Katiba Mpya: Elimu ni kwa Wasioelewa - Ushuhuda

Katiba Mpya si kwa maslahi ya Chadema bali ya Watanzania wote kwani italinda UHURU na HAKI ya Watanzania kujadili mustakabali wa nchi, kuwakosoa walio madarakani bila woga wala vitisho kuchagua Viongozi tuwatakao bila mtutu wa bunduki kupora kura, vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi bila hofu ya kufungiwa au wanahabari kutekwa na kuuawa au kubambikiwa kesi.


 
Mimi siwezi kukulisha maneno.

Umesema:

Tatizo la #2 ni kama lako (ukimaanisha mimi).

Ukasema pia #2 wanahofi chadema kunufaika. Ukamalizia kwa kusema #2 wana chuki na chadema.
 
Si kweli kwamba mchakato ulishindwa kabla ya kuanza. Mchakato ulishindwa baada ya maccm kumtisha Kikwete kwamba kama ataunga mkono rasimu ile basi wataanika hadharani maovu yake kuanzia kampeni za 2005 ambapo alitumia pesa za mafisadi kutoa rushwa na kumchafua SAS.
Cha kushangaza Kikwete siku aliyokabidhiwa rasimu mpya baada ya kupewa aisome kwa wiki nzima aliwasifia sana wajumbe wa Tume kwa kazi nzuri sana na uzalendo wao lakini baada ya kutishwa na kutishika akawageuka wajumbe na kuanza KUWADHALILISHA.


 

UKAWA ilikua ni zao la kitu gani mkuu?
Composition ya wajumbe wa lile bunge ilijaa wanufaika wa iliyopo na waliangalia zaidi mchakato unawaachaje hasa hasa maslahi yao.
 
Soma nilichoandika kwa makini UKAWA haikuwa tayari kukumbatia uhuni wa maccm katika kuifumua rasimu ya Warioba watakavyo wao.

UKAWA ilikua ni zao la kitu gani mkuu?
 
Soma nilichoandika kwa makini UKAWA haikuwa tayari kukumbatia uhuni wa maccm katika kuifumua rasimu ya Warioba watakavyo wao.

Nimeongezea kidogo bandiko langu hapo juu.
 
Reactions: BAK
Sijabisha boss, nachokataa ni kuidai kwa kushinikiza ndani ya miezi mitatu ya madam. Hebu tumpe muda angalau 1 year...kisha tuanze kumdai tena kwa kumsuta, lakini mtu hata bajeti aliyoiandaa yeye ndio imeanza kutumika juzi leo tuanze kutishia kuingia road?
 
Reactions: BAK
Kushinikiza ni muhimu sana hasa ukitilia maanani kwamba sasa ni miaka 30 maccm bado wanatumia janja janja na uhuni ili kuikwamisha katiba hiyo. Unataka tuendelee kuomba kwa miaka mingine 50? Katiba mpya ni HAKI yetu Watanzania na si HISANI kutoka kwa yoyote yule ndani ya maccm au Serikali.

 

Kuna haja ya cool down. Nita address yako yote point kwa point hapa:

1. "Kunyamazia swali la kijinga ni ujinga, hapo umekosea."
----- rejea ukasome hapo ulipoandika. Honestly sijaelewa.

2. "Ule mchakato ulishindwa kabla ya kuanza. Nashangaa sana unataka kupima ubora wa rasimu kwa kiwango cha pesa iliyotumika."
----- Hakuna taarifa popote pale isipokuwa kwako leo kuwa mchakato ulishindwa kabla haujaanza. Kumbuka mchakato huo ulikuwa wa miaka kadhaa uliosheheni wakiwamo watu walioelimika labda kuliko mimi na wewe. Mchakato ushindwe vipi kabla ya kuanza, siyo kichekesho hiki?
------Ubora wa kitu pia hupimwa kwa thamani ya pesa. That's natural, and world wide. Pesa iliyotumika ni clear indication kuwa haukuwa upuuzi tu. Labda kama ni kwa ajili ya mabishano yasiyo na tija?

3. "Nikuulize swali, mambo gani makubwa mawili yapo kwenye ile rasimu unaona yataleta mapinduzi na kuondoa hii ukiukwaji wa katiba ya sasa kukoma kama ilivyo sasa?"

--- Jambo la kwanza ni kwenye Chaguzi. Uwepo wa tume huru, pamoja na kubadilika kwa upatikanaji wa wagombea, wakiwamo huru na wagombea binafsi, tutakuwa na viongozi tunaostahili kuwa nao kwa sera zao kamili, tutakaokuwa na uwezo wa kuwawajibisha kwa kushindwa kukidhi matarajio yetu kwa wakati. Hii italeta uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.

--- Uwepo wa serikali ya mseto. Hili litaweka uwajibikaji wa viongozi si kwa vyama bali kwa wananchi. Serikali itakuwa kweli ni ya uwajibikaji kwa mawazo ya wananchi. Longo longo zote za kubambikiziana kesi zitakuwa hazipo tena.
 

 
Mimi siwezi kukulisha maneno.

Umesema:

Tatizo la #2 ni kama lako (ukimaanisha mimi).

Ukasema pia #2 wanahofi chadema kunufaika. Ukamalizia kwa kusema #2 wana chuki na chadema.

Uliandika:
1. Huna tatizo na katiba mpya ila ukaonyesha una tatizo na Chadema.

Katika red ni ulichoandika wewe kuhusiana na tatizo lako na chadema:



2. Katika majibu yangu nikakutaarifu niliandika uzi wenye kuangazia pamoja na maudhui yako:

Kwenye green nikaonyesha hawa nao KAMA wewe wana tatizo na chadema.

Kwenye blue nikaendelea kuonyesha kuwa wao zaidi kuliko wewe, wao wana CHUKI pia.



Swali langu la msingi kwako. Ni wapi niliposema wewe una CHUKI na Chadema?

Ufafanuzi wako tafadhali.

NB: Tunapojadili mambo ya msingi kama hivi haipendezi kuwekeana maneno mdomoni.

Au nasema uongo ndugu zangu?

Cc: Extrovert , BAK Pascal Mayalla
 
1. Nilimaanisha ile kauli ya kujitetea kwamba ulikua unauliza swali kuwa nilikua under 18? Hapo ndio nikasema kubali kwamba ulikosea, kujificha kwenye kivuli cha swali la kijinga la aina ile ni ujinga pia.

2. Ikiwa mchakato ulihusisha wataalamu na wabobevu na kujumuisha watu wakini, ilikuaje ukakwama? Au ndio yale mambo ya kampuni ya Michael Peter kuwa bankruptcy mikononi mwa guru wa strategy?

3. Tume huru ya uchaguzi na serikali ya mseto ni mambo ya muhimu, lakini bado hayatoi hakikisho kwamba matatizo yetu makubwa yanayotukabili yatamalizwa. Pia tokea awali nimeshasema, kuwa na katiba bora ni jambo moja, kusimamia utekelezaji na usimamizi kwa katiba bora kwa ufanisi ni jambo lingine.

Ikiwa kipimo cha kitu ni pesa iliyopotea ni sawa na yale mashirika yanamwaga pesa nyingi kwenye miradi isiyokua na tija.

Utashi wa kisiasa ulipelekea tukaishia hapa tulipo, pesa zimepotea na katiba mpya hatuna.

Unawekaje wanufaikaji wakubwa wa mfumo mbovu uliopo wawe sehem ya kuufumua na kutupatia katiba mpya itakayoathiri maslahi yao binafsi?
 

..Tatizo ni kwamba Rais Samia Suluhu amevunja katiba na sheria kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani.

..Mbowe, Lissu, na wenzao, wamekemea suala hilo. Je, siyo sahihi kwa chama cha upinzani kumkemea Rais anapokiuka Katiba na Sheria?

..kama CCM hawataki Rais akemewe au arekebishwe na wapinzani, basi wafanye kazi hiyo wao wenyewe. Wamkemee Mwenyekiti wao kwa kukiuka sheria na katiba ya nchi.
 
Chief kama nilichoandika haujanielewa hakuna namna utanielewa.

Rudia tu nilichoandika.
 
Ni sahihi kusema Rais kavunja katiba ikiwa katiba yenyewe imetamka kwamba Rais ana mamlaka ya kutoa agizo au tamko lolote bila hata kuhojiwa na yeyote au chombo chochote?

Ni sahihi wao kukemea. Ila kama katiba imetoa hayo mamlaka je wapo sahihi kukemea kitu ambacho hakipo?

Ni sawa sana wazo lako.
 

..kunapotokea mkanganyiko kiuandishi kama huo inabidi tuangalie waandishi wa katiba walikuwa na maana au lengo gani.

..sidhani kama waandishi wa katiba walinuia kumpa rais mamlaka ya kuvunja katiba au kufanya matendo ya kijinai.

..hivyo basi chadema wako sahihi kumkemea, komkosoa, na kumsahihisha rais samia suluhu kwasababu amevunja sheria kwa kuzuia mikutano ya hadhara.
 

Ni jambo la kheri kuwa tunapiga hatua. Ningependa kujibu hoja zako zote lakini tusiache hoja yako #1 bila kuihitimisha.



Kwenye RED ulikuwa umeandika mambo ya msingi kabisa ya kufanyika kabla ya kuanza kuandika katiba mpya.

Kwenye BLUE nikahitimisha kwa kuonyesha kuwa unayotaka yalikwisha fanyika.

Vipi kupendekeza kufanyika tena yaliyokwishafanyika around 2012/13?

Si ajabu kuwa mtu hakuwa kwenye position ya kufahamu nini kilikuwa tayari kimeshafanyika.

Ndiyo maana kwa nia njema nikuuliza swali langu kwenye GREEN. Swali lile lilikuwa logical. Halikuwa la kijinga.

Ni vizuri hali ya kuaminiana ikawa imetamalaki tunapojadili mambo ya msingi kama watu wazima.

cc: BAK Extrovert
 
Kwakua hii ni katiba ya kijamaa na kwa kukumbuka namna Mwalimu Nyerere aliiexercise naamini hata kuzuia mikutano ni miongoni mwa kilicholengwa.

Nilitamani kuiita hii kitu 'clawback clause' ila naona it's stronger.
 
Mtu kama huyu nadhani inahitaji muda sana kumwelewesha maana inaonekana hana akili kabisa wala anachokiandika hakielewi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…