Katiba Mpya: Dk. Slaa awasilisha maboksi 17 - Yanahusu maoni ya Katiba, Warioba agoma

Katiba Mpya: Dk. Slaa awasilisha maboksi 17 - Yanahusu maoni ya Katiba, Warioba agoma

Wakuu,jana tume ya mabadiliko ya katiba nchini iliyakataa mabox ya maoni ya chadema yaliyopelekwa na roli kama dr slaa alivyobainisha.

Slaa hapo awali aliuleza uma kuwa watapeleka maoni yao kwa roli kwa kuwa ni mengi sana ambapo jana walitimiza adhiba yao ya kupeleka mabox hayo ambayo yalikuwa rundo la mabox walifanya jana ambapo jaji walioba aliwaweka wazi kuwa yeye anataka maoni siyo mabox wala rundo la makaratasi.

chadema hawakupaswa kupeleka mabox bali walipaswa kuchambua na kuandika andiko ambalo linajumuisha maoni yote yaliyokwenye makaratasi kuliko kupeleka makaratasi yote sijui walitaka warioba ndiye akachambue au nani?
 
Wakati mwingine unashindwa kufahamu uelewa wa hawa viongozi wa Chadema.

Mabox ya maoni Dr.Slaa, kayatoa wapi wakati kazi kubwa aliyokuwa akiifanya ni kuzunguka na Chopa akifika sehemu Dr. Slaa yeye ndiyo alikuwa anawahutubia wananchi.

Hayo ni maoni yake binafsi pamoja na wenzake kina Mnyika, na Mbowe.

Kuna utaratibu wa kukusanya maoni kwa hiyo hayo maoni alikuwa anayabeba vipi na Chopa.
 
Yale si maoni, yaani unamshawishi mtu kitu fulan alafu aunamwambia, sisi tunataka iwe hivi, alafu unasema maoni ya wananchi, huo ndio uchakachuaji mkubwa
 
Mhariri wa gaziti la Majira ni mzalendo tena ni mtu makini mwenye kuitakia mema nchi yake.

Kimsingi maoni ya Chadema ni maoni ya Dr. Slaa hata ukiangalia huo ukusanyaji utamuona Dr.Slaa akiwahutubia wananchi.

Tafsiri ya uzalendo mpaka uisifie Chadema.
 
thread imedoda:thumbdown::thumbdown::thumbdown:
 
Kagame sijui jeuri ya kuishi maisha ya vita aliitoa wapi ni mjinga sana hapaswi kuhurumiwa.
 
Nimesikitishwa na kushangazwa na kichwa cha habari cha gazeti la Majira la leo jumapili tarehe 01/09/2013 kinachosomeka "Chadema yakwama".Hii habari inahusu uamuzi wa tume ya kukusanya maoni ya katba kukataa mapendekezo ya CHADEMA ambayo kimsingi ni maoni ya wananchi na si maoni ya CHADEMA kama chama cha siasa.

Mimi naomba kumuuliza mhariri atuambie katika uamuzi huo wa tume ni CHADEMA au ni Demokrasia ndio imekwama?Katika hali akili ya kawaida tu(commonsense) ukweli hapa waliokwamishwa ni wananchi waliotoa maoni yao na si CHADEMA.Kwa maneno mengine wananchi waliotoa maoni yao "wamepuuzwa" na si CHADEMA.Pia ikumbukwe kuwa idadi ya wananchi waliotoa maoni hayo yaliyokuwa kwenye maboksi 17 ni takribani watu milioni 3.5.K

Kwa kuzingatia ukweli huu, ndio napohoji uwezo na uzalendo wa huyu mhariri.Lakini pia inawezekana ndio ule mwendelezo wa waandishi wa habari kutumika kisiasa kwa malengo ya wanasiasa na vyama vyao.Haiingii akilini kwa mwandishi mzalendo kuandika habari ile "kishabiki" kiasi kile!

Waandishi wa habari mtende haki na mjue mna mchango mkubwa katika maendeleo na ustawi wa hii nchi katika kila nyanja iwe siasa,uchumi,elimu,jamii n.k.

Mkuu ijumaa kunamwandishi mmoja wa gazeti la majira aliandika makala moja kuhusu CDM kujenga mnara wa kumuenzi Mwangosi na tamko la jumuiya mojawapo ya wanahabari ....alionesha kuishambulia CDM nilipata hasira nikawasiliana moja kwa moja na yule mwandishi nikajenga hoja zangu juu ya taswira ya gazeti lao la majira na jinsi linavyoshiriki siasa chafu za Ccm alionesha kama kunielewa vile japo alisema alichokiandika ni mtazamo wake na maoni yake. Mwihso nilimwambia fanyeni vyovyote na chafueni vyovyote ila mwisho wa siku wananchi ukweli tunaujua na sisi ndio wapiga kura. Ipo siku CDM itakuwa madarakani nataka kuja kuona unafiki wa magazeti kama mjira utaishia wapi na haitoshi kuwalalamikia hapa jf wakati mwingine watwangieni simu kueleza hisia zetu kama mimi ninavyofanyaga nikikerwa na kutumika kwao
 
Mwisho wa maoni ni kura zitakazopigwa na Watanzania wote. Walichofanya CHADEMA kitajulikana wakati huo. Wamejirahisishia kazi kwa kiwango kikubwa!!
 
We jamaa ndio SIFURI kabisa kichwani, eti Dr Slaa amepata pigo. Pigo kapata Warioba na tume yake kwa kuonyesha kwamba kumbe maoni wanayokusanya hayatakiwi yatoke kwa wanachama wa CHADEMA na Viongozi wao. Hakukuwekwa limit ya maoni kiasi gani yanayotakiwa yakusanywe hivyo chama makini cha CHADEMAkwa kupitia viongozi wake kilitumia fursa ya kila kinapokutana na wanachama wake sehemu mbali mbali nchini na kwa njia nyingine za mawasiliano kukusanya maoni hayo na kisha kuyakabidhi kwa Tume. Warioba anaonekana wazi kabisa yupo ndani ya kamati kama mwanachama wa magamba na hivyo kujitahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha maoni ya wanaCHADEMA hayaingizwi kwenye katiba mpya.


Acha kukimbia mada, Dr Slaa amepata pigo, so do you!
 
Kingunge%20Still(1).jpg



Hebu acha uongo wewe!!!! Tangu lini mtu wa zaidi ya miaka 80 akawa ni age mate wa mwenye miaka 60!!!! Hata picha zinaonyesha jinsi Kingunge alivyokula chumvi nyingi ukilinganisha na Dr Slaa.

Yaani Slaa anamwambi age-mate wake kuwa amechoka!!!

Naona Slaa anajitahidi kupoliticize zoezi zima la Katiba Mpya. Katiba mpya isitumiwe kama political capital...
 
jadili mada mkuu huku kwingine unapoteza muda.Chadema mnafuja ruzuku ya chama kwa matumizi ya ya ovyoo

Pole sana kwa mawazo mgando...chadema hakitegemei ruzuku pekee kujiendesha...inapata support kubwa toka kwa wapenzi, mashabiki, wafadhili na wanachama.hutoa mchango miiingi kwa ajili ya jitihada za ukombozi magamba mnataka kuharibu mpaka katiba mpya.haya tunawaachieni katiba yenu muichakachue wenyewe
 
we kweli zuzu uzi umeletwa tena na mdaku mkuu wa jf hata haieleweki chanzo cha habari nichangie tu bila kuhoji? Hivi nyie mijitu ya ccm mpoje lakini?
Mijitu ya magamba inauzi mno...haijitambui...
 
Huyu babu kabadilishana akili na Mziwanda wake Juniour!
 
Hilo la mabox kukataliwa lilitarajiwa na CHADEMA.Nadhani watu hamjaelewa sawasawa.Kazi waliyofanya CHADEMA ya kutoa Elimu kwa wananchi ni KUBWA kuliko ama KUKUBALIWA au KUKATALIWA.Chadema imefanya kazi kazi yake ya siasa vizuri sana.Kwenye mikutano watu WAMEZALIWA upya.Ni kasi ya ajabu sana inayokwenda nayo Chadema.Walichofanya chadema ni KU-JUSIFY kazi waliyofanya na walioimbia serikali ya CCM kuwa wanakwenda kuifanya.Hivyo CCM wsmepigwa changa la macho!!!Tufuatilie mambo kwa makini!!!
 
Mhariri wa gaziti la Majira ni mzalendo tena ni mtu makini mwenye kuitakia mema nchi yake.

Kimsingi maoni ya Chadema ni maoni ya Dr. Slaa hata ukiangalia huo ukusanyaji utamuona Dr.Slaa akiwahutubia wananchi.

Tafsiri ya uzalendo mpaka uisifie Chadema.
Tena alikua akimaliza kuhutubia anapanda chopa huyoo ,mkutano unaishia hapo watu wanatawanyika,saa ngapi watu walikua wanapewa makaratasi na kuandika maoni?
 
Hilo la mabox kukataliwa lilitarajiwa na CHADEMA.Nadhani watu hamjaelewa sawasawa.Kazi waliyofanya CHADEMA ya kutoa Elimu kwa wananchi ni KUBWA kuliko ama KUKUBALIWA au KUKATALIWA.Chadema imefanya kazi kazi yake ya siasa vizuri sana.Kwenye mikutano watu WAMEZALIWA upya.Ni kasi ya ajabu sana inayokwenda nayo Chadema.Walichofanya chadema ni KU-JUSIFY kazi waliyofanya na walioimbia serikali ya CCM kuwa wanakwenda kuifanya.Hivyo CCM wsmepigwa changa la macho!!!Tufuatilie mambo kwa makini!!!

Katiba ni jambo la Muhimu sana. Nakubaliana nawe kwamba wananchi wamepata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu rasimu.
Naomba tuwekee ushabiki wa vya vyama kando kwa suala hili
 
Kwa mjibu wa gazeti la majira yale maoni ya dr slaa aliyowasilisha tume ya katiba yamekutana na kigingi na hivyo kurudi nayo.
Inasemekana ni yale maoni ya helicopter.

Bangi na madawa ya kulevya ni hatari kwa ubongo....
 
Bangi na madawa ya kulevya ni hatari kwa ubongo....
kweli kabisa mkuu,tena ikiwa ile iliyonyeshewa na mvua kisha ivutwe ukiwa ndani ya chopa,ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom