Katiba Mpya ni hitaji la Wananchi, vyama vya siasa ama?

Katiba Mpya ni hitaji la Wananchi, vyama vya siasa ama?

Unadhirisha kuwa wewe kichwa chako hakina hata chembe ya hekima,unaashiria...
Hata hivyo washukuru sana jf family,who are Great Thinkers kwa kukuvumilia.
Jaribu kunena na kuwaza ukiwa chanya,hoja ipo wazi kabisa lakini unaififisha kwa kufanya mizaha isiyokuwa na msaada wowote kwa yeyote.Umejazwa uzembe wa kufikiri na hao wasiotaka Katiba Mpya ili wajinufaishe.
 
Kama nchi za namna hiyo zipo hadi sasa, basi wana bahati ya kuwa na maraisi kama Nyerere; siku wakipata marais tofauti na wa aina ya Nyerere, wataumia sana.
Hata kama zipo ni wazi kuwa watu wake watakuwa na changamoto zao.
Hivi kwa nini watanzania tunakubali kudumazwa kujitengenezea model yetu ya namna ya kujiongoza kwa kuandika katiba inayokidhi mahitaji ya sasa ya dunia ya kidigitali?
Nani mwenye mamlaka ya kutunyima HAKI ya kuandika katiba yetu?
 
Bado sijapata jibu,Katiba ni hitaji la nani hasa?Wapo wanaoamini ni hitaji la wanasiasa,sisi wengine tunaamini na tunafahamu kuwa Katiba Mpya ni hitaji letu wananchi na ndiyo maana tulishiriki kutoa maoni yetu mbele ya Tume ya Jaji Warioba.
Wanaoshupalia kuwa Katiba Mpya ni hitaji la wanasiasa nao wanaoipinga ni wanasiasa pia.
Wa Tanzania tulilipia ule mchakato kwa gharama kubwa na wanasiasa wakaivuruga tukakosa wote.
Jukumu letu ni kuungana ili tupate Katiba Mpya ya wananchi.
 
Back
Top Bottom