Katiba mpya, Mbowe na Lissu ni wamoja? Wanazungumza lugha moja na kupaza sauti moja? Kwanini wanaonekana kama kila mtu na lake, kila mtu na lwake?

Kaka binafsi naona CDM wamewasoma vizuri sana CCM. Kinachofanyika hapo ni "negotiation tactics" wataalam wa hiyo kitu wanaelewa nasema nini. Ngoja nisiwaharibie CDM mkakati wao, maana ndiyo siasa hizo.
 
Lisu anapiga misumari ya mbavu, kama hupendi ukweli utaona “anazungumza kwa lugha ya machukizo”.
 
Wewe ni CCM sasa CHADEMA wana kuhusu nini?kama wakivurugana wewe si unatakiwa kufurahi acha unafiki kijiana mdogo wewe,Teuzi huwezi kupata huko CCM Acha kuendekeza njaaa
 
Kuna Watu wanachukizwa na juhudi ya Mbowe na Lissu na mbaya zaidi ni wafuasi wa chama Cha mboga mboga kutwa nzima kuleta nyuzi za CDM wanasahau hata kueneza sera ya Chama Chao

Lissu kamatia hapo hapo
 
Kwanza niumie Kwa kukili mayala pascal

Ni mwanasheria na ni wakili msomi

Lakwanza,nitolee mfano kwako hebu niambie wakati umepata ajali ukaumia hiyo mikono ,maumivu yake yakoje?

Lisu ,kapigwa lisasi kapona ,Leo yatengenezwe mabango Lisu na mama wamemalizana akati sikweli haya nimaumivu ya pili makubwa mno kwasababu yanahusu ufikirishi

Swala la Lisu na mbowe waache ,kwasababu mmoja Yuko kwenye maridhiano ,mmoja hajajibiwa kwamaandishi na ikulu mambo muhimu aliyohoji kuhusu maridhiano( Lisu)

Tumwache Lisu afanye KAZI yake ,msomi mzima mayala unazungumzia jukwaa badala ya ujumbe aliosema Lisu akiwa kwenye hilo jukwaa
 
Hivi Magufuli na Samia walikuwa wanaongea lugha moja? Mbona uliufyata
 
Kwa ninavyoona Lissu, Mnyika, Heche na wengine wanzungumza lugha moja, lugha inayopendwa na wanachadema.

Mbowe, Msigwa, Sugu na wengine wanzungumza lugha yao nyingine ambayo inaonekana kuwa ya 'walamba asali'

Sijui kama wamekubaliana au la, lakini hali sio shwari CDM. Hizi ziara za Lissu ni kama zinamlazimisha Mbowe akurupuke nayeye aanze kuzunguka huku na huko ili aonekane bado yupo.
 
Chadema hakuna mtu wa kuandamana.
Hapo ndipo unapokosea,

IPO nguvu ya asili inayoyaunganisha makundi mbalimbali ya wananchi kudai HAKI,

Umeona Wafanyabiashara wakiandamana, utawaona wafanyakazi, wamachinga, wasafirishaji, wakulima, wanamichezo, wote wanaamshwa kudai HAKI juu ya nchi mbali na wanasiasa.

Ikiwa Unadhani mambo yataendelea kuwa yalivyo,

Tusubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…