Katiba Mpya ni hitaji la Wananchi, vyama vya siasa ama?

Gellangi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2016
Posts
2,782
Reaction score
3,018
Habari zenu wana jukwaa letu pendwa JF.

Nimejiuliza swali hili bila kupata jibu la kuridhisha fikra zangu na hivyo ninadhani ni busara kushirikisha wana jukwaa.

Madai ya Katiba Mpya ni nani hasa mhusika wake?Je,ni wananchi,vyama vya siasa au?

Nauliza kwa kuwa sasa ni dhahiri kuwa wanaodai katiba mpya ni wapinzani wa CCM wakiongozwa na CHADEMA na wanaopinga upatikanaji wa katiba mpya ni wana CCM na watu waliopo Serikalini.

Tujiulize, kwanini kila anayedai katiba mpya anahusishwa na wapinzani wa CCM na wanaopinga upatikanaji wake wanakuwa na ukaribu ama wanachama wa CCM?

Je, CCM wanaamini kuwa katiba tuliyonayo ni bora kwa Watanzania? Katiba ya 1977 inaleta ugali mezani kwa wasiokuwa wanccm?

Nimesikia CCM wakishabikia kuwa eti Mh. Mbowe hakuongelea suala la Katiba Mpya alipohutubia kongamano la BAWACHA kule Iringa juzi,hiyo imewapa nafuu CCM au Serikali isiyohitaji katiba mpya kwa kiwango gani?Je,Katiba Mpya ni kwa ajili ya CHADEMA?

Tujadili.
 
Hivi ni kwa nini CCM hawataki Watanzania tupate Katiba Mpya?Kwani katiba iliyopo ilishushwa kama vitabu vitakatifu na hatutakiwi kuvibadilisha au kuhoji?

Nini faida wanayopata wananchi kwa kuendelea kuongozwa na katiba ya analog ilhali dunia sasa ni digital?

Tujadili bila mihemko ya vyama kwa sababu hii tunayoidai siyo katiba ya chama chochote cha siasa bali ni katiba ya nchi yetu.
 
Jukumu la kudai Katiba Mpya ya Tanzania ni jukumu letu sote na siyo la CDM na jukumu la kuikataa Katiba Mpya siyo la CCM bali Watanzania kupitia Referendum.

Tunashuhudia CCM wanavyojitahidi kuchelewesha/kukwamisha Watanzania kupata Katiba Mpya,sisi wengine tunashangazwa na hoja zao.

Watanzania hawajasahau maumivu ya fedha na muda walioupoteza wakati wa mchakato wa kukusanya maoni chini ya Jaji Warioba na Bunge la Katiba.Nani analipia hiyo hasara?

Nyie CCM wakati ule wa uandishi wa Katiba Mpya mlijazana Bungeni kutafuta fedha za kujikimu?
 
Jukumu la kudai Katiba Mpya ya Tanzania ni jukumu letu sote na siyo la CDM na jukumu la kuikataa Katiba Mpya siyo la CCM bali Watanzania kupitia Referendum...
Yanapoanza kuulizwa maswali kama haya yenye jazba, ile nia ya kuwepo katiba mpya inazidi kuchelewa.

Inakuwa ni sababu ya kucheleshwa kwa uwepo wa katiba mpya.
 
Jazba ipo wapi hapo?Anayechukia jazba ndiye anatunyima tusidai Katiba Mpya?Huyo anayechelewesha upatikanaji wa Katiba Mpya ndiye mmiliki wa katiba ya zamani au yeye anafaidika nini tunapolazimika kuitii katiba ambayo kila Mtanzania anafahamu upungufu wake?
Wewe Philipo upo upande upi?Wanaodai Katiba Mpya au wanaopinga hoja hiyo?
 
Wapinzani wa Katiba Mpya mpo?Hamna majibu ya swali la wanaodai mabadiliko ya Katiba?
Kama Katiba tuliyonayo ni bora semeni ili tuache kuwasumbua wananchi na iwapo siyo tuandike Katiba Bora zaidi ili JMT pawe sehemu nzuri ya kuishi.Bali kama katiba tuliyonayo imepitwa na wakati mbona mnazuia isipatikane mpya?
Tujadili.
 
Jazba ipo wapi hapo?Anayechukia jazba ndiye anatunyima tusidai Katiba Mpya?Huyo anayechelewesha upatikanaji wa Katiba Mpya ndiye mmiliki wa katiba ya zamani au yeye anafaidika nini tunapolazimika kuitii katiba ambayo kila Mtanzania anafahamu upungufu wake?
Wewe Philipo upo upande upi?Wanaodai Katiba Mpya au wanaopinga hoja hiyo?
Wanaodai katiba mpya kwani wakati umefika, tatizo ni ukweli kwamba kuipata kuna ugumu wake.

Wanaoweka kauzibe ni wale wanaofaidika na hali ya sasa japokuwa tunaweza kupiga hatua sana pasipo kuibadili ya sasa.

Kuna nchi zina katiba mbovu kuliko hii ya Tanzania lakini zipo sawa kiuchumi kutuzidi.
 
Upo sawa kwamba baadhi ya nchi zinaweza kuwa na katiba mbovu lakini zikawa na uchumi mzuri ingawa sizifahamu.
Ukija hapa kwetu je?Tuna Katiba mbaya na kiuchumi tupo dhoofu hali.Tukijiuliza kuwa tunakwama wapi,jibu ni ubovu Wa katiba inayoweka watawala madarakani badala ya viongozi na katiba haitoi mbadala Wa kupata viongozi bora.
Mwl.Nyerere alituambia ili tuendelee tunahitaji vitu vinne;
1.Ardhi
2.Watu
3.Siasa safi
4.Uongozi bora.
Tumekuwa na utawala Wa TANU&ASP tokea Uhuru hadi 1977 na kuanzia hapo tupo na CCM had I Leo.Je, tumekosa nini hata tusiendelee?Sisi wajuzi tunatambua kuwa kilichokosekana hapa ni uongozi bora na siasa safi kupitia katiba ya nchi.
Je,wewe Phillipo upo upande Wa Katiba Mpya au ya zamani?Yafaa kufahamiana.
 
Uongozi kukosolewa haina maana kwamba umepoteza ubora na uhalali. Trump alikosolewa alipokuwa white house na sasa anamkosoa Biden na serikali yake ya democrats.

Naamini hata hao walio nje ya ikulu wakipewa ikulu leo hii tutawakosoa na umuhimu wa katiba mpya kwa muktadha huu wa sasa utaonekana kuwepo.

Hakuna rais au awamu ambayo kwa asilimia mia moja imekubalika miongoni mwa wadau wa siasa, kila rais anayekuwepo ikulu huonekana aliyeondoka alikuwa na afadhali kumzidi!.

Kuna zile picha ni maarufu sana zenye kuonyesha marais wanne wakiwa wamepanga mstari pale Dodoma, zilipigwa 2015 baada ya JPM kuhutubia bunge, sisi tunaziona ni picha za kawaida lakini majirani zetu hawawezi kupiga picha kama zile, wanazionea wivu.
 
Sahihi kabisa,marais/watawala wengi hapa Afrika wanajikuta wakitenda uhalifu mwingi wawapo madarakani na hivyo huondolewa kwa namna ambavyo visasi/chuki havizuiliki.
Bila kufahamu kuwa kuepuka hali ya uhasama na uwezekano Wa kutenda uhalifu dhidi ya ubinadamu in mifumo bora ya upatikanaji Wa viongozi kupitia Katiba Bora.Wengi hujuta baada ya kuondoka madarakani.
Hakuna mbadala Wa Katiba Bora ili nchi zetu za Kiafrika ziweze kupata maendeleo endelevu kwa wote.
Nakushukuru kwa kuendeleza mjadala.Tujadili.
Iwapo wananchi wamehitaji kuandika Katiba Bora itakayoweka Dira ya Taifa;Ni nani mwenye mamlaka ya kuwazuia?Wanaofanya hivyo wanamwakilisha nani hasa? Karibu.
 
Wananchi wanadhani kila utatuzi wa tatizo lililopo ni katiba mpya. Foleni haitembei ndani ya benki kisingizio ni katiba mpya, kumbe mtandao upo chini kwa siku hiyo.

Vitu vikipanda bei tatizo ni katiba mpya, kumbe ni masuala ya demand na supply yanayosumbua ulimwengu mzima, pengine ni madhara ya vita ya Russia/Ukraine.

Tunadhani kila tatizo utatuzi wake ni wa kudumu na ni uwepo wa katiba mpya peke yake. Ni mtazamo hasi usiotaka kuumiza kichwa na kufikiria zaidi ya ambavyo tumeshafikiria.
 
Umeelewa kweli mjadala uliopo au unapotosha?Unaamini kuwa mifano uliyotoa inahalalisha upinzani wa Katiba mpya hapa Tanzania?
Tunahitaji Katiba mpya kwa sababu hii tuliyonayo imeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi.Tumeshuhudia Katiba ikivunjwa na kupata viongozi wabovu halafu hatuna la kufanya.
 
Sidhani kama imeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi. Siwadharau hao wanaoitwa wananchi lakini naunga mkono wengi wao kushindwa kutafsiri kinachofanywa na serikali kwa manufaa yao wenyewe.

Tatizo la elimu alilozungumzia Lowassa ni pamoja na uelewa mdogo wa masuala mengi ya kisiasa, ambao wanaoitwa wananchi wanaitumia katiba mpya kama suluhisho la matatizo waliyonayo.

Wengi wetu tunazo zile akili za jumla, za kusomea magazeti haswa haya ya kawaida bila ya uwezo mpana wa kufanya tafakuri zile muhimu zenye kuhusiana na mustakabali wa kitaifa.

Ukitekwa na hizi habari za magazeti ya kila siku, utakuwa na fikra za kawaida sana, na kila kinachofanywa na serikali utakichukulia kama suluhisho ni katiba mpya.
 
Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi Ni Mahitaji ya Wanasiasa.

Katiba mpya Bora na Wananchi haiwezi Kuandikwa na Wanasiasa.

Above all, Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi siyo mwisho wa matatizo.

Kenya na Zanzibar wameshaandika Katiba mpya na Wana Tume huru ya uchaguzi lakini mpaka leo matatizo yako pale pale.f

Screenshot_2022-03-11-05-29-13-617_com.twitter.android.png
 
Sidhani kama imeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi. Siwadharau hao wanaoitwa wananchi lakini naunga mkono wengi wao kushindwa kutafsiri kinachofanywa na serikali kwa manufaa yao wenyewe.

Tatizo la elimu alilozungumzia Lowassa ni pamoja na uelewa mdogo wa masuala mengi ya kisiasa, ambao wanaoitwa wananchi wanaitumia katiba mpya kama suluhisho la matatizo waliyonayo.

Wengi wetu tunazo zile akili za jumla, za kusomea magazeti haswa haya ya kawaida bila ya uwezo mpana wa kufanya tafakuri zile muhimu zenye kuhusiana na mustakabali wa kitaifa.

Ukitekwa na hizi habari za magazeti ya kila siku, utakuwa na fikra za kawaida sana, na kila kinachofanywa na serikali utakichukulia kama suluhisho ni katiba mpya.
Hapo ni kama unashauri tuisubiri serikali itakapoamua kutuandikia Katiba Mpya?Kama wananchi wa Tanzania wamesomeshwa na serikali yao at least miaka 7 na bado hawana uelewa nani wa kulaumiwa?Je hoja na habari za magazetini ni za kupuuzwa?
Jambo la Katiba Mpya ni kuhusu ujenzi wa misingi bora ya nchi yetu.Hapo hakuna cha wananchi kutokuelewa.Wazalendo walioandika Katiba ya Tanzania 1964 na 1977 walipatia wapi ufunuo wa kuandika yasiyobadilishika hata nyakati hizi za digital error?Walikuwa malaika nini?
Tuache kujishusha kuwa hatuwezi kujitengenezea hata regulation za kutuongoza wenyewe hadi leo?
 
Habari zenu wana jukwaa letu pendwa JF.

Nimejiuliza swali hili bila kupata jibu la kuridhisha fikra zangu na hivyo ninadhani ni busara kushirikisha wana jukwaa.

Madai ya Katiba Mpya ni nani hasa mhusika wake?Je,ni wananchi,vyama vya siasa au?

Nauliza kwa kuwa sasa ni dhahiri kuwa wanaodai katiba mpya ni wapinzani wa CCM wakiongozwa na CHADEMA na wanaopinga upatikanaji wa katiba mpya ni wana CCM na watu waliopo Serikalini.

Tujiulize, kwanini kila anayedai katiba mpya anahusishwa na wapinzani wa CCM na wanaopinga upatikanaji wake wanakuwa na ukaribu ama wanachama wa CCM?

Je, CCM wanaamini kuwa katiba tuliyonayo ni bora kwa Watanzania? Katiba ya 1977 inaleta ugali mezani kwa wasiokuwa wanccm?

Nimesikia CCM wakishabikia kuwa eti Mh. Mbowe hakuongelea suala la Katiba Mpya alipohutubia kongamano la BAWACHA kule Iringa juzi,hiyo imewapa nafuu CCM au Serikali isiyohitaji katiba mpya kwa kiwango gani?Je,Katiba Mpya ni kwa ajili ya CHADEMA?

Tujadili.
Watanzania wanataka maendeleo wakati huo viongozi wa upinzani wanataka katiba mpya.
 
Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi Ni Mahitaji ya Wanasiasa.

Katiba mpya Bora na Wananchi haiwezi Kuandika na Wanasiasa.

Above all, Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi siyo mwisho wa matatizo.

View attachment 2147275
Umejielekeza isivyo,wanasiasa ni wananchi na kiujumla kila mtu,kila tufanyalo ni siasa na hakuna wakati ambapo tutaacha siasa hadi mauti yatakapotuondoa duniani.I think every human being is a politician by nature.
Pia tuzingatie kuwa kubaki na katiba chakavu siyo suluhisho sahihi.
Mnaoginga katiba mpya msituchukulie poa kuwa hatuna uelewa.
 
Siasa ni nini ?
 
Umeanza lini kufuatilia siasa?

Mbowe, Lissu, Awenya, Msigwa, Heche, Mnyika, Sugu ni MATAJIRI.

Wewe subiria Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ili matatizo yako ya kiuchumi na Uhuru upatikane.

Dunia hii, kama huna vipaumbele Maisha yako yote utayatumia kufaidi watu wengine.

Narudia tena, sipingi Katiba mpya Wala Tume huru ya uchaguzi lakini usitegemee hivi vitu Ni suluhisho la kila tatizo katika Maisha yako hasa kama wewe hauko kwenye tabaka la kisiasa.
 
Watanzania wanataka maendeleo wakati huo viongozi wa upinzani wanataka katiba mpya.
CCM wanang'ang'ania katiba chakavu na bado wananchi hawana maendeleo kwa miaka 61 y
Siasa ni nini ?
Mimi nadhani wewe unamajibu ya hilo swali,umetuambia Katiba Mpya ni hitaji la wanasiasa.Ulikuwa unajadili usichokifahamu?
 
Back
Top Bottom