Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kikao cha siku 2 cha NEC ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kimemalizika na kutoa taarifa kupitia katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho,bwana Nape Nnauye kuwa wamekubaliana kuendelea na msimamo wa kuunga mkono serikali 2.

Pia,bwana Nape ameongeza kuwa watafanyia kazi changamoto za muungano zinazolalamikiwa ambapo wameendaa hoja za kuziwasilisha katika bunge la katiba.Hoja hizo ambaza amekataa kuzitaja ndio zitakuwa na maelezo ya namna ya kutatua kero za muungano

Katika hatua nyingine,Nape amesema hawatishiwa na hatua ya vyama vingine kwenda kwa wananchi kwani hata wao(CCM) wanaweza kwenda kwa wananchi na kuwaeleza jambo hilo.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Hatua hii ni sawa na kutangaza mgogoro mapema!
 
Kwani kulikuwa na haja ya kutangaza wakati hilo linajulikana ? Huu ni ujinga kupinga maoni ya wananchi ambao keshoutaenda kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza wakati hujalifanyia maoni yao ........
Ni vema kuliweka wazi hilo ili watanzania wasipotoshwe na wenye uchu wa madaraka
 
Serikali tatu, mgombea binafsi haviepukiki!
Chama Cha Mwabepande tumieni akili badala ya masabur
 
Msimamo wa ccm ndio msimamo wa wananchi wote wa tanzania wapenda amani na maendeleo,anayepinga serikali MBILI huyo anataka kutubagua watanzania na kuleta chokochoko zisijo na tija!! Kidumu chama cha mapinduzi
 
Ya Tanganyika na Zanzibar sio ? Ama unazungumzia mbili kwa maana gani? By the way wewe ndio yule mwalimu uliyeshindwa kuitetea paper yako Finland baada ya Plagiarism?
 
Naona dalili za kupata katiba mpya sasa zimeeanza kuonekana mapema serikali mbili ndiyo mpango mzima ndiyo zimetufikisha hapa tulipo.
 
Ya Tanganyika na Zanzibar sio ? Ama unazungumzia mbili kwa maana gani? By the way wewe ndio yule mwalimu uliyeshindwa kuitetea paper yako Finland baada ya Plagiarism?
Eti nini wewe mzima kweli.
 
Watanzania tunapaswa kuamua kusuka au kunyoa.

Kama alivyosema JK,watanzania na sisi tuache unyonge na ikibidi tuingie mabarabarani.
Mbona kila siku tupo barabarani wewe unataka barabara ipi au kwa mtei zipo zingine unamaanisha.
 
Back
Top Bottom