Katiba Mpya ni kete kwenye ilani ya CHADEMA 2025

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
KATIBA MPYA NI KETE KWENYE ILANI YA CHADEMA 2025.

Leo 09:15hrs 07/07/2021

Je CCM itakuja na agenda hii kwenye ilani ya kutafutia kura? Je tumeutafakari uzuri na ubaya wa katibs tuliyonayo!? Je tumeshatafakari uzuri na ubaya wa katiba Mpya tunayoitaka!?

Katiba tuliyonayo haikutuvusha wakati wa msiba bali hekima za Watanzania,Busara za Watanzania,na Uvumilivu wa Watanzania,tusiwekeze kwenye hekima,Busara na Uvumilivu tuwekeze kwenye katiba Mpya itayotoa ridhaa ya Watanzania wote baada msiba maana kesho na kesho kutwa watakuja watu wasio na hekima, Busara wala Uvumilivu.

Katiba ya sasa haifikii ukuu wa taasisi ya Urais,Ukuu wa katiba unaishia pale Rais anaposhika madaraka,Sasa hili ni tatizo kubwa kwa maana itahitaji utashi wa Rais kuendesha nchi,tuwekeze kwenye katiba Mpya kwenye madhara ya uvunjaji wa katiba, Rais aweze kuwaji bishwa na taasisi nyingine.

Je ipitishwe katiba pendekezwa ya Warioba au tuanzie alipoishia Jaji Warioba au tuanzie kwenye sheria inayoruhusu kuandika katiba mpya,ni kweli katiba Mpya haipo kwenye ilani ya CCM lakini utashi wa Mh Rais unaweza kuileta katiba Mpya,mambo muhimu yote yatafanywa tukiwa na katiba inayotia mkazo maendeleo ya nchi,

Nimalizie kwa kusema Ilani ni nyenzo ya kutafutia kura Uchaguzi ujao.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
 
CHADEMA wamesema hawashiriki uchaguzi
 
Hapo ndio watajua kipaumbele cha Watanzania sio katiba mpya bali ni maendeleo na maisha bora.
 
Suala la kuanzia ni kuihisisha sheria ili watu watakaoshughulikia katiba wasiwe na maslahi binafsi ndani ya katiba hiyo mpya
 
Nyie wapumbavu kweli, mjue kuwa katiba siyo priority ya Watz walio wengi ni lenu tu wasaka madaraka na hata mkilihubiri majukwaani watawaona mazuzu tu.Ajenda zinazogusa watu kama ufisadi nk hamzipi kipaumbele tena mmeng'ang'ania katiba katiba katiba pumbavu kabisa.
 
Waache wahangaike Mkuu,mwisho wasiku wananchi watawapa za uso tena wabaki wakisema wameibiwa kura.

Tatizo la wapinzani wa nchii ni mihemko. Wanadhani wakibebea bango jambo moja ndo kura zipo hapo. Tofauti na Kigogo,Maria Sarungi,viongozi wachache wa. CDM,mitaani hawaujui huo wimbo wa katiba mpya.

Nashangaa tu Rais wangu na yeye anademka na mambo ya mitandaoni.
 
Yani uje na kipaumbele cha katiba halafu wanachi wakupe kura?

Angalia hata hii kampeni ya sasa hivi ni kakikundi ka watu wajinga wachache sana ndio wamekomalia na itakufa muda si mrefu!
 
Wengi wanaoshadidia katiba mpya wanaangalia tu madaraka ya Rais. Kuna mengi zaidi ya hayo
Katiba ya sasa rais ndiyo nchi.

Anaweza kuamua wewe ufe leo na ukafa na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua wewe usiwe raia leo na ukawa hivyo na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua wewe uwe kizuizini leo au upotee kama sindano ukapotea na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua pale kijijini kwenu pasifanyike chochote cha maendeleo na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua abomoe Jiji lote la Dar es Salaam lihamishiwe Kilombero na hatafanywa chochote.

Sasa nakuuliza wewe bado unataka katiba ya namna hii ?
 
Chadema wanaona mbali sana. Na kwakuwa kika mtanzania kaona makosa ya katiba hii awamunya tano hii itakuwa balaa.

wait and see
 
Katiba ya sasa rais ndiyo nchi.

Anaweza kuamua wewe ufe leo na ukafa na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua wewe usiwe raia leo na ukawa hivyo na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua wewe uwe kizuizini leo au upotee kama sindano ukapotea na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua pale kijijini kwenu pasifanyike chochote cha maendeleo na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua abomoe Jiji lote la Dar es Salaam lihamishiwe Kilombero na hatafanywa chochote.

Sasa nakuuliza wewe bado unataka katiba ya namna hii ?
Usikurupuke soma nilichoandika kwanza. Nakubaliana nawe ila kuna mengi ambayo yanahitajika kubadilishwa, si mamlaka ya urais tu
 
Wengi wanaoshadidia katiba mpya wanaangalia tu madaraka ya Rais. Kuna mengi zaidi ya hayo
Madaraka ya Rais ndio msingi wa ubovu. Maana hata mahakama haiko huru kwa sababu Rais yuko juu ya mahakama. IGP ma CDF hivyo hivyo
 
Katiba ya sasa rais ndiyo nchi.

Anaweza kuamua wewe ufe leo na ukafa na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua wewe usiwe raia leo na ukawa hivyo na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua wewe uwe kizuizini leo au upotee kama sindano ukapotea na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua pale kijijini kwenu pasifanyike chochote cha maendeleo na hatafanywa chochote.

Anaweza akaamua abomoe Jiji lote la Dar es Salaam lihamishiwe Kilombero na hatafanywa chochote.

Sasa nakuuliza wewe bado unataka katiba ya namna hii ?
Katiba iliyopo tatizo namba moja ni madaraka ya Rais. Sio tumnynganta madaraka hayo bali yawe na moderation.

Rais anaweza kuagiza jeshi likabangue korosho kwa meno na hakuna anayebisha. Huu ni upuuzi
 
Madaraka ya Rais ndio msingi wa ubovu. Maana hata mahakama haiko huru kwa sababu Rais yuko juu ya mahakama. IGP ma CDF hivyo hivyo
Kwa mtaji huo, unadhani ni nani wakuweza kukubali ajipunguzie umungu mtu akiwa madarakani? Uliona jinsi Kikwete alivyogeuza kibao wakati ule?
 
Usikurupuke soma nilichoandika kwanza. Nakubaliana nawe ila kuna mengi ambayo yanahitajika kubadilishwa, si mamlaka ya urais tu
Kwani wanaosema wanataka katiba mpya si ndiyo kubadili hayo mambo mengi unayoyasema hapo ?

Au unafikri wanataka kupunguza madaraka ya rais tu ?
 
Kwa mtaji huo, unadhani ni nani wakuweza kukubali ajipunguzie umungu mtu akiwa madarakani? Uliona jinsi Kikwete alivyogeuza kibao wakati ule?
Kwa kweli ni ngoma nzito. Lakini sio sababu ya kutopiga na kupaza sauti mpaka wakubali. Tukiwa wamoja inawezekana. Ile hatua iliyofika ni 50% Twaweza kwenda tena 75%
 
Katiba iliyopo tatizo namba moja ni madaraka ya Rais. Sio tumnynganta madaraka hayo bali yawe na moderation.

Rais anaweza kuagiza jeshi likabangue korosho kwa meno na hakuna anayebisha. Huu ni upuuzi
Kama kuna watu hawakujifunza jambo juu ya umuhimu wa katiba katika awamu ya Tano na uchaguzi wa Marekani 2020 hakuna kingine tutawahubiria wakaelewa
 
Kwani wanaosema wanataka katiba mpya si ndiyo kubadili hayo mambo mengi unayoyasema hapo ?

Au unafikri wanataka kupunguza madaraka ya rais tu ?
Kweli kichwa chako kigumu! Nakubali kuwa madaraka ya Rais yanatakiwa yapunguzwe ila siyo hayo tu.
 
Ndiyo maana wanataka katiba mpya.

Kama wangekuwa na nia ya kupunguza madaraka ya rais si wangeomba amendments tu ?
 
Back
Top Bottom