Nimeyataja hayo yanayotakiwa kufanyika sio kwa bahsti mbaya wala sio kwamba sifaham mchakato umekwamia hatua gani.
Na hii ndio dalili kwamba kuna mushkel kwenye mchakato, wewe unaona rasim iko sawa inahitaji kukamilishwa, mie naona hii iliyopo inahitaji marekebisho kujumuisha baadhi ya mambo nnayoona yameachwa na hayakupewa kipaumbele.
Lakini nikirudi kwenye mtazamo wangu kuhusu suala la katiba mpya, nimeendelea kusisitiza kwamba ikiwa ya sasa inakiukwa, kuna mzizi gani utakaohakikisha hiyo mpya haitasiginwa?
Kumbuka viongozi wetu kila wanapopata nafasi hua wanaapa kuilinda na kuieshimu lakini unaelewa yanayofuata baada ya hapo.
Tuliingizwa kwenye lile zoezi la kupata katiba mpya na watu waliokua na ajenda zao. Hapo ndio niliposema, mchakato ulikwama kabla haujaanza.
Mkuu umeeleza vizuri sana, nafikiri alichomaanisha Castr ni kama vile katiba inajichanganya, inasema mikutano ya kisiasa ni haki isipokua sheria isivunjwe. Hapo hapo inampa Rais nguvu kubwa na kuwa mwamuzi wa mwisho, ikaenda mbali zaidi kwa matendo aliyoyafanya akitekeleza majukumu yake kama mkuu wa nchi
Ile ya kuzuia mikutano ya kisiasa ilikua ni kutufumbua macho na kuonyesha jinsi ngani katiba inaweza kuchezewa na kisifanyike chochote.
Ila napingana na namna ambazo chadema wameamua kushughulika na swala husika.
Kwa miaka 6 wanasiasa walikua hawaongei kauli za kuashiria wanataka ugomvi na Lisu akiwa nje ya Tz alisema kuhusu kutaka kuhakikishiwa usalama arudi Tz.
As far as I know hakuhakikishiwa usalama, ila akaja, akafanya kampeni, akashiriki uchaguzi akataka kua detained akaescape.
Tumeanza na Madame President, immediately akaonyesha kujua Tz tulikua wapi na akaanza jitihada za kutibu, wakina Heri James wakaomba msamaha, waliokua wakiwakanyaga raia kwa miaka sita ghafla wakaside na raia.
Kwa ufupi ikawa inarudishwa Tz ambayo watu mnaweza kaa mezani na kujadili.
Kauli za Mbowe, Lisu na Nyagali haziashirii kama wanaona juhudi za Mama na kama ni sahihi wao kuruka stages zote na kuifikia stage ya kua jeuri na kusumbuana. These are the same people waliomuomba Magufuli wakae naye chini ili waruhusiwe kufanya mikutano. Anakuja anayeweza kuwasikiliza wanaopt kutunishiana misuli.
Ni maajabu kiukweli. Nilitarajia wawe more civil kuliko huu uamuzi.
Nimeyataja hayo yanayotakiwa kufanyika sio kwa bahsti mbaya wala sio kwamba sifaham mchakato umekwamia hatua gani.
Na hii ndio dalili kwamba kuna mushkel kwenye mchakato, wewe unaona rasim iko sawa inahitaji kukamilishwa, mie naona hii iliyopo inahitaji marekebisho kujumuisha baadhi ya mambo nnayoona yameachwa na hayakupewa kipaumbele.
Lakini nikirudi kwenye mtazamo wangu kuhusu suala la katiba mpya, nimeendelea kusisitiza kwamba ikiwa ya sasa inakiukwa, kuna mzizi gani utakaohakikisha hiyo mpya haitasiginwa?
Kumbuka viongozi wetu kila wanapopata nafasi hua wanaapa kuilinda na kuieshimu lakini unaelewa yanayofuata baada ya hapo.
Tuliingizwa kwenye lile zoezi la kupata katiba mpya na watu waliokua na ajenda zao. Hapo ndio niliposema, mchakato ulikwama kabla haujaanza.
La msingi zaidi ni kuwa tunasonga mbele bila jazba, kuitana majina, kuwekeana maneno mdomoni, wala kejeli.
1. Kupatikana kwa katiba si suala la siku moja wala mwezi wala mwaka 1.
2. Ni vizuri uchaguzi 2024/25 inshallah tukiwapo ufanyike kwa mujibu wa katiba mpya Ikiwezekana.
3. Kwenye mchakato wa kuiunda katiba mpya yote yatasikilizwa yakiwamo kuanzia from scratch. Panapo wengi hakuharibiki jambo.
4. Kuna tofauti ya kuanzisha mchakato wa kupatikana katiba mpya na katiba mpya yenyewe.
5. Tulipo ni kwenye hatua ya kuhitaji mchakato kuanzishwa. Ni hapo tu wala si zaidi.
Labda sasa nikuulize na wewe, hadi hapo pana tatizo gani kuwepo na makubaliano ya kuanzishwa kwa mchakato huo hata kwa kupeana tarehe tu?
Mkuu umeeleza vizuri sana, nafikiri alichomaanisha Castr ni kama vile katiba inajichanganya, inasema mikutano ya kisiasa ni haki isipokua sheria isivunjwe. Hapo hapo inampa Rais nguvu kubwa na kuwa mwamuzi wa mwisho, ikaenda mbali zaidi kwa matendo aliyoyafanya akitekeleza majukumu yake kama mkuu wa nchi
Ile ya kuzuia mikutano ya kisiasa ilikua ni kutufumbua macho na kuonyesha jinsi ngani katiba inaweza kuchezewa na kisifanyike chochote.
Najaribu kuiona hii kama clawback clause ila nashindwa kwa sababu hii inanyima hata upenyo tofauti na clawback clause ilivyozoeleka kwamba ni inakuwekea urasimu ambao utakuchelewesha kukamilisha unachotaka kwa wakati. Mfano kuandamana.
Katika uzi wowote ambao kiongozi wa nchi alitoa kauli tata au za kuudhi kuanzia Makonda, UVCCM, Kigwangala, Samia, Msukuma, Magufuli lazima utakuta nikilaani kauli husika.
Yaani msimamo unaouona hapa ndiyo ninao kwa yeyote yule. Hii ni kwakua mimi sina chama, na vitu vidogo kama katiba, uchaguzi na siasa nilivisoma kiasi chake.
So wewe ni keyboard warrior mmoja unayedhani ukiandika matusi itabadilisha ukweli kwamba hauna unachokijua.
La msingi zaidi ni kuwa tunasonga mbele bila jazba, kuitana majina, kuwekeana maneno mdomoni, wala kejeli.
1. Kupatikana kwa katiba si suala la siku moja wala mwezi wala mwaka 1.
2. Ni vizuri uchaguzi 2024/25 inshallah tukiwapo ufanyike kwa mujibu wa katiba mpya Ikiwezekana.
3. Kwenye mchakato wa kuiunda katiba mpya yote yatasikilizwa yakiwamo kuanzia from scratch. Panapo wengi hakuharibiki jambo.
4. Kuna tofauti ya kuanzisha mchakato wa kupatikana katiba mpya na katiba mpya yenyewe.
5. Tulipo ni kwenye hatua ya kuhitaji mchakato kuanzishwa. Ni hapo tu wala si zaidi.
Labda sasa nikuulize na wewe, hadi hapo pana tatizo gani kuwepo na makubaliano ya kuanzishwa kwa mchakato huo hata kwa kupeana tarehe tu?
Hapo mkuu sina neno, na huenda sikueleweka awali, shida yangu sio kwamba siitaki katiba mpya, la hasha.
Lakini nataka kuwe na utaratibu utakaoonyesha kweli kuna nia ya dhati ya kutupatia katiba mpya.
Kwa haraka haraka shida imejitokeza mara ya kwanza, awamu ya nne alitaka kuwafurahisha watu bila kuwa amejipanga, mchakato ukaishia njiani.
Awamu ya tano, iliwekwa wazi kabisa tokea awali kwamba katiba sio kipaumbele.
Awamu ya sita, watu wakasubiri kidogo ofisi izoeleke na kusikia kauli, ilipotoka ndio imezalisha hata huu mjadala tulionao sasa hivi.
Inaweza ikatajwa tarehe kwa pupa kwa lengo la kutuliza kelele na tukaishia kupoteza pesa na muda kama ilivyokua awamu ya nne.
Na wakiwa smart zaidi, inaweza ikapatikana lakini isiwe ile wananchi wanaitaka.
Katika uzi wowote ambao kiongozi wa nchi alitoa kauli tata au za kuudhi kuanzia Makonda, UVCCM, Kigwangala, Samia, Msukuma, Magufuli lazima utakuta nikilaani kauli husika.
Yaani msimamo unaouona hapa ndiyo ninao kwa yeyote yule. Hii ni kwakua mimi sina chama, na vitu vidogo kama katiba, uchaguzi na siasa nilivisoma kiasi chake.
So wewe ni keyboard warrior mmoja unayedhani ukiandika matusi itabadilisha ukweli kwamba hauna unachokijua.
Hapo mkuu sina neno, na huenda sikueleweka awali, shida yangu sio kwamba siitaki katiba mpya, la hasha.
Lakini nataka kuwe na utaratibu utakaoonyesha kweli kuna nia ya dhati ya kutupatia katiba mpya.
Kwa haraka haraka shida imejitokeza mara ya kwanza, awamu ya nne alitaka kuwafurahisha watu bila kuwa amejipanga, mchakato ukaishia njiani.
Awamu ya tano, iliwekwa wazi kabisa tokea awali kwamba katiba sio kipaumbele.
Awamu ya sita, watu wakasubiri kidogo ofisi izoeleke na kusikia kauli, ilipotoka ndio imezalisha hata huu mjadala tulionao sasa hivi.
Inaweza ikatajwa tarehe kwa pupa kwa lengo la kutuliza kelele na tukaishia kupoteza pesa na muda kama ilivyokua awamu ya nne.
Na wakiwa smart zaidi, inaweza ikapatikana lakini isiwe ile wananchi wanaitaka.
Uzi huo uliandikwa Jun 20 mapema sana kabla ya ramli la rais.
Tunakwenda vizuri na kimsingi nakubaliana nawe. Palikuwa na haja ya tarehe au mpango wa wazi wa kuanza mchakato huo ukajulikana. Kwa kusoma tu alama za nyakati niliandika uzi huu:
Katiba Iliyopo ina mapungufu mengi yasiyoweza kuvumilika zaidi. Ni wazi kuwa anayebeza jitihada zozote za kuanzishwa tena kwa mchakato wa kupata katiba mpya kiporo uliobakia, ni kwa sababu tu ya kuwa na uelewa mdogo au ni mnufaika wa moja kwa moja wa katiba mbovu hii iliyopo. Wanaobeza...
www.jamiiforums.com
Nilileta ushuhuda mwingine mapema tokea kwake Nigrastratatract katika uzi huu:
Mabibi na mabwana kumekuwa na vita vikali vya mitandaoni. CCM, Chadema, Corona, Legacy, tuzo za BET nk. Kwa hakika imekuwa ni patashika nguo kuchanika. Hata hivyo pana haja ya kufanyika tathmini za msingi. Kuna uwezekano mkubwa kuwa waungwana, letu sote ni moja. Yawezekana ni kwa sababu ya...
Kwanini hao unaotaka kuwabadili wasikushtukie kuwa nawe una maslahi yako binafsi? Siasa za Tanzania siku zote zinaamini katika zero sum game. Hakuna win-win.
Still on zero-sum game, ushindi kwa Chadema na "wanaharakati wa mtandaoni" utamaanisha kushindwa CCM na "wanaoiunga mkono" ikiwa ni pamoja na taasisi kama Idara ya Usalama wa Taifa. Kwa maana hiyo, the latter will always resist kwa sababu wanajua fika matokeo ya wao kukubali "kushindwa" huko. Kinachohitajika hapo ni consensus ambayo itapelekea matokeo kuwa win-win, kila upande unaona umeshinda.
Profesa Shivji, mbobezi kwenye Constitutional Law, anasema miongoni mwa katiba bora kabisa Afrika ni pamoja na ya Kenya na ya Afrika Kusini. Je katiba hizo zimeweza kutatua changamoto zinazozikabili nchi hizo? Jibu kaa nalo.
Uzi huo uliandikwa Jun 20 mapema sana kabla ya ramli la rais.
Tunakwenda vizuri na kimsingi nakubaliana nawe. Palikuwa na haja ya tarehe au mpango wa wazi wa kuanza mchakato huo ukajulikana. Kwa kusoma tu alama za nyakati niliandika uzi huu:
Mabibi na mabwana ni ukweli usiopingika kuwa kesho yetu iliyo bora zaidi inategemea sana uwepo wa katiba mpya. Kwa hali tuliyofikia kunahitajika zaidi mustakabala mpya wa utangamano. Ni wazi kuwa hayupo mmoja ambaye kwa dhati yake asiyekwazika kabisa kwa lolote na katiba iliyopo labda tu, kwa...
www.jamiiforums.com
Nikilenga kuonesha hili laja na ilikuwa vyema Mama akawahi. Hata sasa ninaamini hajachelewa. Japo tunaelekea kupwelewa.
Kwamba amechelewa au amewahi hilo nafikiri liko juu ya uwezo wetu. Nafikiri umeona alivyoanza kushughulikia suala la hii kitu inaitwa Covid-19. Na ntashangaa sana ikiwa ulikubali nchi ilikua na inao wataalam wabobevu ambao pia walihusika na kushiriki kwenye mchakato uluokwamia njiani wakabaki kimya bila kumshauri Mama nini cha kufanya, ntashangaa.
Kutaja tarehe ikiwa hakuna utayari au kuna vitu vinapingana kwa sasa haitatusaidia, itakua ni kuridhisha watu tu bila sababu na matokeo yake ni mabaya sana.
Kumbuka sio jambo jepesi tu la kutaja tarehe, pale tarehe inapotajwa ndio mchakato unapoanza. Sasa kama kuna vitu vinategemeana ili hilo kukamilika, unafikiri tarehe itatajwa tu hata kama hawana uhakika kama mpango na mambo mengine yanayohusiana yamekaa sawa?
Unaweza kutamka au kutangaza tarehe ya kufunga ndoa au kuanza vikao ikiwa bado mambo ya msingi kama mahari, utambulisho na tathmin ya uwezo na mahitaji ya gharama kukamilisha hilo jambo havijapatiwa majibu?
Kwanini hao unaotaka kuwabadili wasikushtukie kuwa nawe una maslahi yako binafsi? Siasa za Tanzania siku zote zinaamini katika zero sum game. Hakuna win-win.
Still on zero-sum game, ushindi kwa Chadema na "wanaharakati wa mtandaoni" utamaanisha kushindwa CCM na "wanaoiunga mkono" ikiwa ni pamoja na taasisi kama Idara ya Usalama wa Taifa. Kwa maana hiyo, the latter will always resist kwa sababu wanajua fika matokeo ya wao kukubali "kushindwa" huko. Kinachohitajika hapo ni consensus ambayo itapelekea matokeo kuwa win-win, kila upande unaona umeshinda.
Profesa Shivji, mbobezi kwenye Constitutional Law, anasema miongoni mwa katiba bora kabisa Afrika ni pamoja na ya Kenya na ya Afrika Kusini. Je katiba hizo zimeweza kutatua changamoto zinazozikabili nchi hizo? Jibu kaa nalo.
Nimelisoma bandiko lako vizuri na sasa nilijibu kifungu kwa kifungu kama ifuatavyo:
1. Niwe wazi kwenye suala la maslahi binafsi:
(a) Nimeorodhesha bayana baadhi ya dondoo kuonyesha kwa nini mtanzania yeyote (nikiwamo mimi) ana maslahi na dharura kwa mchakato huu wa katiba mpya kuanza.
(b) Nimeweka wazi pia kuwa, kueleweka bayana ya lini utaanza ilikuwa jambo la kheri. Yaani kupatikana angalau kwa tarehe au mwelekeo tu, kungetibu kabisa kiu yetu. Zaidi sana kama angalau chaguzi za 2024/25 inshallah, zingefanyika kwa mujibu wa katiba mpya lingekuwa jambo la kheri mno.
(d) Katiba ni yetu sisi wananchi. Hatutaki kubambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka sepatation of power ya mhimili, tunataka usawa, uwajibikaji, mawazo yetu kusikilizwa nk.
Vipi mtu asiyatake hayo? Labda tu haelewi au ni mnufaika wa katiba fyongo iliyopo.
(d) Sina hakika kwa nini mimi kuwa na maslahi kwenye upatikanaji wa katiba mpya iwe issue baina ya mimi binafsi na mtu yeyote. Ni wazi kuwa driving force kwenye kuhitaji mabadiliko ya katiba ni maslahi binafsi ya watu na ndiyo maana makundi yote huhusishwa kwa ajili ya maridhiano na muafaka.
2. Hakuna win-win situation:
Nadhani una maanisha kutokuwapo usawa wa watu ndani ya nchi. Yaani "live and let die' wala si "live and let live." Mwenye nguvu kumla mdogo.
Dondoo #4 in red kwenye orodha ya matatizo kwenye katiba iliyopo, inaakisi kutambulika kwa tatizo hilo:
Hili si sawa. Hii nchi ni yetu sote. Taasisi au mtu yeyote asiyetaka kutambua usawa wetu kamili, sote kama watanzania huyo si mwenzetu. Kwa hakika huyo Hatufai.
Hili ni moja katika mambo yanaelezea dharura iliyopo kwenye kuuanzisha na kuukamilisha mchakato huu.
3. Marumbano ya Chadema, wanaharakati mitandaoni, CCM nk.
Sisi hiyo haituhusu. Katiba tunayoitaka ni katiba ya wananchi ambapo makundi yote ya watanzania yatashirikishwa. Tunataka mustakabala mwema wa maisha yetu sisi, watoto wetu na watoto wa watoto wetu.
Sisi wananchi hatuwezi kukubali kushikwa mateka kwenye marumbano yoyote yasiyotuhusu. Hata hivyo sisi wananchi tutamwelewa yeyote anayepigania mchakato huu kurejelewa pamoja na sisi kuwa ni mwenzetu. Hali anayepinga kama ni uelewa tutaelimishana.
Inaeleweka kuwa pana watu wamejikita kumfarakanisha Mama na yeyote na kwa lolote hata kama ni la kijinga. Uzi huu hapa chini unahusika:
Kutofautiana kimawazo katika nchi ni jambo la afya. Haiwezekani sote tukawa na mtizamo mmoja. Hata watoto mapacha hutokea wakati wakatofautiana. Kwa bahati mbaya kuna zama zimepita kwa kutofautiana tu pana watu wamekufa, wamepotezwa, wamejeruhiwa, wamedhulumiwa, na mengi ya namna hiyo...
www.jamiiforums.com
Tunatambua pia kuwa wanaochochea mfarakano wa Mama na yeyote wamejikita zaidi kuwafarakanisha Mama na Chadema ambao wamekuwa mstari wa mbele kwenye kuhitaji kurejelewa kwa mchakato huu uliolala 2015. Bila shaka wahafidhina hao walio serikalini watahakikisha Mama hakutani kabisa na Chadema:
Mama Samia wewe ni jemedari wetu mkuu. Mwenye shaka na uwezo wako kuliongoza taifa hili atakuwa hajitambui tu. Hata hivyo nisiache kunukuu tokea katika msahafu wa kikristo pasemapo "si kila aitae bwana bwana atauona ufalme wa mbinguni." Sawia na hii si kila wakuitao Mama Mama wana mapenzi mema...
www.jamiiforums.com
Ni kweli kuwa inahitajika busara kubwa kufikia maridhiano na hasa baina ya Samia na Chadema. Hapo itategemea zaidi busara yake kubwa huku akiwa amezungukwa na mahafidhina wasiokuwa na haja na maslahi yoyote ya wananchi, bali yao binafsi na ya CCM.
4. Inafahamika wazi kwa nadharia na kiuhalisia kuwa Kenya na SA wana katiba bora zaidi Afrika. Hii haimhitaji gwiji wa sheria Prof. Shivji kutamka hilo kwa mtu mwingine kuweza kulitambua.
Kenya leo, Uhuru kazimwa kuhusu BBI. Uhuru kama rais amewahi kutenguliwa na mahakama. Kenya mihimili iko huru kwa maana yake halisi.
SA, Zuma leo yuko gerezani kwa makosa ya kuidharau mahakama tu. Mfano zaidi wa nini kuonyesha usawa wa raia wote mbele ya sheria SA?
Inajulikana wazi kuwa CCM hawana incentive yoyote ya kuridhia uwepo wa katiba mpya. Wana vingi vya kupoteza katika katiba mpya bila ya vya kupata. Hawawezi kuridhia kirahisi bila ya kuwepo msukumo haswa tena wa kutosha.
Tanzania ya leo si ya jana. Tulichezewa sana. Awamu ile imetufunza kujipanga vizuri ili kutokurejea tena Misri. Tuko wengi na hatufungamani na vyama, lakini kila aliye upande wetu tutamsikiliza na kiungwana. Anaye kidhi vigezo vyetu atakuwa mshirika wetu.
Tunajua kuna lugha ambazo CCM huzielewa zaidi. Kwa lugha hizo tutasema naye. Tutaelewana tu.
Tuna tambua safari hii ni ndefu na ngumu, lakini pia tunajua inawezekana (It is difficult but not impossible)!
UPUUZI MTUPU!!! Huoni tatizo HAKI na UHURU wa Watanzania kuchagua Viongozi tuwatakao badala ya chaguzi kuporwa kwa mtutu wa bunduki na wale wahuni wa Tume FAKE ya uchaguzi. Huoni tatizo HAKI na UHURU wa vyama vya upinzani kuminywa huku miaka mitano ikikatika bila ya kufanya mikutano ambayo ni HAKI yao ya kikatiba. Huoni tatizo kwa UHURU na HAKI ya vyombo vya habari kuwa huru kufanya kazi zao bila kuingiliwa na Serikali na hivyo kuwa na hofu ya kufungiwa na kutekwa, kupotezwa kubambikiwa kesi kama Kabendera au hata kuuawa. Kwa upumbavu wako kuangalia Kenya basi inatosha kuruhusu udhalimu na dhuluma za maccm kuendelea nchini. Wapumbavu kama wewe ni tatizo kubwa sana nchini ambalo linawavimbisha vichwa wahuni wa maccm kufanya wayafanyayo bila woga nchini.
Kwanini hao unaotaka kuwabadili wasikushtukie kuwa nawe una maslahi yako binafsi? Siasa za Tanzania siku zote zinaamini katika zero sum game. Hakuna win-win.
Still on zero-sum game, ushindi kwa Chadema na "wanaharakati wa mtandaoni" utamaanisha kushindwa CCM na "wanaoiunga mkono" ikiwa ni pamoja na taasisi kama Idara ya Usalama wa Taifa. Kwa maana hiyo, the latter will always resist kwa sababu wanajua fika matokeo ya wao kukubali "kushindwa" huko. Kinachohitajika hapo ni consensus ambayo itapelekea matokeo kuwa win-win, kila upande unaona umeshinda.
Profesa Shivji, mbobezi kwenye Constitutional Law, anasema miongoni mwa katiba bora kabisa Afrika ni pamoja na ya Kenya na ya Afrika Kusini. Je katiba hizo zimeweza kutatua changamoto zinazozikabili nchi hizo? Jibu kaa nalo.
Kwamba amechelewa au amewahi hilo nafikiri liko juu ya uwezo wetu. Nafikiri umeona alivyoanza kushughulikia suala la hii kitu inaitwa Covid-19. Na ntashangaa sana ikiwa ulikubali nchi ilikua na inao wataalam wabobevu ambao pia walihusika na kushiriki kwenye mchakato uluokwamia njiani wakabaki kimya bila kumshauri Mama nini cha kufanya, ntashangaa.
Kutaja tarehe ikiwa hakuna utayari au kuna vitu vinapingana kwa sasa haitatusaidia, itakua ni kuridhisha watu tu bila sababu na matokeo yake ni mabaya sana.
Kumbuka sio jambo jepesi tu la kutaja tarehe, pale tarehe inapotajwa ndio mchakato unapoanza. Sasa kama kuna vitu vinategemeana ili hilo kukamilika, unafikiri tarehe itatajwa tu hata kama hawana uhakika kama mpango na mambo mengine yanayohusiana yamekaa sawa?
Unaweza kutamka au kutangaza tarehe ya kufunga ndoa au kuanza vikao ikiwa bado mambo ya msingi kama mahari, utambulisho na tathmin ya uwezo na mahitaji ya gharama kukamilisha hilo jambo havijapatiwa majibu?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.