Kwanini hao unaotaka kuwabadili wasikushtukie kuwa nawe una maslahi yako binafsi? Siasa za Tanzania siku zote zinaamini katika zero sum game. Hakuna win-win.
Still on zero-sum game, ushindi kwa Chadema na "wanaharakati wa mtandaoni" utamaanisha kushindwa CCM na "wanaoiunga mkono" ikiwa ni pamoja na taasisi kama Idara ya Usalama wa Taifa. Kwa maana hiyo, the latter will always resist kwa sababu wanajua fika matokeo ya wao kukubali "kushindwa" huko. Kinachohitajika hapo ni consensus ambayo itapelekea matokeo kuwa win-win, kila upande unaona umeshinda.
Profesa Shivji, mbobezi kwenye Constitutional Law, anasema miongoni mwa katiba bora kabisa Afrika ni pamoja na ya Kenya na ya Afrika Kusini. Je katiba hizo zimeweza kutatua changamoto zinazozikabili nchi hizo? Jibu kaa nalo.
Nimelisoma bandiko lako vizuri na sasa nilijibu kifungu kwa kifungu kama ifuatavyo:
1. Niwe wazi kwenye suala la maslahi binafsi:
(a) Nimeorodhesha bayana baadhi ya dondoo kuonyesha kwa nini mtanzania yeyote (nikiwamo mimi) ana maslahi na dharura kwa mchakato huu wa katiba mpya kuanza.
(b) Nimeweka wazi pia kuwa, kueleweka bayana ya lini utaanza ilikuwa jambo la kheri. Yaani kupatikana angalau kwa tarehe au mwelekeo tu, kungetibu kabisa kiu yetu. Zaidi sana kama angalau chaguzi za 2024/25 inshallah, zingefanyika kwa mujibu wa katiba mpya lingekuwa jambo la kheri mno.
(d) Katiba ni yetu sisi wananchi. Hatutaki kubambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka sepatation of power ya mhimili, tunataka usawa, uwajibikaji, mawazo yetu kusikilizwa nk.
Vipi mtu asiyatake hayo? Labda tu haelewi au ni mnufaika wa katiba fyongo iliyopo.
(d) Sina hakika kwa nini mimi kuwa na maslahi kwenye upatikanaji wa katiba mpya iwe issue baina ya mimi binafsi na mtu yeyote. Ni wazi kuwa driving force kwenye kuhitaji mabadiliko ya katiba ni maslahi binafsi ya watu na ndiyo maana makundi yote huhusishwa kwa ajili ya maridhiano na muafaka.
2. Hakuna win-win situation:
Nadhani una maanisha kutokuwapo usawa wa watu ndani ya nchi. Yaani "live and let die' wala si "live and let live." Mwenye nguvu kumla mdogo.
Dondoo #4 in red kwenye orodha ya matatizo kwenye katiba iliyopo, inaakisi kutambulika kwa tatizo hilo:
Hili si sawa. Hii nchi ni yetu sote. Taasisi au mtu yeyote asiyetaka kutambua usawa wetu kamili, sote kama watanzania huyo si mwenzetu. Kwa hakika huyo Hatufai.
Hili ni moja katika mambo yanaelezea dharura iliyopo kwenye kuuanzisha na kuukamilisha mchakato huu.
3. Marumbano ya Chadema, wanaharakati mitandaoni, CCM nk.
Sisi hiyo haituhusu. Katiba tunayoitaka ni katiba ya wananchi ambapo makundi yote ya watanzania yatashirikishwa. Tunataka mustakabala mwema wa maisha yetu sisi, watoto wetu na watoto wa watoto wetu.
Sisi wananchi hatuwezi kukubali kushikwa mateka kwenye marumbano yoyote yasiyotuhusu. Hata hivyo sisi wananchi tutamwelewa yeyote anayepigania mchakato huu kurejelewa pamoja na sisi kuwa ni mwenzetu. Hali anayepinga kama ni uelewa tutaelimishana.
Inaeleweka kuwa pana watu wamejikita kumfarakanisha Mama na yeyote na kwa lolote hata kama ni la kijinga. Uzi huu hapa chini unahusika:
Kutofautiana kimawazo katika nchi ni jambo la afya. Haiwezekani sote tukawa na mtizamo mmoja. Hata watoto mapacha hutokea wakati wakatofautiana. Kwa bahati mbaya kuna zama zimepita kwa kutofautiana tu pana watu wamekufa, wamepotezwa, wamejeruhiwa, wamedhulumiwa, na mengi ya namna hiyo...
Tunatambua pia kuwa wanaochochea mfarakano wa Mama na yeyote wamejikita zaidi kuwafarakanisha Mama na Chadema ambao wamekuwa mstari wa mbele kwenye kuhitaji kurejelewa kwa mchakato huu uliolala 2015. Bila shaka wahafidhina hao walio serikalini watahakikisha Mama hakutani kabisa na Chadema:
Mama Samia wewe ni jemedari wetu mkuu. Mwenye shaka na uwezo wako kuliongoza taifa hili atakuwa hajitambui tu. Hata hivyo nisiache kunukuu tokea katika msahafu wa kikristo pasemapo "si kila aitae bwana bwana atauona ufalme wa mbinguni." Sawia na hii si kila wakuitao Mama Mama wana mapenzi mema...
Ni kweli kuwa inahitajika busara kubwa kufikia maridhiano na hasa baina ya Samia na Chadema. Hapo itategemea zaidi busara yake kubwa huku akiwa amezungukwa na mahafidhina wasiokuwa na haja na maslahi yoyote ya wananchi, bali yao binafsi na ya CCM.
4. Inafahamika wazi kwa nadharia na kiuhalisia kuwa Kenya na SA wana katiba bora zaidi Afrika. Hii haimhitaji gwiji wa sheria Prof. Shivji kutamka hilo kwa mtu mwingine kuweza kulitambua.
Kenya leo, Uhuru kazimwa kuhusu BBI. Uhuru kama rais amewahi kutenguliwa na mahakama. Kenya mihimili iko huru kwa maana yake halisi.
SA, Zuma leo yuko gerezani kwa makosa ya kuidharau mahakama tu. Mfano zaidi wa nini kuonyesha usawa wa raia wote mbele ya sheria SA?
Inajulikana wazi kuwa CCM hawana incentive yoyote ya kuridhia uwepo wa katiba mpya. Wana vingi vya kupoteza katika katiba mpya bila ya vya kupata. Hawawezi kuridhia kirahisi bila ya kuwepo msukumo haswa tena wa kutosha.
Tanzania ya leo si ya jana. Tulichezewa sana. Awamu ile imetufunza kujipanga vizuri ili kutokurejea tena Misri. Tuko wengi na hatufungamani na vyama, lakini kila aliye upande wetu tutamsikiliza na kiungwana. Anaye kidhi vigezo vyetu atakuwa mshirika wetu.
Tunajua kuna lugha ambazo CCM huzielewa zaidi. Kwa lugha hizo tutasema naye. Tutaelewana tu.
Tuna tambua safari hii ni ndefu na ngumu, lakini pia tunajua inawezekana (It is difficult but not impossible)!
Hiyo ndiyo habari yenyewe.
Cc:
BAK Extrovert Pascal Mayalla Wakudadavuwa johnthebaptist JokaKuu Salary Slip Erythrocyte The Boss Mshana Jr denooJ