndani ya gari hilo alikuwamo Dk. Slaa, huku maofisa wengine wa CHADEMA wakiwa katika magari tofauti.

Mara baada ya kukabidhi maoni hayo ya wananchi, Dk. Slaa alisema amesikitishwa na hatua ya tume hiyo kushindwa kubaki na maoni yaliyokusanywa kupitia taasisi zinazoeleweka kwa kile alichoeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa tume hiyo kupokea maoni ya watu waliojifungia ndani na kusema maoni hayo yametoka kwa wananchi.

Alisema tume inaweza kuibua maswali kutoka kwa taasisi na wananchi namna inavyoweza kujiridhisha na maoni yanayofikishwa kwao kwa kile alichoeleza kushindwa kupokea maoni ya awali kutoka kwa wananchi.

Aidha, Dk. Slaa alisikitishwa na utaratibu wa tume hiyo kushindwa kuwa na mpango maalumu wa kupokea maoni na kuweka kumbukumbu ya upokeaji huo.

"Sijui kama hawa watu walijipanga juu ya upokeaji wa maoni, angalia sisi kama tusingelazimisha watugongee muhuri kwa ajili ya uthibitisho wa upokeaji tungeondoka hivi hivi, sasa hali hii wamefanyiwa watu wangapi ambao hawana kitabu cha kusaini?" alihoji Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa katika randama walizowasilisha kwa tume, wameweka hoja 66 baada ya kujiridhisha na hoja nyingine zilizoko katika rasimu ya Katiba yenye hoja 240.
Alisema hoja ambazo hazijaguswa katika randama waliyowasilisha ni zile ambazo zinakubaliwa na CHADEMA pamoja na wananchi waliotoa maoni kupitia mikutano ya CHADEMA.

Namna walivyopata maoni
Kuhusu idadi ya watu waliotoa maoni yaliyowasilishwa jana, Dk. Slaa alisema hadi juzi walipokuwa wakifunga randama, kulikuwa na watu zaidi ya milioni 3.4 waliotoa maoni kwa njia mbalimbali.

Alitaja njia hizo kuwa ni mabaraza ya wazi ambapo walikusanya maoni ya watu 3,200,889 kutoka katika majimbo 81 waliyoyafikia, katika mabaraza ya ndani walifika kata 586 na kukusanya maoni 11,7274.

Njia nyingine zilizotajwa na Dk. Slaa ni ngazi ya majimbo ambapo walifanya mikutano ya ndani katika majimbo 189 ya Tanzania Bara na kukusanya maoni 130,000, kwa njia ya barua pepe walipata watu 612 waliotoa maoni huku kukiwa na ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa watu 12,345 pamoja na mitandao ya kijamii na kufanya jumla ya watu waliotoa maoni kuwa 3,462,805.

Dk. Slaa alisema ushahidi wa maoni hayo upo wazi kwao na kuwataka tume ijiridhishe kwa vyama vingine vinavyosema wameshakusanya maoni ya watu zaidi ya milioni mbili.

"Sisi tumefanya haya na wenzetu walete ushahidi kama huu badala ya kukaa vyumbani na kuwatengenezea Watanzania maoni na vitu vya kuingizwa katika Katiba. Hapa tunaililia Tanzania tuitakayo na si kwa masilahi ya chama chochote," alisema Dk. Slaa.


Aliongeza kuwa mazingira na matamko yanayotolewa na Chama Cha Mapinduzi kuwa wamekusanya maoni ya wananchi wengi na hayawezi kufikiwa na vyama vingine yana nia mbaya kwa nchi na hayaleti taswira nzuri kwa tume.

Usiri wa Tume kwa waandishi
Dk. Slaa pia alisema licha ya tume kuweka suala la uwazi kuwa ni moja ya tunu za taifa, bado imeshindwa kudhihirisha uwazi huo kwa kuwazuia waandishi wa habari kuingia na kushuhudia makabidhiano yanayofanywa katika ofisi za tume.

Alisema suala la Katiba ni la Watanzania wote na vyombo vya habari ni mhimili mkubwa wa serikali usio rasmi wenye kutegemewa kwa kiasi kikubwa na wananchi kutoa taarifa sahihi, lakini vinapozuiwa kushuhudia matukio hayo kwa uwazi ni kuwanyima fursa Watanzania kupata habari sahihi.

Aliongeza kuwa kama tume ya Katiba inafanya usiri katika kupokea maoni ya wananchi, wanaweza vipi kuwaridhisha Watanzania kuwa maoni waliyotoa ndiyo yaliyofanyiwa kazi.

Kuhusu Kingunge
Akizungumzia kauli ya Kingunge Ngombale- Mwiru, aliyoitoa juzi kuhusu umuhimu wa serikali mbili, Dk. Slaa alisema Watanzania wanapaswa kumsamehe mzee Kingunge kwa kuwa sasa amechoka.
Alisema katika vitu alivyopaswa kuvifanya Kingunge katika muda wake wa utumishi serikalini ni pamoja na kusimamia kero mbali mbali zinazolalamikiwa leo, hivyo kuendelea kuwaambia wananchi wasifikirie juu ya muundo wa Muuungano ni kuwakosea heshima.

"Mimi ninamsamehe mzee wangu huyu ila atambue muungano ulio bora ni ule unaoridhiwa kwa hiari na si kulazimisha mfumo unaoonekana una matatizo," alisema Dk. Slaa.


 
Kweli chadema ni chama cha wananchi! Warioba ameanza kupata woga kutoka kwa maccm wenzake, kukataa kupokea mabox hayo lengo ni kukibeba chama cha ccm kilichojifungia chumbani na kupika data za watoa maoni!
 
Kwa mjibu wa gazeti la majira yale maoni ya dr slaa aliyowasilisha tume ya katiba yamekutana na kigingi na hivyo kurudi nayo.
Inasemekana ni yale maoni ya helicopter.
 
Tume ya Katiba ina watu makini. Haiwezi kukubali maoni yasiyo na kichwa wala miguu.
 
hivi dr slaa bado yuko hai,maana kafulia kisiasa na akili.
 
maoni gani haya ambayo unamshawishi mtu atoae maoni kulingana na msimamo wa chama, tunavyojua chadema kilikuwa kinafanya mikutano ambayo ilikuwa ikieleza moja kwa moja maoni ya chama km vile serikali tatu, kuwa majimbo kitu ambacho kililenga wananchi kutokua huru kwenye kutoa maoni kwani kabla ya kutoa maoni yake yeye mwenyewe, Na huu ndiyo ULIKUWA uchakachuaji mkubwa wa maoni uliofanywa na cdm. NA HAYA SI MAONI YA WANAnCHI BALI NI YA CHAMA,
 
Watanzania msihofu,2016 tutatengeneza katiba ya Watz na si ya ccm
 
safi sana dr.wetu wa ukweli umetimiza wajibu wako.japo tumeona mizengwe mapema ya warioba na wenzake.
 
WanaJF!

Dr Slaa amepata PIGO la mwaka baada ya tume ya katiba inayoongozwa na jaji mstaafu Joseph Warioba kukataa kupokea maboksi yapatayo 17 yanayo daiwa kuwa na maoni yaliyo kusanywa na CHADEMA kutoka kwa wananchi, badala yake tume hiyo imepokea vitabu viwili tu vya randama kwa ajili ya maoni hayo.

Dr Slaa pamoja na jitihada zake zote za kufanya mikutano ya kwenye majukwaa na kupaa na "chopa" ameambulia patupu, kwa kuwa Dr Slaa pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA walikuwa wakifanya marudio ya ile kazi ambayo tume ya jaji Warioba ya ukusanyaji wa maoni mpaka kufikia hatua ya kuandaa rasimu ya katiba mpya. Sasa iweje leo tume ipokee maboksi 17?

Aidha, Dr Slaa pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA wanafahamu fika namna ambavyo mabaraza ya kikatiba yanavyopaswa kuendesha shughuli zake za ukusanyaji wa maoni, lakini kwa kuwa CHADEMA imezoea UKAIDI, ikaamua kufanya shughuli hiyo ya ukusanyaji maoni kwa taratibu zake yenyewe, matokeo yake ndio haya ya kukataliwa kupokelewa kwa maboksi 17 ya maoni, ingawa yalibebwa kwenye "Range Rover Sport"ambayo ndani yake alikuwamo Dr Slaa.

Dr Slaa, JIFUNZE KUFATA TARATIBU.
 
Hii kitu wataitoa tu,mi niliweka hapa saa kumi na mbili,wakaifuta kwa speed ya kinyamkela.
 
Kwisha habari yake,dr.slaa mhuni alikusanya vijana ndio waandike maoni hotelini.
 
Umepata wapi hizi habari?

mkuu chadema hamjitambui kabisa kabisa.,yaani hovyo kwelikweli.Ona saaa baada ya habari kuijadili unauliza imetoka wapi.Lakini isingekuwa inauliza kuhusu chadema ungefyata mkia.
 
Mleta mada inawezekana sio mtu wa kawaida. Yaan hujayaona yote yanayolikabili taifa letu kama madawa ya kulevya na ujambaz uliokidhiri bali wewe umeona la maoni kukataliuwa kweli? Vitu vingine jaman!
 
Kwisha habari yake,dr.slaa mhuni alikusanya vijana ndio waandike maoni hotelini.

ONYO kali kwa CHADEMA lilitolewa ikiwa kama ni kuwa tahadhari, lakini wakakaidi, leo Dr Slaa ana lalamika kuwa tume inapendelea vyama vingine na kuionea CHADEMA. Hivi Dr Slaa alisoma wapi?
 
Back
Top Bottom