Katiba Mpya ni muhimu kwa Sekta Zote

Katiba Mpya ni muhimu kwa Sekta Zote

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Uwepo wa mustakabala mpya wa mahusiano baina watu na watu pia watu na serikali hauwezi kudunishwa.

Ni muhimu kuzipitia sekta mbalimbali katika kuamshana kwenye harakati hizi takatifu.

Tuanze hapa na Sekta ya Usafirishaji:

Sekta hii ni katika sekta zilizonyanyasika vilivyo.

Ukitaka kunyanyaswa bila sababu nunua au endesha gari na hasa likiwa la biashara (abiria au lorry).

Dereva wa gari la abiria rushwa kwa polisi ni wajibu. Kila siku kuna jipya. Standard PGO hamna. Haya ya ajali ni janja ya nyani tu:

Ilikuwa ving'amuzi leo speed governor. Hakueleweki kushoto wala kulia.

Hii ni sekta binafsi lakini serikali imelazimisha mkono wake humo pasipokuwa na uhalali wowote.

Madereva hawa wanatakiwa kustaafu kwa lazima ya serikali wafikapo umri wa miaka 60.

Cha ajabu ni kuwa kwanini takwa la kustaafu kwa lazima haliko kwa wanasiasa au katika sekta zingine zozote binafsi?

Au ni mwendo wa kustaajabu ya Mussa tu?
 
Wewe ni nani ?

Hao wanaitwa ma time saver. Hawana lolote.

Kumbe ukinunua gari lako la biashara kwa mujibu wa sheria ukifikisha miaka 60 huruhusiwi hata kuligusa?!

Ila wanasiasa wao ndiyo bwerere kwa raha zao?

Sekta kwa Sekta yatambulike maswahiba yao kuwatambulisha mwisho wake u njiani.
 
Chadema bhana 😂😂 baada ya kuona wamekosa ulaji bungeni ndo wamekuja na kelele za katiba mpya
 
Katiba mpya ilikwamishwa na wanasiasa.
Haiwezi kuletwa na wanasiasa.
Katiba mpya sio Mali ya CCM wala Wapinzani hasa Chadema.
Ili katiba mpya ipatikane ni Lazima Chadema wajivue koti kudai katiba mpya kwanza na CCM wajivue koti la katiba mpya sio kipao mbele chao.

Katiba mpya ibaki kuwa ni Mali ya wananchi kama lilivyo Jeshi la wananchi.

Kila mwananchi ameshaona udhifu wa katiba ya zamani iliyochakaa. Katiba iliyoundwa na watu waliokuwa na Tamaa ya kutawala kwenye nafasi walizoachiwa na Wakoloni maadui wa Afrika.

Wale wasomi waliokuwa wamejipenyeza katikati ya wapigania Uhuru wazalendo walikua ni waafrika waliokuwa wamelelewa na kukaa na Wakoloni na kutamani sana kuishi maisha ya anasa na ufahari na ubwana mkubwa kama walivyokuwa Wakoloni . Waliaminiwa na kukaribishwa na wapigania Uhuru waliokuwa wameumizwa na ukoloni, baada ya Uhuru wasomi wakavaa makoti yote ya Ukoloni mpaka Leo kwa kutumia sheria na Katiba ya Wakoloni iliyochangamka tu.

Hivyo kwa sasa watanzania wote ni vizuri tukawakataa wakoloni weusi na tamaa zao.
Wala rushwa Leo ndio wanaozuia katiba mpya kwa muavuli wa dola.
Wahujumu uchumi ndio wanaojificha chini ya mwavuli wa chama Tawala kuzuia katiba mpya ili waendelee kuwarithisha watoto wao rasilimali za nchi bila kuweka ushindani sawa.
Ndio maana hawataki chaguzi huru ili wasije wakatokea watoto wa wakulima wenye uwezo na fikra pevu kama akina Alfonsi Mawazo kule Geita. Wanatumia Katiba inayowapa nafasi ya kuwaua na kuwapoteza watoto wa wengine nje ya familia zao ili Keki isije ikawafikia wengine nje ya chama chao cha ulaji.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Daah hizo takwimu mmepiga lini mbona mm na jamaa zangu zaid ya watatu hapa kitaa hatuhitaji hy katiba au hao watu watatu ni viumbe gani

Twaweza ni taasisi hujawahi kuisikia?

Twaweza iliwahi pia kusema CCM na jiwe inaungwa mkono na wajinga bila shaka ukiwamo wewe na hao wenzio hapo kitaani - Lumumba.

Twaweza ndiyo waliomfanya jiwe kujaa upepo na kuja na ile sheria ya takwimu.

Hao ndiyo twaweza.

Subiri huko Chatto ni mkoa utangazwe.
 
Twaweza ni taasisi hujawahi kuisikia?

Twaweza ili wapi pia kusema CCM na jiwe inaungwa mkono na wajinga bila shaka ukiwamo wewe na hao wenzio hapo kitaani - Lumumba.

Twaweza ndiyo waliomfanya jiwe kukaa upepo na kuja na ile sheria ya takwimu.

Hao ndiyo twaweza.

Subiri huko Chatto ni mkoa utangazwe.
Sawa nakubaliana na hayo yote, sasa nambie hao watu watatu n viumbe gani mbona sisi wengine hatuhitaji hy katiba.?
 
Huelewi nini kuhusu 66.7% probability?

Au ni katika kuthibitisha yaliyokwisha anikwa kwenye tafiti za nyuma za twaweza?
 
Hao ni hawa hapa

Huelewi nini kuhusu 66.7% probability?

Au ni katika kuthibitisha yaliyokwisha anikwa kwenye tafiti za nyuma za twaweza?
Em lala hukooooooo hakuna cha katiba mpya wala baba ake katiba mpya
 
Tulishasema hiii katiba inayodaiwa na vikundi vyenye masilahi ya vyama vyao vya kisiasa itakuwa katiba ya hovyo kutokea duniani kote. Katiba yakweli italetwa na wanawanchi wasio na mlengo wa chama chochote cha kisiasa.

Uwepo wa mustakabala mpya wa mahusiano baina watu na watu pia watu na serikali hauwezi kudunishwa.

Ni muhimu kuzipitia sekta mbalimbali katika kuamshana kwenye harakati hizi takatifu.

Tuanze hapa na Sekta ya Usafirishaji:

Sekta hii ni katika sekta zilizonyanyasika vilivyo.

Ukitaka kunyanyaswa bila sababu nunua au endesha gari na hasa likiwa la biashara (abiria au lorry).

Dereva wa gari la abiria rushwa kwa polisi ni wajibu. Kila siku kuna jipya. Standard PGO hamna. Haya ya ajali ni janja ya nyani tu:

View attachment 1973505

Ilikuwa ving'amuzi leo speed governor. Hakueleweki kushoto wala kulia.

Hii ni sekta binafsi lakini serikali imelazimisha mkono wake humo pasipokuwa na uhalali wowote.

Madereva hawa wanatakiwa kustaafu kwa lazima ya serikali wafikapo umri wa miaka 60.

Cha ajabu ni kuwa kwanini takwa la kustaafu kwa lazima haliko kwa wanasiasa au katika sekta zingine zozote binafsi?

Au ni mwendo wa kustaajabu ya Mussa tu?
 
Tulishasema hiii katiba inayodaiwa na vikundi vyenye masilahi ya vyama vyao vya kisiasa itakuwa katiba ya hovyo kutokea duniani kote. Katiba yakweli italetwa na wanawanchi wasio na mlengo wa chama chochote cha kisiasa.

Mlisemea wapi hayo na mkiwa na nani mjumbe mpya?

Mada umeielewa lakini?

Kama dereva wa gari la biashara anahitaji katiba mpya sekta ipi haina uhitaji huo?

Hali kadhalika usisahau vyama vya siasa ni sekta pia katika ujumuishi wake.
 
Katiba mpya ilikwamishwa na wanasiasa.
Haiwezi kuletwa na wanasiasa.
Katiba mpya sio Mali ya CCM wala Wapinzani hasa Chadema.
Ili katiba mpya ipatikane ni Lazima Chadema wajivue koti kudai katiba mpya kwanza na CCM wajivue koti la katiba mpya sio kipao mbele chao.

Katiba mpya ibaki kuwa ni Mali ya wananchi kama lilivyo Jeshi la wananchi.

Kila mwananchi ameshaona udhifu wa katiba ya zamani iliyochakaa. Katiba iliyoundwa na watu waliokuwa na Tamaa ya kutawala kwenye nafasi walizoachiwa na Wakoloni maadui wa Afrika.

Wale wasomi waliokuwa wamejipenyeza katikati ya wapigania Uhuru wazalendo walikua ni waafrika waliokuwa wamelelewa na kukaa na Wakoloni na kutamani sana kuishi maisha ya anasa na ufahari na ubwana mkubwa kama walivyokuwa Wakoloni . Waliaminiwa na kukaribishwa na wapigania Uhuru waliokuwa wameumizwa na ukoloni, baada ya Uhuru wasomi wakavaa makoti yote ya Ukoloni mpaka Leo kwa kutumia sheria na Katiba ya Wakoloni iliyochangamka tu.

Hivyo kwa sasa watanzania wote ni vizuri tukawakataa wakoloni weusi na tamaa zao.
Wala rushwa Leo ndio wanaozuia katiba mpya kwa muavuli wa dola.
Wahujumu uchumi ndio wanaojificha chini ya mwavuli wa chama Tawala kuzuia katiba mpya ili waendelee kuwarithisha watoto wao rasilimali za nchi bila kuweka ushindani sawa.
Ndio maana hawataki chaguzi huru ili wasije wakatokea watoto wa wakulima wenye uwezo na fikra pevu kama akina Alfonsi Mawazo kule Geita. Wanatumia Katiba inayowapa nafasi ya kuwaua na kuwapoteza watoto wa wengine nje ya familia zao ili Keki isije ikawafikia wengine nje ya chama chao cha ulaji.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app

Vyama vya siasa, wenye maslahi kisiasa, wanaokerwa na kukosekana usawa, wanaokereka na mihimili ya utawala kutokuwapo huru, nk, kila kundi na kero zake.

Uzi huu unaangazia sekta ya usafirishaji kama kiwakilishi kimoja kati ya mamia kwa maelfu ya makundi yanayoyoweza kujitambulisha kama sekta.

Hakuna popote katika uzi mzima palipolenga kundi moja rasmi kama wanasiasa. Hata hivyo kwa kuwatambua wanasiasa nao kama sekta wamejumuishwa ili kuweza kuwarejea, imetambuliwa sekta zote kuhitaji katiba mpya wakiwamo wao.

Kuinyanyapaa sekta yoyote kwa kumtumia mtu au kikundi fulani cha watu ili kuhalalisha hoja, huko ni kutafuta visingizio uchwara visivyoweza kuwa na mashiko.

Mada inaongelea sekta zote kuhitaji katiba mpya.

Twaweza wamegongelea na nyundo:

TWAWEZA: Katika Watanzania watatu , Wawili wanataka Katiba Mpya

Labda utueleze sekta ipi isiyohitaji katiba mpya kama hukubaliani na hoja.
 
Mlisemea wapi hayo na mkiwa na nani mjumbe mpya?

Mada umeielewa lakini?

Kama dereva wa gari la biashara anahitaji katiba mpya sekta ipi haina uhitaji huo?

Hali kadhalika usisahau vyama vya siasa ni sekta pia katika ujumuishi wake.
Vyama vya siasa mtaaalikwa tuuu kama ikitokea. Lazima katiba ijengwe na wananchi wasio na mlengo wa kisiasa, ili wananchi wawe na uwezo wa kuvijadili vyama hivyo namna ya kuvimiliki. Katiba ni mama wa vyama vya siasa vyote na si vyama vya siasa kudai katiba ya wananchi.
 
Shukuru basi japo kwa kukukaribu mgeni?

Nikirejea kwenye mada - sekta zote zinahitaji katiba mpya wakiwamo madereva wa lori sembuse nani basi?

Sekta gani wewe upo tufanye tathmini kama yenu haihitaji?

Bila shaka Sirro na wale nduguze wanajulikana kuwa hawahitaji katiba mpya kata kata.
 
Harakati za katiba mpya zimeshachafuliwa na vijana wa ufipani. Hivyo jambo hili lisitishwe mara moja
 
Back
Top Bottom