Ambagile anasema kuwa anaona itakuwa ngumu sana kupata katiba mpya kwa sababu anaona vyama vya siasa vimeanza kugombea agenda kuwa hiyo agenda ya Katiba ni ya chama fulani, anasema Katiba mpya ni ya Watanzania na Si ya CCM, CHADEMA, Waislam, Wakristo, Simba au Yanga.
Anasema ni kama tunaanza ushindani wa nani alileta Agenda na mwisho watasema wao ndio wamiliki na kuandika vitu kwa matakwa yao na si ya Jamii.
Anaongeza kuwa agenda hii inaonekana kama ni ya wanasiasa na si wananchi kwa sababu haoni vyama vya wafanyakazi, wakulima nk wakidai katiba mpya ila ni wanasiasa pekee kitu ambacho si afya.
Anasema katiba mpya ni mali ya watanzania na inapaswa kuwa agenda ya Watanzania wote kwa sababu kila mtu anataka katiba mpya .
Credit: Wasafi FM