Pamoja na kuwa Mama Samia anaweza kuwa anayo nia njema na ya dhati kuhusiana na haki, uhuru na usawa wa watu, kizingiti kitaendelea kuwa wale wahafidhina wanaomzunguka.
CCM hao watakuwa ndiyo walio waasisi wa ile salamu yetu pendwa ya "Kazi Iendelee" na hata kile kidokezo chetu cha "JPM = Samia" kwa maana halisi.
Pamoja na jitihada zake binafsi alizokwisha onyesha yawezekana bado atakuwa kwenye mashinikizo makubwa kuuishi u mwendazake.
Lengo na madhumuni ya wahafidhina hao yumkini ni kuendeleza misimamo ya bwana JPM bila JPM kuwepo. Kikubwa zaidi kikiwa ni kuyalinda maslahi yao binafsi.
Mengine tunayoyaona yatakuwa ni janja ya nyani tu.
Yatambulike mambo ya msingi yaliyokuwa katika rasimu ya katiba ya Warioba:
Hii ni kama ambavyo mjumbe huyu ndugu mjumbe Domhome (heshima kwako sana mkuu) alivyoyaweka kwa ufasaha kabisa.
Kwa hali kama hiyo, ni CCM gani katika waliojimilikisha hii nchi na vyote vilivyomo watakaoridhia mchakato wenye rasimu yenye maudhui kama hayo kirahisi bila ya kuwapo na mpambano wa haja kweli kweli au wenye resistance ya kutosha?
Pana haja ya kupanua wigo wa washirika katika vita vitakatifu hivi vyenye vionjo vyote vya kuturejeshea yote tuliyokuwa tumepokwa na kujikuta tumekuwa:
Wabambikiziwa kesi, wahanga wa dhuluma, kubebeshwa mizigo ya kodi zisizotuhusu, Ku, kubagazwa nk.
Hayupo asiye pendwa usawa wala uwepo wa utawala ambapo mihimili yote itakuwa na uhuru kamili.
Asasi za dini, kiraia, wana harakati na hata vyama vingine vya siasa vitakavyokuwa tayari.
Uelekeo ni wazi, kulishiriki vuguvugu hili ni thwawabu.
Ninawasilisha!