Katiba mpya, Mbowe na Lissu ni wamoja? Wanazungumza lugha moja na kupaza sauti moja? Kwanini wanaonekana kama kila mtu na lake, kila mtu na lwake?

Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, zenye swali la msingi, kisha majibu utayatoa wewe.

Swali la leo la bandiko hili ni kuhusu hoja ya kuipambania katiba mpya: Je, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe na Makamo Mwenyekiti wake, Mhe. Tundu Lissu ni Wamoja? Wanapambana pamoja, wanazungumza lugha moja na kupaza sauti moja? Je, ni mimi tu nawaona ni kama watu wawili tofauti, kila mtu na lake, na kila mtu na lwake?

Kwa kuanzia nijitambulishe ili kujenga uhalali wa kuzungumzia jambo lolote la CHADEMA.

CHADEMA, japo ni chama cha wanachama, ni chama cha umma, yaani it's a public party na sio a private party. Mimi ni Mwananchi wa kawaida wa Tanzania ambaye mlipa kodi ya kuendeshea nchi.

Hivyo kila Mtanzania yoyote, anayelipa kodi kwa serikali ya JMT, ana haki ya kutoa mawazo yake yoyote kuhusu uendeshaji wa serikali ya JMT na kuhoji jambo lolote linalihusu matumizi ya fedha zake ambazo ni kodi yake.

CHADEMA kinaendeshwa kwa fedha za ruzuku ya vyama vya siasa, hivyo sisi walipa kodi, tuna haki kuzungumza na kuzungumzia jambo lolote kuhusu CHADEMA kwasababu ni fedha zetu zinazoendesha CHADEMA.

Nazifuatilia ziara za uhamasishaji wa katiba mpya na uimarishaji wa chama, zinazofanywa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, na Makamo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, naziona kama hazina coordination na haziko coordinated, japo zote zina lengo moja la amsha amsha na uhamasishaji wa katiba mpya na kuimarisha chama, mimi naziona kama Mbowe na Lissu, hawazungumzi lugha moja.

Mbowe anazungumza as a mature politicia, anazungumza kama a statesman in waiting kuja kuwa kiongozi mkubwa wa nchi kwa kuzungumza kwa upole, kwa heshima na lugha ya kistaarabu wakati Lissu anazungumza kama mwanaharakati anayepigania katiba mpya huku akizumza kwa ukali, na lugha kali, na sometimes hata kwa lugha ya machukizo!

Mbowe anazungumza kama a compromised leader aliyeko kwenye meza ya mazungumzo ya maridhiano na kuna mambo tayari wameisha kubaliana na kuridhiana japo bado hawajafikia muafaka na kuyatangaza wazi, wakati Lissu anazungumza as if CHADEMA bado iko kwenye Mapambano na yeye ni yuko vitani, yuko msituni kwenye fighting ya mapambano ya kupambania katiba mpya.

Jee haya anayoyazumza Lissu, Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability? ametumwa na CHADEMA au ni yake? Kwa vile Mbowe anaonekana a compromised leader, kutokana na kuwa ni mtu wa shukrani kwa Mama kwa alomtendea, hivyo inambidi awe mpole tuu, hivyo ili Mbowe asionekane mbaya kwa Samia, haya mambo ambayo Lissu anazunguka kuyaongea, ni Mbowe amemtuma au amekubaliana nae. Kama ni hivyo, mbona mikutano ya Lissu haionekani kuwa na proper logistical support? Mfano ni huu, Lissu akiwa kwenye jukwaa la mabanzi (Kichanja) Huu kweli ni mkutano uliopangwa na Chadema kama chama au individual stand alone arrangements?.

Kama hayo Lissu anayozunguka kuyasema ni yake na hajatumwa na yeyote, then CHADEMA kina wajibu wa kumdhibiti, na wasipo mdhibiti now, huko mbele atakuja kuwagharimu very dearly!

Kwenye issue ya katiba mpya Rais Samia anaihandle vyema, ameunda kikosi kazi huku akifanya mazungumzo ya maridhiano na CHADEMA, kwa stage tuliofikia, ni nzuri na haihitaji mapambano na mapigano, sasa hizi lugha za kianaharakati za Lissu, anapambana na nani? Na Mama? na CCM au.

My Take
Ili Chadema ifanikiwe kwenye jambo lake lolote, viongozi wake wakuu, Chairman, VC na SG, lazima wazungumze pamoja, kwa lugha moja na sauti moja na sio kama hali ilivyo sasa kila mtu anazungumza lake, na kwa upande wa maandalizi ni kila mtu na lwake.

Viongozi wawili wakuu mnapo toa kauli zinazopishana pishana, mnawachanganya wafuasi wenu kujiuliza washike lipi?

Kwe haya Mapambano ya katiba mpya, jee Mbowe na Lissu ni pamoja?

Paskali.
Kaka binafsi naona CDM wamewasoma vizuri sana CCM. Kinachofanyika hapo ni "negotiation tactics" wataalam wa hiyo kitu wanaelewa nasema nini. Ngoja nisiwaharibie CDM mkakati wao, maana ndiyo siasa hizo.
 
Lisu anapiga misumari ya mbavu, kama hupendi ukweli utaona “anazungumza kwa lugha ya machukizo”.
 
Wewe ni CCM sasa CHADEMA wana kuhusu nini?kama wakivurugana wewe si unatakiwa kufurahi acha unafiki kijiana mdogo wewe,Teuzi huwezi kupata huko CCM Acha kuendekeza njaaa
 
Kuna Watu wanachukizwa na juhudi ya Mbowe na Lissu na mbaya zaidi ni wafuasi wa chama Cha mboga mboga kutwa nzima kuleta nyuzi za CDM wanasahau hata kueneza sera ya Chama Chao

Lissu kamatia hapo hapo
 
Kwanza niumie Kwa kukili mayala pascal

Ni mwanasheria na ni wakili msomi

Lakwanza,nitolee mfano kwako hebu niambie wakati umepata ajali ukaumia hiyo mikono ,maumivu yake yakoje?

Lisu ,kapigwa lisasi kapona ,Leo yatengenezwe mabango Lisu na mama wamemalizana akati sikweli haya nimaumivu ya pili makubwa mno kwasababu yanahusu ufikirishi

Swala la Lisu na mbowe waache ,kwasababu mmoja Yuko kwenye maridhiano ,mmoja hajajibiwa kwamaandishi na ikulu mambo muhimu aliyohoji kuhusu maridhiano( Lisu)

Tumwache Lisu afanye KAZI yake ,msomi mzima mayala unazungumzia jukwaa badala ya ujumbe aliosema Lisu akiwa kwenye hilo jukwaa
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, zenye swali la msingi, kisha majibu utayatoa wewe.

Swali la leo la bandiko hili ni kuhusu hoja ya kuipambania katiba mpya: Je, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe na Makamo Mwenyekiti wake, Mhe. Tundu Lissu ni Wamoja? Wanapambana pamoja, wanazungumza lugha moja na kupaza sauti moja? Je, ni mimi tu nawaona ni kama watu wawili tofauti, kila mtu na lake, na kila mtu na lwake?

Kwa kuanzia nijitambulishe ili kujenga uhalali wa kuzungumzia jambo lolote la CHADEMA.

CHADEMA, japo ni chama cha wanachama, ni chama cha umma, yaani it's a public party na sio a private party. Mimi ni Mwananchi wa kawaida wa Tanzania ambaye mlipa kodi ya kuendeshea nchi.

Hivyo kila Mtanzania yoyote, anayelipa kodi kwa serikali ya JMT, ana haki ya kutoa mawazo yake yoyote kuhusu uendeshaji wa serikali ya JMT na kuhoji jambo lolote linalihusu matumizi ya fedha zake ambazo ni kodi yake.

CHADEMA kinaendeshwa kwa fedha za ruzuku ya vyama vya siasa, hivyo sisi walipa kodi, tuna haki kuzungumza na kuzungumzia jambo lolote kuhusu CHADEMA kwasababu ni fedha zetu zinazoendesha CHADEMA.

Nazifuatilia ziara za uhamasishaji wa katiba mpya na uimarishaji wa chama, zinazofanywa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, na Makamo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, naziona kama hazina coordination na haziko coordinated, japo zote zina lengo moja la amsha amsha na uhamasishaji wa katiba mpya na kuimarisha chama, mimi naziona kama Mbowe na Lissu, hawazungumzi lugha moja.

Mbowe anazungumza as a mature politicia, anazungumza kama a statesman in waiting kuja kuwa kiongozi mkubwa wa nchi kwa kuzungumza kwa upole, kwa heshima na lugha ya kistaarabu wakati Lissu anazungumza kama mwanaharakati anayepigania katiba mpya huku akizumza kwa ukali, na lugha kali, na sometimes hata kwa lugha ya machukizo!

Mbowe anazungumza kama a compromised leader aliyeko kwenye meza ya mazungumzo ya maridhiano na kuna mambo tayari wameisha kubaliana na kuridhiana japo bado hawajafikia muafaka na kuyatangaza wazi, wakati Lissu anazungumza as if CHADEMA bado iko kwenye Mapambano na yeye ni yuko vitani, yuko msituni kwenye fighting ya mapambano ya kupambania katiba mpya.

Jee haya anayoyazumza Lissu, Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability? ametumwa na CHADEMA au ni yake? Kwa vile Mbowe anaonekana a compromised leader, kutokana na kuwa ni mtu wa shukrani kwa Mama kwa alomtendea, hivyo inambidi awe mpole tuu, hivyo ili Mbowe asionekane mbaya kwa Samia, haya mambo ambayo Lissu anazunguka kuyaongea, ni Mbowe amemtuma au amekubaliana nae. Kama ni hivyo, mbona mikutano ya Lissu haionekani kuwa na proper logistical support? Mfano ni huu, Lissu akiwa kwenye jukwaa la mabanzi (Kichanja) Huu kweli ni mkutano uliopangwa na Chadema kama chama au individual stand alone arrangements?.

Kama hayo Lissu anayozunguka kuyasema ni yake na hajatumwa na yeyote, then CHADEMA kina wajibu wa kumdhibiti, na wasipo mdhibiti now, huko mbele atakuja kuwagharimu very dearly!

Kwenye issue ya katiba mpya Rais Samia anaihandle vyema, ameunda kikosi kazi huku akifanya mazungumzo ya maridhiano na CHADEMA, kwa stage tuliofikia, ni nzuri na haihitaji mapambano na mapigano, sasa hizi lugha za kianaharakati za Lissu, anapambana na nani? Na Mama? na CCM au.

My Take
Ili Chadema ifanikiwe kwenye jambo lake lolote, viongozi wake wakuu, Chairman, VC na SG, lazima wazungumze pamoja, kwa lugha moja na sauti moja na sio kama hali ilivyo sasa kila mtu anazungumza lake, na kwa upande wa maandalizi ni kila mtu na lwake.

Viongozi wawili wakuu mnapo toa kauli zinazopishana pishana, mnawachanganya wafuasi wenu kujiuliza washike lipi?

Kwe haya Mapambano ya katiba mpya, jee Mbowe na Lissu ni pamoja?

Paskali.
Hivi Magufuli na Samia walikuwa wanaongea lugha moja? Mbona uliufyata
 
Kwa ninavyoona Lissu, Mnyika, Heche na wengine wanzungumza lugha moja, lugha inayopendwa na wanachadema.

Mbowe, Msigwa, Sugu na wengine wanzungumza lugha yao nyingine ambayo inaonekana kuwa ya 'walamba asali'

Sijui kama wamekubaliana au la, lakini hali sio shwari CDM. Hizi ziara za Lissu ni kama zinamlazimisha Mbowe akurupuke nayeye aanze kuzunguka huku na huko ili aonekane bado yupo.
 
Chadema hakuna mtu wa kuandamana.
Hapo ndipo unapokosea,

IPO nguvu ya asili inayoyaunganisha makundi mbalimbali ya wananchi kudai HAKI,

Umeona Wafanyabiashara wakiandamana, utawaona wafanyakazi, wamachinga, wasafirishaji, wakulima, wanamichezo, wote wanaamshwa kudai HAKI juu ya nchi mbali na wanasiasa.

Ikiwa Unadhani mambo yataendelea kuwa yalivyo,

Tusubiri.
 
Back
Top Bottom