Kama hujui siasa za bongo zinavyokwenda nibora ukafyata mkia. Leohii ukimwambia mtu wa pwani na kusini kwa ujumla kuhusu CDM atakujibu "hao ni makafili na siwapi kurayangu" alkadhalika kwa wakaskazini hamuwezi ungamkono harakati zozote zifanywazo na CUF.
Kwenye safari za Wafalme na wajakazi wao nao wapo. Yeye hagombei, anaokoa tu jahazi la CCM
Wenzangu wanabodi, hususan wale waliberali, turudini kwenye ile hoja nyingine, maana mntaka kutumia 'kombora' la uliberali kama exit ya zile tuhuma nyeti zinazowakabili CUF na hasa mwenyekiti wenu na mgombea urais wa maisha, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, kuwa;
1. Ni washirika wakubwa wa CCM kiasi mlijitoa mhanga, mkaligawanya taifa kwa misingi ya udini, ili CCM inusurike kuondoka madarakani iendelee kutawala.
2. Profesa Lipumba ni kati ya viongozi wa siasa wanaopaswa kuogopwa kama ukoma hapa nchini kutokana na kuwa na malengo ya kuwagawa Watanzania (wanaopendana kama ndugu) katika misingi ya imani za dini, hasa uislamu na ukristo. Inaonekana hata hatambui haki za watu wenye imani za dini zingine tofauti na hizo mbili na wapagani.
Ni mtu hatari sana huyu!
Lakini katika hali inayoonesha au kudhihirisha kumkoma nyani gidari...Tume ya Katiba Mpya, kupitia rasimu yake ya juzi, imepigilia msumari, hasa katika ibara ya 75(h)...
Ibara hiyo inayozungumzia sifa za mtu kuwa rais inasema;
Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya kushika madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, ikiwa;
(h) Sera ZAKE au sera za CHAMA CHAKE, si za mrengo wa kuligawa taifa kwa misingi ya ukabila, udini, rangi au jinsia.
Wandugu wangu, hapo kwenye herufi kubwa msisitizo ni wa kwangu. Lakini hapa CUF ambao siku za hivi karibuni wameskikika wakililia 'utamu' wa kuwa mojawapo ya vyama vya upinzani, wakati keki yao walishaila baada ya kuamua kuungana na CCM kisirisiri kwenye uchaguzi mkuu kama alivyotoboa Profesa Lipumba kwenye ule mkanda wake wa udini na wakaungana na CCM kwanza sirini, kisha hadharani huko Zanzibar, hawachomoki.
Hadi tunavyozungumza hapa, si CUF wala Profesa Lipumba waliotoa hoja za maana juu ya ule mkanda wa video unaomuonesha Prof mzima akifanya kazi ambayo hata mtoto wa chekechea, akisimuliwa atasema 'hakuna maana ya kwenda shule, kama elimu haijamsaidia hata huyu profesa...kuwagawa watu...kwa udini'.
Atashindwa nini kutugawa kwa ushia, sunni, ukabila, kisha maeneo!
Tunashukuru watu wa tume, katika eneo hili, hakuna Mtanzania mpenda nchi yake, atapingana nanyi hapo. Ingawa kunasikika minong'oni kuwa Profesa na watu wake watakataa, maana ndiyo uchochoro wanaotaka tena kuutumia kuibakisha CCM madarakani, maana wao kama wao, hawawezi kushinda. Wanajua.
Watanzania wote, bila kujali tofauti zetu zingine tuiunge mkono hii ibara hasa hicho kipengele.
Wote wataanguka anguko moja, maana wako pamoja.
mkia upi lakini.
Me, naona unapiga tantalila tu, ila unajua kua alicho kifanya Professor sio makosa na sio wakwanza kufanya hivyo kwa hawa wanasiasa wetu, sasa kama wewe ungekua mkereketwa wa hayo basi ungeanza na Edward Lowasa, kilasiku anashinda makanisani akifanya harambe. Harambe ambazo zinaambatana na kuomba uungwaji mkono ktk harakati zake za Urais, chaajabu nakuona unaenda lase na Professor na kuanza kumdhi, kwatarifa yako Professor kajaa nyoyoni mwetu sisi tulie kosa haki sawa, kwahiyo propaganda zenu haziwezi kumchafua.Kitoabu
Hoja iliyopo ni hawa jamaa au huyo jamaa kuwa hatari kwa kueneza udini, badala ya siasa. Tena kwa kuibeba CCM na mkuu wao anakiri kabisa kuwa wao na CCM ni damu damu. Maana yake hapo ni kwamba wako kinyume na Watanzania. Nani Mtanzania makini anataka chama mamluki kinachotumiwa na CCM kuendeleza mambo yale yale. Labda wewe! Watanzania makini wanataka upinzani makini ili CCM iondoke madarakani.
Vyama vyote vikifanya siasa safi vitapata mashabiki, wafuasi na wanachama kila mahali. Au unataka kuibua lingine tena la ukabila na ukanda, baada ya kuona hili la udini, limesanuka. Waislamu wajanja na makini wamelikataa.
Naona nawe unazo fikra kama za Profesa, vipi wamoja nini au ndiyo yale mambo ya "Wastara hazumbuki, wa mbili havai moja".
Jamani tunashukuru rasimu ya katiba katika kipengele hicho imetuokoa taifa zima...maana ule mkanda ni hatari
Mods mnaweza kutusaidia kuuweka tena hapa...hatari ile du!
hata akigombea ni nani atakayempa huo urais.
mkuu, hiyo katiba mpya ni mwiba kwa watu wengi sana hasa CUF na CHADEMA kwani vyote vina mwelekeo wa kidini. mbaya zaidi kwa chadema ni kuwa sera yao ya majimbo ambayo waliwadanganya watanzania kuwa ni kuharakisha maendeleo, imebainika kuwa itachochea uasi, itawagawa watu kwa misingi ya dini na ukabila. tume imekataa kata kata na kwa hali hiyo, chadema inabidi wajitathmini upya
hivi jf hatuwezi kuunda tume ya kuchunguza kwa nini prof. Lipumba hajaoa?
Me, naona unapiga tantalila tu, ila unajua kua alicho kifanya Professor sio makosa na sio wakwanza kufanya hivyo kwa hawa wanasiasa wetu, sasa kama wewe ungekua mkereketwa wa hayo basi ungeanza na Edward Lowasa, kilasiku anashinda makanisani akifanya harambe. Harambe ambazo zinaambatana na kuomba uungwaji mkono ktk harakati zake za Urais, chaajabu nakuona unaenda lase na Professor na kuanza kumdhi, kwatarifa yako Professor kajaa nyoyoni mwetu sisi tulie kosa haki sawa, kwahiyo propaganda zenu haziwezi kumchafua.
hata akigombea ni nani atakayempa huo urais.
mkuu, katiba mpya haitoi mwanya kwa watu kama akina slaa kugombea. Mtahangaika sana lakini hamtaweza
Vipi uwakala na umamluki wa CUF na Profesa kwa CCM, mtaacha lini. Tunamtaka mwenyewe aje hapa atuambie hiyo biashara yao itakwisha lini, maana inatesa taifa hili kuendelea kuibakiza CCM madarakani.
hata dr slaa, marando na wengine kibao ni mamluki wa ccm. ndo maana dr slaa hajakana kumiliki na kuilipia kadi ya ccm
kwamtoro,idrisa na kichangani kwenye maskani zake.
Na anapotolea matamko ya kugawa watz
Vipi hebu tudondoshee kaushahidi ka video mwanangu akikiri naye alimbeba Kikwete na CCM baada ya jahazi kuelekea kuzama kama tulivyomuona Lipumba akikiri na kama tulivyoona ndoa ya mkeka kule visiwani.
Hivi Lipumba aliposema jahazi lilikuwa linaelekea kuzama na CCM na Kikwete wangeshindwa si alikuwa anamaanisha kushindwa na Dkt. Slaa na CHADEMA!
Sasa mbona unapingana na profesa majalala anayetumika na CCM bhana, acha hizo bhana, usiende kinyume na mafunzo ya profesa, kutumika na CCM.